< Ezekieli 2 >
1 Akanambia, “Mwana wa adamu, simama kwa miguu yako; kisha nitaongea na wewe.”
他对我说:“人子啊,你站起来,我要和你说话。”
2 Kisha, alipokuwa akiongea na mimi, Roho akaingia ndani yangu na ikaniweka kwenye miguu yangu, na nikamsikia akiongea na mimi.
他对我说话的时候,灵就进入我里面,使我站起来,我便听见那位对我说话的声音。
3 Akanambia, “Mwana wa adamu, nakutuma kwa watu wa Israeli, kwa mataifa yanayoasi ambayo yameasi dhidi yangu-wote wao na babu zao wameasi juu yangu hata hivi leo!
他对我说:“人子啊,我差你往悖逆的国民以色列人那里去。他们是悖逆我的,他们和他们的列祖违背我,直到今日。
4 Vizazi vyao vina sura za kikaidi na mioyo migumu. Nakutuma wewe kwenda kwao, na utawaambia, 'Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.'
这众子面无羞耻,心里刚硬。我差你往他们那里去,你要对他们说:主耶和华如此说。
5 Labda watasikia au hawatasikia. Ni nyumba za uasi, lakini angalau watajua kwamba nabii alikuwa miongoni mwao.
他们或听,或不听,(他们是悖逆之家),必知道在他们中间有了先知。
6 Wewe, mwanadamu, usiwaogope au maneno yao. Usiogope, ingawa utakuwa pamoja na mitemba na miiba na ijapokuwa unaishi na nge. Usiogope maneno yao au kuvunjika moyo kwa nyuso zao, kwa kuwa ni nyumba zenye kuasi.
人子啊,虽有荆棘和蒺藜在你那里,你又住在蝎子中间,总不要怕他们,也不要怕他们的话;他们虽是悖逆之家,还不要怕他们的话,也不要因他们的脸色惊惶。
7 Lakini utawaambia maneno yangu, labda watasikia au hapana, kwa sababu ni waasi mno.
他们或听,或不听,你只管将我的话告诉他们;他们是极其悖逆的。
8 Lakini wewe, mwanadamu, silikiliza kile nisemacho kwako. Usiwe muasi kama nyumba za uasi. Fungua mdomo wako na ule kile ninachotaka kukupa!”
“人子啊,要听我对你所说的话,不要悖逆像那悖逆之家,你要开口吃我所赐给你的。”
9 Kisha nikaona, na mkono ulikuwa umenyooshwa kwangu; ndani yake kulikuwa na hati ya kukunja.
我观看,见有一只手向我伸出来,手中有一书卷。
10 Akaikinjua mbele yangu; ilikuwa imeandikwa pande zote mbele na nyuma, na yalikuwa yameandikwa maombolezo kwenye hiyo hati ya kukunja, na huzuni, na ole.
他将书卷在我面前展开,内外都写着字,其上所写的有哀号、叹息、悲痛的话。