< Ezekieli 18 >

1 Neno la Yahwe likanijia tena, kusema,
וַיְהִי דְבַר־יְהֹוָה אֵלַי לֵאמֹֽר׃
2 “Je mnamaana gani, ninyi mliotumia hii mithali kuhusiana na nchi ya Israeli na kusema, 'Wababa wamekula zabibu mbichi, na meno ya watoto imetiwa ganzi'?
מַה־לָּכֶם אַתֶּם מֹֽשְׁלִים אֶת־הַמָּשָׁל הַזֶּה עַל־אַדְמַת יִשְׂרָאֵל לֵאמֹר אָבוֹת יֹאכְלוּ בֹסֶר וְשִׁנֵּי הַבָּנִים תִּקְהֶֽינָה׃
3 Kama nishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-bila shaka hakutakuwa na fursa yoyote tena kwa ajili yenu kuitumia hii mithali katika Israeli.
חַי־אָנִי נְאֻם אֲדֹנָי יֱהֹוִה אִם־יִהְיֶה לָכֶם עוֹד מְשֹׁל הַמָּשָׁל הַזֶּה בְּיִשְׂרָאֵֽל׃
4 Tazama! Kila uhai ni mali yangu-uhai wa baba na uhai wa mwana pia, ni mali yangu! roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa!
הֵן כׇּל־הַנְּפָשׁוֹת לִי הֵנָּה כְּנֶפֶשׁ הָאָב וּכְנֶפֶשׁ הַבֵּן לִי־הֵנָּה הַנֶּפֶשׁ הַחֹטֵאת הִיא תָמֽוּת׃
5 Itasemwaje kuhusu mtu mwenye haki na achukuaye yaliyo halali na haki-
וְאִישׁ כִּֽי־יִהְיֶה צַדִּיק וְעָשָׂה מִשְׁפָּט וּצְדָקָֽה׃
6 kama asipokula juu ya milima au kuinua macho yake kwa sananmu za nyumba ya Israeli, na hakumnajisi mke wa jirani yake, wala kumsemesha mwanamke katika kipindi chake cha mwezi, je! Yu mwenye haki?
אֶל־הֶֽהָרִים לֹא אָכָל וְעֵינָיו לֹא נָשָׂא אֶל־גִּלּוּלֵי בֵּית יִשְׂרָאֵל וְאֶת־אֵשֶׁת רֵעֵהוּ לֹא טִמֵּא וְאֶל־אִשָּׁה נִדָּה לֹא יִקְרָֽב׃
7 Je! Itasemwaje kuhusu mtu ambaye hakumkandamiza yeyote, na kumrudisha mdeni wake kwa kile kilichokuwa kimewekwa kwa ajili ya rehani, na hakuiba lakini kuwapatia chakula wenye njaa na kuwafunika uchi kwa nguo, je yu mwenye haki?
וְאִישׁ לֹא יוֹנֶה חֲבֹלָתוֹ חוֹב יָשִׁיב גְּזֵלָה לֹא יִגְזֹל לַחְמוֹ לְרָעֵב יִתֵּן וְעֵירֹם יְכַסֶּה־בָּֽגֶד׃
8 Je! Itasemwaje kuhusu mtu ambaye hakuchukua faida kubwa kwa ile pesa aliyokopa, na hakuchukua faida kubwa kwa kile alichokiuza?
בַּנֶּשֶׁךְ לֹֽא־יִתֵּן וְתַרְבִּית לֹא יִקָּח מֵעָוֶל יָשִׁיב יָדוֹ מִשְׁפַּט אֱמֶת יַעֲשֶׂה בֵּין אִישׁ לְאִֽישׁ׃
9 Amesemwa kwamba amechukua yaliyo halali na kuimarisha uaminifu kati ya watu. Kama huyo mtu akitembea katika sheria zangu na kuzishika hukumu zangu kufanya kwa uaminifu, kisha ahadi kwa ajili ya mtu mwenye haki ni hii: Ataishi hakika! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
בְּחֻקּוֹתַי יְהַלֵּךְ וּמִשְׁפָּטַי שָׁמַר לַעֲשׂוֹת אֱמֶת צַדִּיק הוּא חָיֹה יִֽחְיֶה נְאֻם אֲדֹנָי יֱהֹוִֽה׃
10 Lakini akizaa mwana mnyang'anyi mmwaga damu na kufanya mengi katika haya mambo kama yalivyotajwa hapa,
וְהוֹלִיד בֵּן־פָּרִיץ שֹׁפֵךְ דָּם וְעָשָׂה אָח מֵאַחַד מֵאֵֽלֶּה׃
11 hata kama baba yake hakufanya mojawapo katika haya mambo, lakini akala juu ya milima na akamnajisi mke wa jirani yake, Je! itasemwaje juu yake?
וְהוּא אֶת־כׇּל־אֵלֶּה לֹא עָשָׂה כִּי גַם אֶל־הֶהָרִים אָכַל וְאֶת־אֵשֶׁת רֵעֵהוּ טִמֵּֽא׃
12 Huyu mtu huwakandamiza maskini na wahitaji, na huwakamata na kuwanyang'anya, na hawarudishii dhamana, na huyanua macho yake kwa sanamu na kufanya matendo maovu,
עָנִי וְאֶבְיוֹן הוֹנָה גְּזֵלוֹת גָּזָל חֲבֹל לֹא יָשִׁיב וְאֶל־הַגִּלּוּלִים נָשָׂא עֵינָיו תּוֹעֵבָה עָשָֽׂה׃
13 na hukopesha pesa kwa faida ya juu sana na kufanya faida kubwa juu ya anachokiuza, Je! huyo mtu ataishi? Hakika hataishi! Atakufa hakika na damu yake itakuwa juu yake kwa sababu amefanya haya mambo ya chuki.
בַּנֶּשֶׁךְ נָתַן וְתַרְבִּית לָקַח וָחָי לֹא יִֽחְיֶה אֵת כׇּל־הַתּוֹעֵבוֹת הָאֵלֶּה עָשָׂה מוֹת יוּמָת דָּמָיו בּוֹ יִֽהְיֶֽה׃
14 Lakini Tazama! tuseme kuna mtu aliyezaa mwana, na mwana wake huona dhambi zote za baba yake alizozifanya, na kupitia kuziona, hakuyafanya hayo mambo.
וְהִנֵּה הוֹלִיד בֵּן וַיַּרְא אֶת־כׇּל־חַטֹּאת אָבִיו אֲשֶׁר עָשָׂה וַיִּרְאֶה וְלֹא יַעֲשֶׂה כָּהֵֽן׃
15 Huyo mwana hakula juu ya milima, na hakuinua macho yake kwa sanamu za nyumba ya Israeli, na hakumtia unajisi mke wa jirani yake, Je! itasemwaje juu yake?
עַל־הֶהָרִים לֹא אָכָל וְעֵינָיו לֹא נָשָׂא אֶל־גִּלּוּלֵי בֵּית יִשְׂרָאֵל אֶת־אֵשֶׁת רֵעֵהוּ לֹא טִמֵּֽא׃
16 Yule mwana hakumkandamiza yeyote, au kutwaa dhamana, au kupoteza vitu, lakini badala yake kutoa chakula chake kwa wenye njaa na kuwafunika wenye uchi kwa nguo.
וְאִישׁ לֹא הוֹנָה חֲבֹל לֹא חָבָל וּגְזֵלָה לֹא גָזָל לַחְמוֹ לְרָעֵב נָתָן וְעֵרוֹם כִּסָּה־בָֽגֶד׃
17 Huyo mwana hakumkandamiza yeyote au au kuchukua faida ambayo ni ya juu sana au kufanya manufaa kwa ajili ya mkopo, lakini ameyashika maagizo yangu na kuenenda sawa sawa na sheria zangu; huyo mwana hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake: Ataishi hakika!
מֵעָנִי הֵשִׁיב יָדוֹ נֶשֶׁךְ וְתַרְבִּית לֹא לָקָח מִשְׁפָּטַי עָשָׂה בְּחֻקּוֹתַי הָלָךְ הוּא לֹא יָמוּת בַּעֲוֺן אָבִיו חָיֹה יִֽחְיֶֽה׃
18 Baba yake, kwa kuwa aliwakandamiza wengine kwa nguvu nyingi na kumnyang'anya ndugu yake, na kufanya yasiyo mema miongoni mwa watu wake-tazama, atakufa katika uovu wake.
אָבִיו כִּֽי־עָשַׁק עֹשֶׁק גָּזַל גֵּזֶל אָח וַאֲשֶׁר לֹא־טוֹב עָשָׂה בְּתוֹךְ עַמָּיו וְהִנֵּה־מֵת בַּעֲוֺנֽוֹ׃
19 Lakini ninyi husema, 'Kwa nini mwana asibebe uovu wa baba yake?' Kwa sababu mwana hubeba yaliyo halali na haki na kuzitunza amri zangu; huzifanya. Ataishi hakika!
וַאֲמַרְתֶּם מַדֻּעַ לֹא־נָשָׂא הַבֵּן בַּעֲוֺן הָאָב וְהַבֵּן מִשְׁפָּט וּצְדָקָה עָשָׂה אֵת כׇּל־חֻקּוֹתַי שָׁמַר וַיַּעֲשֶׂה אֹתָם חָיֹה יִֽחְיֶֽה׃
20 Yule atendaye dhambi, ndiye ambaye atakufa. Mwana hatabeba uovu wa baba yake, na baba hatabeba uovu wa mwana wake. Haki ya yule atendaye haki itakuwa juu yakwe mwenyewe, na uovu wa mwenye uovu utakuwa juu yake mwenyewe.
הַנֶּפֶשׁ הַחֹטֵאת הִיא תָמוּת בֵּן לֹֽא־יִשָּׂא ׀ בַּעֲוֺן הָאָב וְאָב לֹא יִשָּׂא בַּעֲוֺן הַבֵּן צִדְקַת הַצַּדִּיק עָלָיו תִּֽהְיֶה וְרִשְׁעַת (רשע) [הָרָשָׁע] עָלָיו תִּֽהְיֶֽה׃
21 Lakini kama mwovu ageukapo kutoka dhambi zake zote alizofanya, na kuzitunza sheria zangu zote na kufanya yaliyo halali na haki, kisha hakika ataishi na hatakufa.
וְהָרָשָׁע כִּי יָשׁוּב מִכׇּל־חַטֹּאתָו אֲשֶׁר עָשָׂה וְשָׁמַר אֶת־כׇּל־חֻקּוֹתַי וְעָשָׂה מִשְׁפָּט וּצְדָקָה חָיֹה יִֽחְיֶה לֹא יָמֽוּת׃
22 Makosa yote aliyoyafanya hayatakumbukwa juu yake. Ataishi kwa hiyo haki aliyoitenda.
כׇּל־פְּשָׁעָיו אֲשֶׁר עָשָׂה לֹא יִזָּכְרוּ לוֹ בְּצִדְקָתוֹ אֲשֶׁר־עָשָׂה יִֽחְיֶֽה׃
23 Je! Nitafurahia juu ya kifo cha mwovu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-na sio katika kugeuka kwake kutoka njia yake ili kwamba aweze kuishi?
הֶחָפֹץ אֶחְפֹּץ מוֹת רָשָׁע נְאֻם אֲדֹנָי יֱהֹוִה הֲלוֹא בְּשׁוּבוֹ מִדְּרָכָיו וְחָיָֽה׃
24 Lakini kama mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye haki yake na kufanya maovu na kutenda machukizo kama machukizo yote ambayo mtu mwovu afanyayo, basi ataishi? Haki yake yote aliyoifanya haitakumbukwa wakati atakaponisaliti katika uhaini wake. Hivyo atakufa katika dhambi alizofanya.
וּבְשׁוּב צַדִּיק מִצִּדְקָתוֹ וְעָשָׂה עָוֶל כְּכֹל הַתּוֹעֵבוֹת אֲשֶׁר־עָשָׂה הָרָשָׁע יַעֲשֶׂה וָחָי כׇּל־צִדְקֹתָו אֲשֶׁר־עָשָׂה לֹא תִזָּכַרְנָה בְּמַעֲלוֹ אֲשֶׁר־מָעַל וּבְחַטָּאתוֹ אֲשֶׁר־חָטָא בָּם יָמֽוּת׃
25 Lakini ninyi husema, 'Njia ya Bwana si sawa!' sikilizeni, nyumba ya Israeli! Je njia zangu haziko sawa? Je si njia ambazo haziko sawa?
וַאֲמַרְתֶּם לֹא יִתָּכֵן דֶּרֶךְ אֲדֹנָי שִׁמְעוּ־נָא בֵּית יִשְׂרָאֵל הֲדַרְכִּי לֹא יִתָּכֵן הֲלֹא דַרְכֵיכֶם לֹא יִתָּכֵֽנוּ׃
26 Wakati mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye makosa yake, na kufanya maovu na kufa kwa sababu ya hayo, kisha atakufa katika uovu ambao alioufanya.
בְּשׁוּב־צַדִּיק מִצִּדְקָתוֹ וְעָשָׂה עָוֶל וּמֵת עֲלֵיהֶם בְּעַוְלוֹ אֲשֶׁר־עָשָׂה יָמֽוּת׃
27 Lakini wakati mtu mwovu ageukapo kutoka uovu wake alioufanya na kufanya yaliyo halali na haki, kisha ataulinda uhai wake.
וּבְשׁוּב רָשָׁע מֵֽרִשְׁעָתוֹ אֲשֶׁר עָשָׂה וַיַּעַשׂ מִשְׁפָּט וּצְדָקָה הוּא אֶת־נַפְשׁוֹ יְחַיֶּֽה׃
28 Kwa kuwa ameona na kugeuka kutokana na makosa yake yote ambayo aliyoyafanya. Hakika ataishi, na hatakufa.
וַיִּרְאֶה (וישוב) [וַיָּשׇׁב] מִכׇּל־פְּשָׁעָיו אֲשֶׁר עָשָׂה חָיוֹ יִֽחְיֶה לֹא יָמֽוּת׃
29 Lakini nyumba ya Israeli husema, 'Njia ya Bwana haiko sawa!' Ni namna gani njia zangu si sawa, nyumba ya Israeli? Ni njia zenu ndizo si sawa.
וְאָֽמְרוּ בֵּית יִשְׂרָאֵל לֹא יִתָּכֵן דֶּרֶךְ אֲדֹנָי הַדְּרָכַי לֹא יִתָּֽכְנוּ בֵּית יִשְׂרָאֵל הֲלֹא דַרְכֵיכֶם לֹא יִתָּכֵֽן׃
30 Kwa hiyo nitamuhukumu kila mtu miongoni mwenu kulingana na njia zake, nyumba ya Israeli! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo. Tubuni na rudini kutoka kwenye makosa yenu yote ili kwamba wasiwe kikwazo cha uovu dhidi yenu.
לָכֵן אִישׁ כִּדְרָכָיו אֶשְׁפֹּט אֶתְכֶם בֵּית יִשְׂרָאֵל נְאֻם אֲדֹנָי יֱהֹוִה שׁוּבוּ וְהָשִׁיבוּ מִכׇּל־פִּשְׁעֵיכֶם וְלֹא־יִהְיֶה לָכֶם לְמִכְשׁוֹל עָוֺֽן׃
31 Tupilia mbali makosa yenu yote mliyoyafanya; jifanyieni moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, nyumba ya Israeli?
הַשְׁלִיכוּ מֵעֲלֵיכֶם אֶת־כׇּל־פִּשְׁעֵיכֶם אֲשֶׁר פְּשַׁעְתֶּם בָּם וַעֲשׂוּ לָכֶם לֵב חָדָשׁ וְרוּחַ חֲדָשָׁה וְלָמָּה תָמֻתוּ בֵּית יִשְׂרָאֵֽל׃
32 Kwa kuwa sifurahii kifo cha yule afaye-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-hivyo tubuni na muishi!”
כִּי לֹא אֶחְפֹּץ בְּמוֹת הַמֵּת נְאֻם אֲדֹנָי יֱהֹוִה וְהָשִׁיבוּ וִֽחְיֽוּ׃

< Ezekieli 18 >