< Ezekieli 14 >

1 Baadhi ya viongozi wa Israeli wakaja kwangu na kuketi mbele yangu.
Baadhi ya wazee wa Israeli walinijia na kuketi mbele yangu.
2 Ndipo neno la Yahwe likanijia, likisema,
Ndipo neno la Bwana likanijia kusema:
3 “Mwanadamu, hawa watu wamchukua sanamu zao kwenye mioyo yao na kuweka pingamizi la uovu wao mbele ya nyuso zao wenyewe. Je naweza kuulizwa yote na wao?
“Mwanadamu, watu hawa wameweka sanamu katika mioyo yao na kuweka vitu viovu vya kukwaza mbele ya macho yao. Je, kweli niwaruhusu waniulize jambo lolote?
4 Kwa hiyo watangazie hivi na waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Kila mtu wa nyumba ya Israeli achukuaye sanamu moyoni mwake, au awekeye pingamizi la uovu mbele ya uso wake, na kisha yule ajaye kwa nabii-Mimi, Yahwe, nitamjibu kulingana na sanamu zake.
Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Wakati Mwisraeli yeyote anapoweka sanamu moyoni mwake na kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akaenda kwa nabii, Mimi Bwana nitamjibu peke yangu sawasawa na ukubwa wa ibada yake ya sanamu.
5 Nitafanya hivi ili kwamba niweze kuirudisha nyumba ya Israeli katika mioyo yao ambayo ilikuwa mbali nami kwa ajili ya sanamu zao.'
Nitafanya jambo hili ili kukamata tena mioyo ya watu wa Israeli, ambao wote wameniacha kwa ajili ya sanamu zao.’
6 Kwa hiyo sema kwa nyumba ya Israeli, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tubuni na rudini kutoka kwenye sanamu zenu! Rudisheni nyuma nyuso zenu kutoka kwenye kachukizo yenu yote.
“Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Tubuni! Geukeni kutoka kwenye sanamu zenu na mkatae matendo yenu yote ya machukizo!
7 Kwa kuwa kila mmoja kutoka kwenye nyumba ya Israeli na kila mmoja wa wageni wanaoishi katika Israeli ajitengaye nami, achukuaye sanamu zake kwenye moyo wake na kuweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake mwenyewe, na kisha yule ajaye kwa nabii kunitafuta-mimi, Yahwe, nitamjibu mimi mwenyewe.
“‘Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote anayeishi katika Israeli anapojitenga nami na kujiwekea sanamu katika moyo wake na kwa hivyo kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akamwendea nabii kuuliza shauri kwangu, mimi Bwana nitamjibu mwenyewe.
8 Hivyo nitauweka uso wangu juu ya huyo mtu na kumfanya ishara na mithali, kwa kuwa nitamkata kutoka kati ya watu wangu, na mtajua kuwa mimi ni Yahwe.
Nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na kumwadhibu na kumfanya ishara kwa watu. Nitamkatilia mbali kutoka watu wangu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.
9 Kama nabii atadanganywa na kuongea ujumbe, kisha Mimi Yahwe, nitamdanganya huyo nabii; Nitanyoosha mkono wangu na kumwangamizaku toka kati watu wangu Israeli.
“‘Naye nabii kama atakuwa ameshawishika kutoa unabii, Mimi Bwana nitakuwa nimemshawishi nabii huyo, nami nitaunyoosha mkono wangu dhidi yake na kumwangamiza kutoka miongoni mwa watu wangu Israeli.
10 Watabeba uovu wao wenyewe; uwovu wa nabii utakua uleule kama uovu wa yule aulizaye kutoka kwake.
Watachukua hatia yao, nabii atakuwa na hatia sawa na yule mtu aliyekuja kuuliza neno kwake.
11 Kwa sababu hiyo basi, nyumba ya Israeli haitaenda mbali kutoka kunifuata mimi wala kujinajisi wenyewe kupitia dhambi zao zote. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao-hivi ndivyo Yahwe asemavyo.”'
“‘Ndipo watu wa Israeli hawataniacha tena, wala kujitia unajisi tena kwa dhambi zao zote. Ndipo watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao, asema Bwana Mwenyezi.’”
12 Kisha neno la Yahwe likanijia, likisema,
Neno la Bwana likanijia kusema,
13 “Mwanadamu, wakati nchi itakapo asi dhidi yangu kwa kufanya dhambi ili kwamba ninyooshe mkono wangu dhidi yake na kuvunja tegemea la mkate wake, na kuleta njaa juu yake na kukata mnyama kutoka kwenye nchi;
“Mwanadamu, kama nchi itanitenda dhambi kwa kutokuwa waaminifu nami nikinyoosha mkono wangu dhidi yake kukatilia mbali upatikanaji wake wa chakula na kuipelekea njaa na kuua watu wake na wanyama wao,
14 kisha hata kama hawa watu watatu-Nuhu, Danieli, na Ayubu-walikuwa katikati ya nchi, wangeweza kuokoa maisha yao wenyewe kwa haki-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
hata kama watu hawa watatu: Noa, Danieli na Ayubu wangekuwa ndani ya nchi hiyo, ndio hao tu wangeweza kujiokoa wenyewe kwa uadilifu wao, asema Bwana Mwenyezi.
15 Kama nikileta wanyama waovu kwenye nchi na kuwafanya wasizae hivyo basi itakuwa hakuna mtu asiweze kupita kwa sababu ya hao wanyama,
“Au kama nikipeleka wanyama pori katika nchi hiyo yote na kuifanya isiwe na watoto, nayo ikawa ukiwa kwamba hakuna mtu apitaye katika nchi hiyo kwa sababu ya wanyama pori,
16 kisha hata kama watu hawa hawa watatu ndani yake-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuwaokoa hata watoto wao wala binti; isipokuwa maisha yao yataokoka, lakini nchi itakuwa ukiwa.
hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao peke yao wangeokolewa, lakini nchi ingekuwa ukiwa.
17 Au nikileta upanga juu ya hiyo nchi na kusema, 'Upanga, nenda kwenye nchi na wakate wote mtu na mnyama kutoka huo',
“Au kama nikileta upanga dhidi ya nchi hiyo na kusema, ‘Upanga na upite katika nchi yote,’ nami nikiua watu wake na wanyama wao,
18 kisha hata kama hawa watu watatu watakuwa katikatai ya nchi-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuwaokoa japo watoto wao wala binti; ila tu maisha yao wenyewe yangeokolewa.
hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao wenyewe tu wangeokolewa.
19 Au kama nikipeleka tauni juu ya nchi na kumwaga dhahabu yangu juu yake kwa damu, ili kuwakata mtu na mnyama,
“Au kama nikipeleka tauni katika nchi hiyo na kumwaga ghadhabu yangu juu yake kwa njia ya kumwaga damu, kuua watu wake na wanyama wao,
20 kisha hata kama Nuhu, Danieli, na Ayubu wangekuwa kwenye hiyo nchi-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuokoa hata watoto wao au binti; maisha yao pekee yangeokoka kwa haki.
hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hata kama Noa, Danieli na Ayubu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kumwokoa mwana wala binti. Wao wangeweza kujiokoa wenyewe tu kwa uadilifu wao.
21 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: hakika nitafanya mambo makali sana kwa kuleta adhabu zangu nne-njaa, upanga, wanyama wa porini, na tauni-juu ya Yerusalemu kuwakata wote mtu na mnyama kutoka kwake.
“Kwa maana hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Itakuwa vibaya kiasi gani nitakapopeleka dhidi ya Yerusalemu hukumu zangu nne za kutisha, yaani, upanga, njaa, wanyama pori na tauni, ili kuua watu wake na wanyama wao!
22 Kisha, tazama! mabaki yatasalia kwake, watakaokoka wataenda pamoja na wana na binti. Tazama! Watawatokea, na mtaona njia zao na matendo yao yakiwafariji kuhusu adhabu niliyoipeleka Yerusalemu, na kuhusu kila kitu kingine ambacho nilichopeleka juu ya nchi.
Lakini watakuwepo wenye kuokoka, wana na binti wataletwa kutoka nje ya nchi hiyo. Watawajia ninyi, nanyi mtakapoona mwenendo wao na matendo yao, mtafarijika kuhusu maafa niliyoleta juu ya Yerusalemu, kwa ajili ya yale yote niliyoleta juu yake.
23 Waliokoka watawafariji ninyi mtakapoona njia zao na matendo yao, hivyo mtayajua haya mambo niliyoyafanya juu yake, kwamba sijayafanya bure! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”
Mtafarijika wakati mtakapoona mwenendo wao na matendo yao, kwa kuwa mtajua kwamba sikufanya lolote ndani yake bila sababu, asema Bwana Mwenyezi.”

< Ezekieli 14 >