< Ezekieli 1 >
1 Katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, na siku ya tano ya mwezi, ikawa kuhusu kwamba nilikuwa nikiishi miongoni mwa wafungwa karibu na Kebari Kanali. Mbingu zilifunguka, na kuona maono ya Mungu.
三十年四月五日,當我在革巴爾河畔,在俘虜之中的時候,天開了,我見了天主的異像,
2 Katika siku ya tano katika mwezi huo-ilikuwa mwaka wa tano wa utumwani wa Mfalme Yehoyakini-
時在耶苛泥雅王充軍後第五年四月五日;
3 Neno la Yahwe likamjia Ezekieli mwana wa Buzi kuhani, katika nchi ya Wakaldayo karibu na Keberi Kanali, na mkono wa Yahwe ulikuwa juu yake hapo.
那時在加色丁地,靠近革巴爾河,上主的話傳給步齊的兒子厄則克耳司祭,上主的手臨於我。
4 Kisha nikaona, kulikuwa na upepo wa dhoruba unakuja kutoka kaskazini; wingu kubwa pamoja na moto wa nuru ndani yake na kung'aa ukizunguka ndani yake, na moto ulikuwa na rangi ya kaharabu ndani ya hilo wingu.
我觀望,看,有一陣暴風由北方吹來,颳來一大塊火光四射的雲彩,雲中有一團旋轉的火,火中有一種發亮的金屬。
5 Katikati kulikuwa na viumbe vinne vinavyofanana. Mwonekano wao ulikuwa hivi: walikuwa wanamfanano wa mtu,
火中似乎有四個活物的形狀,牠們的外表是這樣:都有人的形狀。
6 lakini walikuwa na sura nne kila mmoja, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne.
每個有四種形像,每個有四隻翅膀。
7 Miguu yao ilikuwa imenyooka, lakini nyayo za miguu yao zilikuwa kama kwato za ndama zilizokuwa zinang'aa kama shaba iliyosuguliwa.
牠們的腳是直立的腳,腳掌像牛蹄,發亮像磨光的銅。
8 Bado walikuwa na mikono ya binadamu chini ya mabawa yao chini kwenye pande zote nne. Kwa wote wanne, nyuso zao na mabawa vilikuwa hivi:
在牠們四面的翅膀下邊,都有人手;四個活物各有自己的形像和翅膀。
9 mabawa yao yalikuwa yameungana na kiumbe kingine, na hawakurudi walipokuwa wameenda; badala yake, kila mmoja alienda mbele.
牠們的翅膀互相連接,在行走時不必轉身,各朝著自己的前面行走。
10 Mfanano wa nyuso zao ulikuwa kama uso wa mwanadamu. Wanne hao walikuwa na uso wa simba kwa upande wa kuume. Hao wanne pia walikuwa na uso wa tai.
關於牠們外表的形像:牠們四個的正面都具有人的形像,右邊有獅的形像,左邊牛的形像,背面有鷹的形像。
11 Nyuso zao zilikuwa hivyo, na mabawa yao yalikuwa yametawanyika juu, hivyo basi kila kiumbe kilikuwa na jozi ya za mabawa yaliyokuwa yameshikamana na bawa la kiumbe kingine, na pia jozi za mabawa yaliyokuwa yamefunika miili yao.
牠們的翅膀向上伸開,每個用兩隻翅膀互相連接,用兩隻翅膀遮蔽身體。
12 Kila mmoja alienda mbele, hivyo basi popote Roho alipowaelekeza kwanda, walienda bila kurudi.
每個朝著自己的前面行走;神力催迫牠們往那裏去,牠們就往那裏去;行走時不必轉身。
13 Kama kwa mfanano wa hao viumbe hai, mwonekano wao ulikuwa ni kama kuchoma kaa la moto, kama mwonekano wa nuru; mng'ao wa moto pia ulihama karibu na miongoni mwa viumbe, na kulikuwa na nuru za radi.
在活物中間有壹種相似燃著的炭火,又好似火炬在活物中旋轉。這火有亮光,由火中射出閃光。
14 Hao viumbe hai vilikuwa vikihama mbio mbele na nyuma, na walikuwa na mwonekano wa radi!
活物來回疾馳,好像閃電。
15 Kisha nikawatazama wale viumbe hai; kulikuwa na gurudumu moja juu ya aridhi kando ya vile viumbe hai.
我觀望那些活物時,看,靠近那些活物的四面,在地上各有一個輪子。
16 Huu ndio ulikuwa mwonekano na umbo wa hizo gurudumu: kila gurudumu lilikuwa kama zabarajadi, na manne hayo yalikuwa na mfano mmoja; mwonekano wao na umbo vilikuwa kama gurudumu lililoungana na jingine.
那些輪子及其構造的外表,光澤有如橄欖石,四輪都有同樣的形狀。四輪結構的樣式,好像輪子套在輪子中。
17 Wakati yale magurudumu yalipokuwa yakitembea, yalienda bila kurudi kwenye mwelekeo wowote viumbe vilipokuwa vimeelekea.
輪子轉動時,可向四方旋轉,前行時不必轉轍。
18 Kama kwa upande kingo, walikuwa warefu na wakutisha, kwa upande kingo kulikuwa na macho yamezunguka kote.
輪輞高大,我看見四個輪輞都佈滿了眼睛。
19 Popote vile viumbe hai vilipokuwa vikielekea, yale magurudumu yalielekea karibu nao. Wakati vile viumbe hai vilipoinuka kutoka kwenye nchi, na yale magurudumu yaliinuka pia.
活物行走時,輪子也在牠們旁邊轉動;活物由地面升起時,輪子也升起。
20 Popote Roho alipokwenda, walikwenda, na yale magurudumu yaliinuka karibu nao, roho wa kiumbe hai ilikuwa magurudumu.
神力催迫活物往那裏去,牠們就往神力催迫的方向去;輪子也同時與牠們一起升起,因為活物的神力在輪子內。
21 Popote vile viumbe vilipoelekea, magurudumu pia yalielekea huko; na wakati wale viumbe viliposimama hata hivyo, magurudumu yalisimama bado; wakati viumbe viliposimama kutoka kwenye nchi, magurudumu yalisimama karibu nao, kwa sababu yule roho wa wale viumbe alikuwa kwenye magurudumu.
活物行走,輪子也轉動;活物站住,輪子也停住;活物由地上升起,輪子也隨之升起,因為活物的神力在輪子內。
22 Juu ya vichwa vya wale viumbe hai kulikuwa na mfanano wa anga la kutanuka; ilikuwa inang'aa kama mfano wa barafu juu ya vichwa vyao.
在活物的頭上,有相似穹蒼的東西,好像發亮的水晶,在牠們頭上展開。
23 Chini ya anga, kila mabawa ya kiumbe kimoja yalinyooshwa mbele na kugusana kila mabawa na kiumbe kimoja. Pia kila kiumbe hai kilikuwa na jozi moja kwa ajili ya kujifunika vyenyewe; kila kimoja kilikuwa na jozi moja kwa ajili ya kujifunika mwili wake mwenyewe.
在穹蒼下伸直牠們的翅膀,一隻的翅膀與另一隻的翅膀彼此相接,又各有兩隻翅膀遮蔽著身體。
24 Kisha nikasikia sauti ya mabawa yao. Kama mlio wa maji mengi. Kama sauti ya mwenye enzi popote walipoelekea. Kama sauti ya jeshi. Popote pale waliposimama, walishusha mabawa yao.
當牠們行動時,我聽見翅膀的颯颯聲,像洪水之聲,又像全能者的聲音,又似軍營中的喧噪之聲。當牠們站住時,就歛起翅膀。
25 Sauti ikaja kutoka juu ya anga juu ya vichwa vyao popote waliposimama na kushusha mabawa yao.
那時,由牠們頭頂上的穹蒼那裏,發出一種響聲;活物即站住,就歛起翅膀。
26 Juu ya anga juu ya vichwa vyao kulikuwa na mfanao wa kiti cha enzi ambacho kilikuwa na mwonekano wa jiwe la samawati, na juu mfano wa kiti cha enzi kilifanana kama mwonekano wa mwanadamu.
在她們頭頂上的穹蒼上面,有一塊像藍玉的石頭,有寶座的形狀;在這狀如寶座之上,有一個外貌像人的坐在上頭。
27 Nikaona umbo lenye mwonekano wa chuma chenye kung'aa pamoja na moto ndani yake kutoka kwenye mwonekano wa juu ya nyonga zake juu; Nikaona kutoka kwenye mwonekano wa nyonga zake upande wa chini mwonekano wa moto na mng'ao umezunguka kote.
我望見在他相似腰部的上面,好像有發亮的金屬,內裏和周圍好像一團火。我又望見在相似腰部的下面,好像有火的形狀,周圍有光環繞,
28 Kama mwonekano wa upinde wa mvua kwenye mawingu katika siku ya mvua ulikuwa na mwonekano wa taa iliyowaka imeizunguka. ulikuwa na mwonekano unaofanana na utukufu wa Yahwe. Wakati nilipouona, nilihisi kwenye uso wangu, na nikasikia sauti ikiongea.
環繞在周圍的光,猶如落雨時雲彩中所出現的虹霓。這就是上主的光榮顯現時的奇象。我一看見,就伏地掩面,同時也聽見有一位講話的聲音。