< Kutoka 6 >

1 Kisha Yahweh akasema na Musa, “Sasa utaona nitakacho fanya kwa Farao. Utaona hili, kwa kuwa ata waacha waenda kwa mkono wangu hodari. Kwasababu ya mkono wangu hodari, ata waondoa nje ya nchi.”
Dixitque Dominus ad Moysen: Nunc videbis quae facturus sum Pharaoni: per manum enim fortem dimittet eos, et in manu robusta eiiciet illos de terra sua.
2 Mungu akasema na Musa na kumwambia, “Mimi ni Yahweh.
Locutusque est Dominus ad Moysen dicens: Ego Dominus
3 Nilimtokea Ibrahimu, Isaka, na Yakobo kama Mungu mwenye nguvu; lakini kwa jina langu, Yahweh, sikujuliikana kwao.
qui apparui Abraham, Isaac, et Iacob in Deo omnipotente: et nomen meum ADONAI non indicavi eis.
4 Pia niliimarisha agano langu na wao, ilikuwapatia nchi ya Kanani, nchi walioishi kama sio raia, nchi walio tanga tanga.
Pepigique foedus cum eis, ut darem eis Terram Chanaan, terram peregrinationis eorum, in qua fuerunt advenae.
5 Zaidi ya yote, nimesikia kilio cha Waisraeli ambao wa Misri wame wa chukua watumwa, na nimekumbuka agano langu.
Ego audivi gemitum filiorum Israel, quo Aegyptii oppresserunt eos: et recordatus sum pacti mei.
6 Kisha basi, sema kwa Waisraeli, 'Mimi ni Yahweh. Nitawatoa kwenye utumwa chini ya wa Misri, na kuwaweka huru na nguvu zao. Nitawaokoa kwa kudhihirisha nguvu zangu, na kwa matendo ya ajabu ya hukumu.
Ideo dic filiis Israel: Ego Dominus qui educam vos de ergastulo Aegyptiorum, et eruam de servitute: ac redimam in brachio excelso, et iudiciis magnis.
7 Nitawaleta kwangu kama watu wangu, na nitakuwa Mungu wenu. Mtajua kuwa mimi ndiye Yahweh Mungu wenu, aliye watoa kwenye utumwa chini ya wa Misri.
Et assumam vos mihi in populum, et ero vester Deus: et scietis quod ego sum Dominus Deus vester qui eduxerim vos de ergastulo Aegyptiorum:
8 Nitawaleta kwenye nchi niliyo muahidi kumpa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Nitawapa kama mali yenu. Mimi ni Yahweh.”'
et induxerim in terram, super quam levavi manum meam ut darem eam Abraham, Isaac, et Iacob: daboque illam possidendam vobis, ego Dominus.
9 Musa alipo waambia haya Waisraeli, hawakumsiliza kwasababu ya mateso magumu ya utumwa wao.
Narravit ergo Moyses omnia filiis Israel: qui non acquieverunt ei propter angustiam spiritus, et opus durissimum.
10 Hivyo Yahweh akazungumza na Musa na kumwambia,
Locutusque est Dominus ad Moysen, dicens:
11 “Nenda umwambie Farao, mfalme wa Misri, awaache watu wa Israeli waondoke kwenye nchi yake.”
Ingredere, et loquere ad Pharaonem regem Aegypti, ut dimittat filios Israel de terra sua.
12 Musa akamwambia Yahweh, “Kama Waisraeli hawajanisikiliza mimi, kwa nini Farao anisikillize mimi, tangu mimi sio mzuri wakuzungumza?”
Respondit Moyses coram Domino: Ecce filii Israel non audiunt me: et quo modo audiet Pharao, praesertim cum incircumcisus sim labiis?
13 Yahweh akasema na Musa na Aruni. Akawapa amri ya Waisraeli na Farao, mfalme wa Misri, awatoe Waisraeli kutoka nchi ya Misri.
Locutusque est Dominus ad Moysen et Aaron, et dedit mandatum ad filios Israel, et ad Pharaonem regem Aegypti ut educerent filios Israel de terra Aegypti.
14 Hawa walikuwa vichwa wa nyumba za baba yao: wana wa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa Hanoki, Palu, Hezroni, na Karmi. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Rubeni.
Isti sunt principes domorum per familias suas. Filii Ruben primogeniti Israelis: Henoch et Phallu, Hesron et Charmi.
15 Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Zohari, na Shauli - mwana wa mwanamke wa Kanani. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Simeoni.
hae cognationes Ruben. Filii Simeon: Iamuel et Iamin, et Ahod, et Iachin, et Soar, et Saul filius Chananitidis: hae progenies Simeon.
16 Hapa yameorodheshwa majina ya wana wa Lawi, pamoja na uzo wao. Walikuwa ni Gerishoni, Kohathi, na Merari. Lawi aliishi mpaka alipo kuwa na miaka 137.
Et haec nomina filiorum Levi per cognationes suas: Gerson et Caath et Merari. Anni autem vitae Levi fuerunt centum triginta septem.
17 Wana wa Gerishoni walikuwa Libni na Shimei.
Filii Gerson: Lobni et Semei, per cognationes suas.
18 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na uzieli. Kohathi aliishi hadi miaka 133.
Filii Caath: Amram, et Isaar, et Hebron et Oziel. anni quoque vitae Caath, centum triginta tres.
19 Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi. Hawa walikuja kuwa mababu wa ukoo wa Walawi, pamoja na uzao wao.
Filii Merari: Moholi et Musi. hae cognationes Levi per familias suas.
20 Amramu alimuoa Yokebedi, dada yake baba yake. Alimzalia Aruni na Musa. Amramu aliishi miaka 137 na akafa.
Accepit autem Amram uxorem Iochabed patruelem suam: quae peperit ei Aaron et Moysen. Fueruntque anni vitae Amram, centum triginta septem.
21 Wana wa Izhari walikuwa Kora, Nefegi, na Zikri.
Filii quoque Isaar: Core, et Nepheg, et Zechri.
22 Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elizafani na Sithri.
Filii quoque Oziel: Misael, et Elisaphan et Zethri.
23 Aruni alimuoa Elisheba, binti wa Aminadabu, dada wa Nashoni. Alimzaa Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari.
Accepit autem Aaron uxorem Elisabeth filiam Aminadab, sororem Nahason, quae peperit ei Nadab, et Abiu, et Eleazar, et Ithamar.
24 Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasa. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Wakora.
Filii quoque Core: Aser, et Elcana, et Abiasaph. hae sunt cognationes Coritarum.
25 Eleazari, mwana wa Aruni, alimuoa mmoja wa mabinti Wa Putieli. Alimzalia Fineazi. Hawa walikuwa vichwa wa nyumba za baba yao miongoni mwa Walawi, pamoja na uzao wao.
At vero Eleazar filius Aaron accepit uxorem de filiabus Phutiel: quae peperit ei Phinees. hi sunt principes familiarum Leviticarum per cognationes suas.
26 Hawa wanaume wawili walikuwa Musa na Aruni ambao Yahweh alisema, “Waleteni Waisraeli kutoka nchi ya Misri, kwa makundi ya wanaume wapiganaji.”
Iste est Aaron et Moyses, quibus praecepit Dominus ut educerent filios Israel de Terra Aegypti per turmas suas.
27 Aruni na Musa wakazungumza na Farao, mfalme wa Misri, awaruhusu Waisraeli watoke Misri. Hawa walikuwa Musa na Aruni wale wale.
Hi sunt, qui loquuntur ad Pharaonem regem Aegypti, ut educant filios Israel de Aegypto: iste est Moyses et Aaron,
28 Pale Yahweh alipo zungumza na Musa katika nchi ya Misri,
in die qua locutus est Dominus ad Moysen, in Terra Aegypti.
29 alimwambia, “Mimi ni Yahweh. Sema kwa Farao, mfalme wa MIsri, kila kitu nitacho kwambia.”
Et locutus est Dominus ad Moysen, dicens: Ego Dominus: loquere ad Pharaonem regem Aegypti, omnia quae loquor tibi.
30 Lakini Musa alimwambia Yahweh, “Mimi sio mzuri wa kuongea, hivyo kwanini Farao anisikilize mimi?”
Et ait Moyses coram Domino: En incircumcisus labiis sum, quo modo audiet me Pharao?

< Kutoka 6 >