< Kutoka 32 >
1 Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Aruni, wakamwambia, “Njoo, katufanyizie sanamu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.”
И видевше людие, яко умедли Моисей снити с горы, восташа людие на Аарона и глаголаша ему: востани и сотвори нам боги, иже пойдут пред нами: Моисей бо сей человек, иже изведе нас от земли Египетския, не вемы, что бысть ему.
2 Hivyo Aruni akawaambia, “Zitoeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee.”
И рече им Аарон: измите усерязи златыя, яже во ушесех жен ваших и дщерей, и принесите ко мне.
3 Watu wote wakavua pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, na wakamletea Aruni.
И изяша вси людие усерязи златы, яже во ушесех жен их, и принесоша ко Аарону.
4 Akapoke mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha. Nao wakasema, “Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.”
И взя от рук их и слия их делом литым, и сотвори им телца литаго. И рекоша: сии бози твои, Израилю, иже изведоша тя из земли Египетския.
5 Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Aruni akatangaza akasema,
И видев Аарон, созда олтарь прямо ему, и проповеда Аарон, глаголя: праздник Господнь утре.
6 “Kesho itakuwa sikukuu kwa Yahweh.” Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze.
И обутреневав наутрие, вознесе всесожжения и принесе жертву спасения. И седоша людие ясти и пити и восташа играти.
7 Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Shuka upesi, kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao.
И рече Господь к Моисею глаголя: иди скоро, сниди отсюду, беззаконноваша бо людие твои, ихже извел еси из земли Египетския:
8 Wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu. Wakasema, 'Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.
преступиша с пути скоро, егоже заповедал еси им: сотвориша себе телца, и поклонишася ему, и пожроша ему, и реша:
9 Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu.
сии бози твои, Израилю, иже изведоша тя из земли Египетския:
10 Basi sasa usinizuie. Ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize. Nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.”
и ныне остави Мя, и возярився гневом на ня, потреблю их, и сотворю тя в язык велик.
11 Musa akamsihi sana Yahweh Mungu wake, na kusema,”Yahweh, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?
И помолися Моисей пред Господем Богом и рече: вскую, Господи, яришися гневом на люди Твоя, ихже извел еси из земли Египетския крепостию великою и мышцею Твоею высокою?
12 Kwa nini Wamisri kusema, 'Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi?' Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.
Да не когда рекут Египтяне, глаголюще: с лукавством изведе их погубити в горах и потребити их от земли: утоли гнев ярости Твоея и милостив буди о злобе людий Твоих,
13 Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, 'Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.'”
помянув Авраама и Исаака и Иакова, Твоя рабы, имже клялся еси Собою, и рекл еси к ним, глаголя: зело умножу семя ваше, яко звезды небесныя множеством, и всю сию землю, юже рекл еси дати семени их, и обладают ею во веки.
14 Na Yahweh akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake.
И умилостивися Господь о зле, еже рече сотворити людем Своим.
15 Kisha Musa akageuka akashuka katika mlima, na zile mbao mbili za mawe mikononi mwake. Mbao zilizoandikwa pande zote mbili, upande huu na upande huu ziliandikwa.
И возвратився Моисей, сниде с горы: и две скрижали свидения в руку его, скрижали каменны написаны от обою страну их, сюду и сюду быша написаны:
16 Na zile mbao zilikuwa kazi ya Mungu nayo maandiko yalikuwa maandiko ya Mungu, yaliyochorwa katika zile mbao.
и скрижали дело Божие быша, и написание, написание Божие изваяно на скрижалех.
17 Na Yoshua aliposikia kelele za watu walipokuwa wakipiga kelele, akamwambia Musa, “Kuna kelele ya vita kambini.
И услышав Иисус глас людий кричащих, рече к Моисею: глас ратный в полце.
18 “Lakini Musa akasema, “Hiyo si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushinda vitani, wala si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushindwa; bali kelele za watu waimbao ndizo ninazozisikia mimi.”
И рече Моисей: несть глас начинающих одолевати, ниже глас начинающих бежати, но глас начинающих напиватися вином аз слышу.
19 Hata alipoyakaribia kambini akaiona ile ndama, na watu wakicheza. Hasira ya Musa ikawaka. Akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima.
И егда приближашеся к полку, узре телца и лики: и возярився гневом Моисей, поверже из руку своею обе скрижали, и сокруши я под горою:
20 Akaitwaa ile ndama waliyoifanya, akaichoma moto, akaisaga hata ikawa mavumbi, akainyunyiza juu ya maji. Akawanywesha wana wa Israeli.
и взем телца, егоже сотвориша, сожже его во огни и сотре его подробну, и разсыпа его по воде, и напои ею сыны Израилевы.
21 Musa akamwambia Aruni, “Watu hawa wamekufanyani hata ukaleta dhambi hii kuu juu yao?
И рече Моисей Аарону: что сотвориша тебе людие сии, яко навел еси на них грех велик?
22 Aruni akasema, “Hasira yako isiwake, bwana wangu. Wewe unawajua watu hawa, ya kuwa wamejielekeza kwa mabaya.
И рече Аарон к Моисею: не гневайся, господине: ты бо веси людий сих устремление.
23 Maana waliniambia, 'Katufanyie miungu, itakayokwenda mbele yetu. Kwa maana mtu huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui yaliyompata.'
Глаголаша бо ми: сотвори нам боги, иже пойдут пред нами: Моисей бо сей человек, иже изведе ны от Египта, не вемы, что бысть ему:
24 Nikawaambia, 'Mtu ye yote aliye na dhahabu na aivue; basi wakanipa, nami nikaitupa ndani ya moto, akatoka ndama huyu.”
и рекох им: иже имать злато, измите: и изяша, и даша мне, и ввергох е во огнь, и излияся телец сей.
25 Basi Musa alipoona ya kuwa watu hawa wameasi (maana Haruni amewaacha waasi, ili wawe dhihaka kati ya adui zao)
Видев же Моисей люди, яко разделишася, раздели бо их Аарон в порадование супостатом их:
26 Ndipo Musa akasimama katika mlango wa marago, akasema, “Mtu awaye yote aliye upande wa Yahweh na aje kwangu.” Wana wa Lawi wote wakamkusanyikia.
ста же Моисей во вратех полка и рече: аще кто есть Господнь, да идет ко мне. Снидошася убо к нему вси сынове Левиины.
27 Akawaambia, Yahweh, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake.'”
И рече им: сия глаголет Господь Бог Израилев: препояшите кийждо свой мечь при бедре и пройдите, и возвратитеся от врат до врат сквозе полк, и убийте кийждо брата своего и кийждо ближняго своего и кийждо соседа своего.
28 Na hao wana wa Lawi wakafanya kama vile alivyosema Musa, wakaanguka siku ile kama watu elfu tatu.
И сотвориша сынове Левиины, якоже глагола им Моисей: и паде от людий в той день до трех тысящ мужей.
29 Musa akasema, Jiwekeni wakfu kwa Yahweh leo, kila mtu juu ya mwanawe na juu ya ndugu yake; ili Yahweh awape baraka leo.”
И рече им Моисей: наполнисте руки вашя днесь Господу, кийждо в сыне своем и в брате своем, да дастся на вас благословение.
30 Hata asubuhi yake Musa akawaambia watu, “Mmetenda dhambi kuu. Sasa nitakwenda juu kwa Yahweh. Labda nitafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu.”
И бысть на утрие, рече Моисей к людем: вы согрешисте грех велик: и ныне взыду к Богу, да умолю о гресе вашем.
31 Musa akarejea kwa Yahweh akasema,” Oh! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu.
И возвратися Моисей ко Господу и рече: молюся ти, Господи: согрешиша людие сии грех велик и сотвориша себе боги златы:
32 Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao – na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika.”
и ныне, аще убо оставиши им грех их, остави: аще же ни, изглади мя из книги Твоея, в нюже вписал еси.
33 Yahweh akamwambia Musa, “Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.
И рече Господь к Моисею: аще кто согреши предо Мною, изглажу его из книги Моея:
34 Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake. Tazama, malaika wangu atakutangulia. Lakini pamoja na hayo siku nitakayowajilia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao.”
ныне же иди, сниди и возведи люди сия на место, еже рех тебе: се, Ангел Мой предидет пред лицем твоим: в оньже день присещу, наведу на них грех их.
35 Kisha Yahweh akawapiga hao watu, kwa walivyoifanya ile ndama, ambayo Aruni aliifanya.
И порази Господь люди за сотворение телца, егоже сотвори Аарон.