< Kutoka 30 >
1 Nawe fanya madhabahu ya kufukizia uvumba; utaifanyiza kwa mti wa mshita.
你應做焚香的壇,用皂莢木製造,
2 Urefu wake utakuwa dhiraa moja, na upana wake dhiraa moja; itakuwa mraba; na kwenda juu kwake dhiraa mbili; pembe zake zitakuwa za kitu kimoja nayo.
長一肘,寬一肘,方形,高二肘,四角從壇上突出。
3 Nawe utaifunikiza dhahabu safi juu yake - na mbavu zake kando kando, na pembe zake. Nawe utaifanyia ukingo wa dhahabu kuizunguka.
壇、壇的上面、四壁、周圍和四角,都包上純金;壇周圍做上金花邊。
4 Kisha utaifanyia pete mbili za dhahabu, chini ya ukingo wake katika mbavu zake mbili, katika pande zake mbili utazifanya; nazo zitakuwa mahali pa kuitia miti ya kuichukulia madhabahu.
壇兩側花邊下,做兩個金環,兩面都做,為穿紅桿,抬香壇之用。
5 Na ile miti utaifanya kwa mti wa mshita, na kuifunikiza dhahabu safi.
用皂莢木做兩根紅桿包上金。
6 Nawe utaitia mbele ya lile pazia lililo karibu na sanduku la ushuhuda mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, hapo nitakapokutana nawe.
把香壇安置在約櫃前面掛的帳幔前,就是在我與你會晤的約櫃上的贖罪蓋之前。
7 Na Aruni atafukiza uvumba wa manukato juu yake; kila siku asubuhi. Atakapozitengeneza zile taa, ataufukiza,
亞郎要在壇上焚燒香料;每天早晨整理燈盞時要焚香;
8 na Aruni atakapoziwasha zile taa wakati wa jioni, ataufukiza, uwe uvumba wa daima mbele za Yahweh katika vizazi vyenu vyote.
晚間亞郎換放燈盞時也要焚香:這是你們世世代代在上主前不斷的焚香禮。
9 Hamtafukiza juu yake uvumba mgeni, wala sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, wala hamtamimina juu yake sadaka ya kinywaji.
在這壇上不准焚別的香,也不准獻全燔祭和素祭或奠祭。
10 Naye Aruni atafanya upatanisho juu ya pembe zake mara moja kila mwaka. Kwa damu ya ile sadaka ya dhambi ya kufanya upatanisho, mara moja kila mwaka ataifanyia upatanisho, katika vizazi vyenu vyote. Ni takatifu sana kwa Yahweh.”
亞郎每年一次為這壇的四角上行贖罪禮,用贖罪祭贖罪犧牲的血,每年一次為這壇行贖罪禮。你們世世代代應行此禮,將壇祝聖於上主為至聖之物。」造會幕的人丁稅
11 BWANA akanena na Musa,
上主訓示梅瑟說:「
12 “Utakapowahesabu wana wa Israeli, kama itakavyotokea hesabu yao, ndipo watakapompa BWANA kila mtu ukombozi kwa ajili ya roho yake, hapo utakapowahesabu; ili kwamba yasiwe maradhi kati yao, hapo utakapowahesabu.
當你統計以色列子民人數的時候,凡被統計的人,每人應獻給上主贖命金,免得在統計的時候,災禍降在他們身上。
13 Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa atatoa nusu shekeli kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu; (shekeli ni gera ishirini). Nusu shekeli kwa sadaka ya Yahweh.
凡被統計過的,每人應按聖所的衡量繳納半「協刻耳,」─一「協刻耳」等於二十「革辣,」─這半「協刻耳」是給上主的獻儀。
14 Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa tangu huyo ambaye umri wake ni miaka ishirini, au zaidi, atatoa hiyo sadaka kwangu.
凡被統計過的,自二十歲以上起,要獻給上主獻儀:
15 Watu watakapo leta hii sadaka kwangu kufanya upatananisho, matajiri hawataleta zaidi, wala maskini hawataleta kilichopungua katika hiyo nusu shekeli.
富的不多納,窮的也不少,一概出半「協刻耳,」給上主作獻儀,作你們的贖命金。
16 Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania. Ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele yangu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
你從以色列子民所取得的贖命金,應拿來為會幕用。這是子民在上主前是一個記念,也贖回了你們的性命。」銅盆
17 Yahweh akamwambia Musa,
上主訓示梅瑟說:「
18 “Fanya na birika la shaba, na tako lake la shaba, ili kuogea; nawe utaliweka kati ya hema ya kukutania na madhabahu, nawe utalitia maji.
你應作一銅盆座,為洗濯,之用;把盆安在會幕和祭壇之間,盆中放上水,
19 Na Aruni na wanawe wataosha mikono yao na miguu yao humo.
好叫亞郎和他的兒子們在盆中洗手洗腳。
20 Hapo waingiapo ndani ya hema ya kukutania au waendepo karibu na madhabahu kunitumikia kwa kuchoma sadaka, watajiosha majini, ili wasife.
他們進會幕,或走近祭壇行禮,或向上主焚燒火祭時,要用水洗,免得死亡。
21 Basi wataosha mikono yao na miguu yao ili kwamba wasife; na neno hili litakuwa amri kwao milele, kwake yeye na kwa wazao wake katika vizazi vyao vyote.
他們應洗手洗腳,免得死亡:這為他和他的子孫世世代代是永遠的規律。」傅禮的油
22 Kisha Yahweh akasema na Musa,
上主訓示梅瑟說:「
23 “Jitwalie manukato yaliyo bora, manemane mbichi shekeli mia tano, na mdalasini wenye harufu nzuri 250, na kane shekeli 250
你要拿上等的香料:純鄭沒藥五百「協刻耳,」香肉桂為沒藥的一半,即二百五十「協刻耳,」香菖蒲二百五十「協刻耳,」
24 na kida shekeli mia tano, kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu, na mafuta ya zeituni kiasi cha vibaba vitano.
桂皮按聖所的衡量五百「協刻耳,」橄欖油一「辛,」
25 Nawe utayafanya mafuta ya kutiwa matakatifu, marhamu iliyochanganywa kwa kazi ya ustadi ya mtengezaji manukato; yatakuwa ni mafuta matakatifu ya kutiwa.
用這些材料配製傅禮用的聖油,像配製香膏的方法配製,作為傅禮用的聖油。
26 Nawe utaipaka hema ya kukutania kwa mafuta hayo, na hilo sanduku la ushuhuda,
用此油傅會幕和約櫃,
27 na hiyo meza, na vyombo vyake vyote, na kinara cha taa, na vyombo vyake,
供桌和其上的一切器具,燈台和一切用具,香壇,
28 na madhabahu ya kufukizia uvumba, na madhabahu ya kuteketezea sadaka, pamoja na vyombo vyake vyote, na birika, na tako lake.
全燔祭壇和壇上的一切用具、盆和盆座。
29 Nawe utavitakasa vitu hivyo, ili viwe vitakatifu sana; tena kila kivigusacho vyombo vile kitakuwa kitakatifu.
你祝聖過的,都成了至聖之物,凡接觸這些物件的,也成為聖的。
30 Nawe utawatia mafuta Aruni na wanawe, na kuwatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
你也要給亞郎喊他的兒子們傅油,祝聖他們作我的司祭。
31 Nawe utanena na wana wa Israeli na kuwaambia, Haya yatakuwa ni mafuta matakatifu ya kutiwa kwa ajili yangu mimi katika vizazi vyenu vyote.
你要吩咐以色列子民說:你們應世世代代以此為傅禮用的聖油,
32 Hayatamiminwa katika kiwiliwili cha binadamu, wala msifanye mengine mfano wa haya kama yalivyoungwa kwa viungo vyake; ni matakatifu, na kwenu ninyi yatakuwa matakatifu.
不准將此油倒在俗人身上,也不准用這配製的方法配製這樣的油,因為是聖油,你們應以為聖物。
33 Mtu awaye yote atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu awaye yote atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.'”
無論誰若配製這樣的油,或用這由傅了凡人,應將他從百姓中剷除。」製香法
34 Yahweh akamwambia Musa, “Jitwalie manukato mazuri, yaani, natafi, na shekelethi, na kelbena; viungo vya manukato vizuri pamoja na ubani safi; vitu hivyo vyote na viwe vya kipimo kimoja.
上主向梅瑟說:「你要取這些香料:就是蘇合香、香螺和白松香;這些香料與純乳香應有相等的分量,
35 Nawe utafanya uvumba wa vitu hivyo, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenazaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu.
以香膏的配製法配成香,再加上鹽,使之成為純潔和聖的。
36 Nawe baadhi yake utayaponda sana, na kuyaweka mbele ya ushuhuda ndani ya hema ya kukutania, hapo nitakapokutana nawe; nayo yatakuwa kwenu matakatifu sana.
將一部份研成碎末,獻在會幕中的約櫃前,即我與你會晤的地方;這為你是至聖之物。
37 Na uvumba utakaofanya, hamtajifanyia uvumba wenye viungo sawasawa na uvumba huo; utakuwa kwenu mtakatifu kwa ajili yangu.
你所配製的這種香,不准配製為自己用,應當作聖物,只為上主用。
38 Mtu ye yote atakayefanya mfano wa huo, ili kuunusa, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.
無論誰若配製這樣的香料,為聞香氣,應將他從百姓中鏟除。」