< Kutoka 29 >
1 Sasa Hivi ndivyo wapaswa kufanya kuwatenga ili wanitumikie kama makuhani. Chukuwa mtoto wa ng'ombe dume na kondoo bila lawama,
“你使亚伦和他儿子成圣,给我供祭司的职分,要如此行:取一只公牛犊,两只无残疾的公绵羊,
2 mkate bila hamira, na keki bila hamira iliyo changanywa na mafuta. Pia chukuwa maandazi bila hamira yalio pakwa mafuta. Fanya maandazi kwa unga mzuri wa ngano.
无酵饼和调油的无酵饼,与抹油的无酵薄饼;这都要用细麦面做成。
3 Lazima uweke kwenye ndoo moja, leta kwenye ndoo, na kuleta pamoja na ng'ombe dume na wana kondoo wawili.
这饼要装在一个筐子里,连筐子带来,又把公牛和两只公绵羊牵来。
4 Lazima nawe umlete Aruni na wana wake wawili katika lango la kuingilia hema la kukutania. Lazima uwasafishe Aruni na wana wake kwenye maji.
要使亚伦和他儿子到会幕门口来,用水洗身。
5 Kisha twaa hayo mavazi na kumvika Haruni; itie kanzu, na joho ya naivera, na naivera, na kifuko cha kifuani, na kumkaza kwa huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi.
要给亚伦穿上内袍和以弗得的外袍,并以弗得,又带上胸牌,束上以弗得巧工织的带子。
6 Nawe mvike kile kilemba kichwani, na ile taji takatifu utaitia katika kile kilemba.
把冠冕戴在他头上,将圣冠加在冠冕上,
7 Ndipo utakapotwaa hayo mafuta ya kutiwa, na kummiminia kichwani mwake, na kumtia mafuta.
就把膏油倒在他头上膏他。
8 Kisha walete hao wanawe na kuwavika kanzu.
要叫他的儿子来,给他们穿上内袍。
9 Nawe uwakaze mishipi, Aruni na wanawe, na kuwavika kofia. Nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele. Nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.
给亚伦和他儿子束上腰带,包上裹头巾,他们就凭永远的定例得了祭司的职任。又要将亚伦和他儿子分别为圣。
10 Kisha utamleta huyo ng’ombe mbele ya hema ya kukutania; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo ng’ombe.
“你要把公牛牵到会幕前,亚伦和他儿子要按手在公牛的头上。
11 Kisha utamchinja huyo ng’ombe mbele ya Yahweh pa hema ya kukutania. BWANA,
你要在耶和华面前,在会幕门口,宰这公牛。
12 Kisha twaa baadhi ya damu ya ng’ombe, uitie katika pembe za madhabahu kwa kidole chako; na kuimimina damu yote chini ya madhabahu.
要取些公牛的血,用指头抹在坛的四角上,把血都倒在坛脚那里。
13 Kisha chukuwa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu.
要把一切盖脏的脂油与肝上的网子,并两个腰子和腰子上的脂油,都烧在坛上。
14 Lakini nyama yake huyo ng’ombe, na ngozi yake, na mavi yake, utayachoma kwa moto nje ya marago; ni sadaka kwa ajili ya dhambi.
只是公牛的皮、肉、粪都要用火烧在营外。这牛是赎罪祭。
15 Pia mtwae kondoo mume mmoja; na Aruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo mume.
“你要牵一只公绵羊来,亚伦和他儿子要按手在这羊的头上。
16 Kisha utamchinja huyo kondoo mume, na kuitwaa damu yake, na kuinyunyiza katika madhabahu kuizunguka kando-kando.
要宰这羊,把血洒在坛的周围。
17 Kisha utamkata-kata kondoo vipande vyake, na kuyaosha matumbo yake na miguu yake, na kuiweka pamoja na vipande vyake na kichwa chake,
要把羊切成块子,洗净五脏和腿,连块子带头,都放在一处。
18 nawe mteketeze kondoo mzima juu ya madhabahu. Ni sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yaYahweh; ni harufu nzuri, sadaka iliyosongezwa kwa Yahweh kwa njia ya moto.
要把全羊烧在坛上,是给耶和华献的燔祭,是献给耶和华为馨香的火祭。
19 Kisha mtwae huyo kondoo mwingine; na Aruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo.
“你要将那一只公绵羊牵来,亚伦和他儿子要按手在羊的头上。
20 Kisha utamchinja kondoo, na kuitwaa damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la Aruni la upande wa kuume, na katika ncha za masikio ya kuume ya wanawe, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kuume, na katika vidole vikuu vya miguu yao ya kuume, na kuinyunyiza hiyo damu katika madhabahu kuizunguka kando-kando.
你要宰这羊,取点血抹在亚伦的右耳垂上和他儿子的右耳垂上,又抹在他们右手的大拇指上和右脚的大拇指上;并要把血洒在坛的四围。
21 Kisha twaa katika hiyo damu iliyo juu ya madhabahu, na katika hayo mafuta ya kutiwa, na kumnyunyizia Aruni, juu ya mavazi yake, na wanawe, na mavazi yao pia, pamoja naye; naye atatakaswa, na mavazi yake, na wanawe, na mavazi ya wanawe, pamoja naye.
你要取点膏油和坛上的血,弹在亚伦和他的衣服上,并他儿子和他儿子的衣服上,他们和他们的衣服就一同成圣。
22 Tena yatwae mafuta ya huyo kondoo mume, na mkia wake wa mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo katika hizo figo, na paja la kuume; kwani ni kondoo ambaye ni wa kuwekwa kwa kazi takatifu.
“你要取这羊的脂油和肥尾巴,并盖脏的脂油与肝上的网子,两个腰子和腰子上的脂油并右腿(这是承接圣职所献的羊)。
23 Utwae na mkate mmoja wa unga, na mkate mmoja ulioandaliwa kwa mafuta, na kaki moja katika kile kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, kilichowekwa mbele ya Yahweh.
再从耶和华面前装无酵饼的筐子中取一个饼,一个调油的饼和一个薄饼,
24 Nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Aruni, na katika mikono ya wanawe; nawe utavitikisa-tikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh.
都放在亚伦的手上和他儿子的手上,作为摇祭,在耶和华面前摇一摇。
25 Kisha uvitwae vile vitu mikononi mwao, na kuviteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa, viwe harufu nzuri mbele yangu; ni sadaka iliyotengenezwa kwangu kwa njia ya moto.
要从他们手中接过来,烧在耶和华面前坛上的燔祭上,是献给耶和华为馨香的火祭。
26 Kisha twaa kidari cha huyo kondoo wa kuwekwa kwake Haruni kwa kazi takatifu, na kukitikisa-tikisa kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za Yahwe nacho kitakuwa ni sehemu yako.
“你要取亚伦承接圣职所献公羊的胸,作为摇祭,在耶和华面前摇一摇,这就可以作你的分。
27 Nawe kitakase kile kidari cha ile sadaka ya kutikiswa, na lile paja la sadaka ya kuinuliwa, lililotikiswa, na lililoinuliwa juu, vya yule kondoo wa kuwekwa kwa kazi takatifu, huyo aliyekuwa kwa ajili ya Aruni na wanawe.
那摇祭的胸和举祭的腿,就是承接圣职所摇的、所举的,是归亚伦和他儿子的。这些你都要成为圣,
28 Navyo vitakuwa vya Haruni na wanawe posho ya lazima sikuzote itokayo kwa hao wana wa Israeli; kwa kuwa ni sadaka ya kuinuliwa; nayo itakuwa ni sadaka ya kuinuliwa itokayo kwa hao wana wa Israeli katika dhabihu zao za sadaka za amani, ni sadaka yao ya kuinuliwa kwa ajili ya Yahweh.
作亚伦和他子孙从以色列人中永远所得的分,因为是举祭。这要从以色列人的平安祭中,作为献给耶和华的举祭。
29 Na hayo mavazi matakatifu ya Aruni yatakuwa ya wanawe baada yake, wayavae watakapotiwa mafuta, na watakapowekwa kwa kazi takatifu.
“亚伦的圣衣要留给他的子孙,可以穿着受膏,又穿着承接圣职。
30 Huyo mwanawe atakayekuwa kuhani badala yake atayavaa muda wa siku saba, hapo atakapoingia ndani ya hiyo hema ya kukutania, ili atumike ndani ya mahali patakatifu.
他的子孙接续他当祭司的,每逢进会幕在圣所供职的时候,要穿七天。
31 Nawe twaa huyo kondoo mume aliyekuwa wa kuwekwa kwa kazi takatifu, na kuitokosa nyama yake katika mahali patakatifu.
“你要将承接圣职所献公羊的肉煮在圣处。
32 Na Aruni na wanawe wataila ile nyama ya kondoo, na mikate iliyo katika kile kikapu, hapo mbele ya mlango wa hema ya kukutania.
亚伦和他儿子要在会幕门口吃这羊的肉和筐内的饼。
33 Nao watakula vile vitu ambavyo upatanisho ulifanywa kwa hivyo, ili kuwaweka kwa kazi takatifu na kuwatakasa; lakini mgeni asivile, maana, ni vitu vitakatifu.
他们吃那些赎罪之物,好承接圣职,使他们成圣;只是外人不可吃,因为这是圣物。
34 Na kwamba kitu cho chote cha ile nyama, iliyo kwa ajili ya kuweka kwa kazi takatifu, au cho chote cha hiyo mikate, kikisalia hata asubuhi, ndipo utavichoma kwa moto hivyo vilivyosalia; havitaliwa, maana, ni vitu vitakatifu
那承接圣职所献的肉或饼,若有一点留到早晨,就要用火烧了,不可吃这物,因为是圣物。
35 Ni hivyo utakavyowatendea Aruni na wanawe kama nilivyo kuagiza. Utawaweka kwa kazi takatifu siku saba.
“你要这样照我一切所吩咐的,向亚伦和他儿子行承接圣职的礼七天。
36 Kila siku utamtoa ng’ombe wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho; nawe utaisafisha hiyo madhabahu, hapo utakapofanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu; nawe utaitia mafuta, ili kuitakasa.
每天要献公牛一只为赎罪祭。你洁净坛的时候,坛就洁净了;且要用膏抹坛,使坛成圣。
37 Utafanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu muda wa siku saba, na kuitakasa; ndipo madhabahu itakapokuwa takatifu sana; kila kitu kiigusacho madhabahu kitakuwa kitakatifu.
要洁净坛七天,使坛成圣,坛就成为至圣。凡挨着坛的都成为圣。”
38 Lazima utoe kwenye madhabahu wana-kondoo wa mwaka mmoja wawili siku baada ya siku
“你每天所要献在坛上的就是两只一岁的羊羔;
39 daima. Mwana-kondoo mmoja utamchinja asubuhi; na mwana-kondoo wa pili utamchinja jioni
早晨要献这一只,黄昏的时候要献那一只。
40 Pamoja na mwana-kondoo mmoja utatoa vibaba vitatu vya unga mzuri uliochanganyika na mafuta yenye kupondwa, kiasi cha kibaba na robo kibaba; na divai kiasi cha kibaba na robo kibaba, iwe sadaka ya kinywaji.
和这一只羊羔同献的,要用细面伊法十分之一与捣成的油一欣四分之一调和,又用酒一欣四分之一作为奠祭。
41 Na huyo mwana-kondoo wa pili utamchinja wakati wa jioni. Nawe utamfanyia vivyo kama ile sadaka ya unga ya asubuhi, na kama ile sadaka yake ya kinywaji. Hii itatoa harufu nzuri, ni dhabihu ya kusongezwa kwangu kwa njia ya moto.
那一只羊羔要在黄昏的时候献上,照着早晨的素祭和奠祭的礼办理,作为献给耶和华馨香的火祭。
42 Itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema ya kukutania mbele ya Yahweh, hapo nitakapokutana nanyi, ili niseme na wewe hapo.
这要在耶和华面前、会幕门口,作你们世世代代常献的燔祭。我要在那里与你们相会,和你们说话。
43 Nami nitakutana na wana wa Israeli hapo; na hiyo hema itafanywa takatifu na utukufu wangu. Nami nitaitakasa hiyo hema ya kukutania, na hiyo madhabahu.
我要在那里与以色列人相会,会幕就要因我的荣耀成为圣。
44 Pia Aruni na wanawe nitawatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
我要使会幕和坛成圣,也要使亚伦和他的儿子成圣,给我供祭司的职分。
45 Na mimi nitakaa kati ya wana wa Israeli, nami nitakuwa Mungu wao.
我要住在以色列人中间,作他们的 神。
46 Nao watanijua kuwa mimi ndimi Yahweh, Mungu wao, niliyewaleta watoke katika nchi ya Misri, nipate kukaa kati yao. Ni mimi Yahweh, Mungu wao.
他们必知道我是耶和华—他们的 神,是将他们从埃及地领出来的,为要住在他们中间。我是耶和华—他们的 神。”