< Kutoka 27 >
1 Nawe fanya madhabahu ya mti wa mshita, urefu wake utakuwa ni dhiraa tano na upana wake dhiraa tano. Hiyo madhabahu itakuwa mraba na kwenda juu kwake kutakuwa dhiraa tatu.
“你要用皂荚木做坛。这坛要四方的,长五肘,宽五肘,高三肘。
2 Nawe fanya pembe nne kama mfano wa pembe za ng'ombe. Hizo pembe zitakuwa za kitu kimoja na madhabahu, nawe utayafunika kwa shaba.
要在坛的四拐角上做四个角,与坛接连一块,用铜把坛包裹。
3 Lazima vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake. Vyombo vyake vyote utavifanya vya shaba.
要做盆,收去坛上的灰,又做铲子、盘子、肉锸子、火鼎;坛上一切的器具都用铜做。
4 Nawe uifanyie hiyo madhabahu wavu wa shaba. Kisha utie pete nne za shaba katika hizo pembe nne za ule wavu.
要为坛做一个铜网,在网的四角上做四个铜环,
5 Nawe lazima uweke huo wavu chini ya kizingo kiizungukacho madhabahu upande wa chini.
把网安在坛四面的围腰板以下,使网从下达到坛的半腰。
6 Nawe fanya miti kwa ajili ya madhabahu, miti ya mshita, na kuifunika shaba.
又要用皂荚木为坛做杠,用铜包裹。
7 Na hiyo miti itatiwa katika viduara, na ile miti itakuwa katika pande mbili za madhabahu, wakati wa kuichukua.
这杠要穿在坛两旁的环子内,用以抬坛。
8 Uifanye ya mbao, yenye mvungu ndani yake kama ulivyooneshwa mlimani.
要用板做坛,坛是空的,都照着在山上指示你的样式做。”
9 Nawe ufanye ua wa maskani. Upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia moja.
“你要做帐幕的院子。院子的南面要用捻的细麻做帷子,长一百肘。
10 Na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na vitako vyake ishirini, vitako vyake vitakuwa vya shaba kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
帷子的柱子要二十根,带卯的铜座二十个。柱子上的钩子和杆子都要用银子做。
11 Ni vivyo hivyo upande wa kaskazini, urefu wake hiyo chandarua utakuwa ni dhiraa mia moja, na nguzo zake ishirini, na vitako vyake ishirini vitakuwa vya shaba, kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
北面也当有帷子,长一百肘,帷子的柱子二十根,带卯的铜座二十个。柱子上的钩子和杆子都要用银子做。
12 Na upande wa magharibi, upana wa ua kutakuwa na chandarua ya dhiraa hamsini; nguzo zake kumi, na vitako vyake kumi.
院子的西面当有帷子,宽五十肘,帷子的柱子十根,带卯的座十个。
13 Na upana wa ule ua upande wa mashariki kuelekea mashariki utakuwa ni dhiraa hamsini.
院子的东面要宽五十肘。
14 Chandarua upande mmoja wa lango itakuwa dhiraa kumi na tano upana wake. Lazima nguzo zake zitakuwa tatu na vitako vyake vitatu.
门这边的帷子要十五肘,帷子的柱子三根,带卯的座三个。
15 Upande wa pili ni vivyo hivyo chandarua ya dhiraa kumi na tano; nguzo zake tatu, na vitako vyake vitatu.
门那边的帷子也要十五肘,帷子的柱子三根,带卯的座三个。
16 Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa cha nguo ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na vitako vyake vinne.
院子的门当有帘子,长二十肘,要拿蓝色、紫色、朱红色线,和捻的细麻,用绣花的手工织成,柱子四根,带卯的座四个。
17 Nguzo zote za ule ua ziuzungukao pande zote zitakuwa na vitanzi vya fedha; kulabu zake za fedha, na vitako vyake vya shaba.
院子四围一切的柱子都要用银杆连络,柱子上的钩子要用银做,带卯的座要用铜做。
18 Urefu wa huo ua utakuwa dhiraa mia moja, na upana wake utakuwa dhiraa hamsini kotekote, na kwenda juu kwake dhiraa tano; yawe ya nguo ya kitani nzuri, na vitako vyake vitakuwa vya shaba.
院子要长一百肘,宽五十肘,高五肘,帷子要用捻的细麻做,带卯的座要用铜做。
19 Vyombo vyote vya maskani vitumiwavyo katika utumishi wake wote, na vigingi vyake vyote, na vigingi vyote vya ule ua, vitakuwa vya shaba.
帐幕各样用处的器具,并帐幕一切的橛子,和院子里一切的橛子,都要用铜做。”
20 awe waamuru wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya nuru, ili kufanya ile taa kuwaka daima.
“你要吩咐以色列人,把那为点灯捣成的清橄榄油拿来给你,使灯常常点着。
21 Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza tangu jioni hadi asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.
在会幕中法柜前的幔外,亚伦和他的儿子,从晚上到早晨,要在耶和华面前经理这灯。这要作以色列人世世代代永远的定例。”