< Kutoka 22 >
1 Kama mwanaume akiiba ng'ombe aua kondoo na kumuua au kumuuza, kisha lazima alipe ng'ombe watano au ng'ombe mmoja, na kondoo wanne kwa mmoja.
“Kama mtu akiiba maksai au kondoo na kumchinja au kumuuza, ni lazima alipe ngʼombe watano badala ya maksai mmoja na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja.
2 Kama mwizi akikutwa anavunja ndani, na kama akipigwa na kufa, hakutakuwa na hatia ya mauaji hayatakuwa juu ya mtu yeyote.
“Kama mwizi akishikwa anavunja nyumba akapigwa hata akafa, aliyemuua hana hatia ya kumwaga damu;
3 Lakini kama jua limechomoza kabla ya yeye kuvunja ndani, hatia ya mauaji itakuwa juu ya aliyemuua. Mwizi lazima afanya alipe alichoiba. Kama hana chochote, kisha lazima auzwe kwa uwizi wake.
lakini jambo hilo likitokea wakati jua limechomoza, huyo mtu atakuwa na hatia ya kumwaga damu. “Mwizi huyo sharti alipe, lakini kama hana kitu, lazima auzwe ili alipe kwa ajili ya wizi wake.
4 Kama mnyama amekutwa hai eneo lake, kama ni ng'ombe, punda, au kondoo, lazima alipe mara mbili.
“Kama mnyama aliyeibwa akikutwa hai mikononi mwake, ikiwa ni maksai au punda au kondoo, lazima alipe mara mbili.
5 Kama mwanaume akiwapeleka malishoni mifugo yake au shamba la mizabibu na akawaachia wanyama wake, na kawa wanakula shambani mwa mwanaume mwengine, lazima afanye malipo bora kutoka shambani mwake na shamba lake la mizabibu.
“Kama mtu akichunga mifugo yake katika shamba au shamba la mizabibu, na akawaachia wajilishe katika shamba la mtu mwingine, ni lazima alipe vitu bora kutoka kwenye shamba lake mwenyewe au kutoka shamba lake la mizabibu.
6 Kama moto ukitokea na kusambaa kwenye miba hadi mbegu, au mimea, au shamba kuteketezwa, yeye aliye anzisha moto lazima afanye malipo.
“Kama moto ukiwaka na kuenea kwenye vichaka vya miiba na kuteketeza miganda ya nafaka au nafaka ambayo haijavunwa, au kuteketeza shamba lote, mtu yule aliyewasha moto lazima alipe.
7 Kama mwanaume akitoa pesa au mali kwa jirani yake amtunzie, na kama itaibiwa nyumbani mwa huyo mwanaume, kama mwizi akipatikana, huyo mwizi lazima alipe mara mbili.
“Kama mtu akimpa jirani yake fedha au mali nyingine amtunzie, na kama vikiibwa kutoka nyumba ya huyo jirani, kama mwizi atashikwa, lazima alipe mara mbili.
8 Lakini kama mwizi asipo patikana, kisha mmiliki wa nyumba ata kuja mbele za waamuzi kuona kama ameeka mkono wake kwenye mali za jirani yake.
Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atafika mbele ya waamuzi ili kuthibitisha kuwa hakuchukua mali ya mwenzake.
9 Kwa kila lumbano kuhusu jambo, kama ni ng'ombe, punda, kondoo, nguo, au chochote kilichopotea mtu anacho sema, “Hichi ni changu,” malalamiko ya pande zote lazima zije kwa waamuzi. Mwanaume ambaye waamuzi wanamkuta na hatia ata lipa mara mbili kwa jirani yake.
Pakiwepo jambo lolote la mali isiyo halali, ikiwa ni maksai, punda, kondoo, mavazi, ama mali yoyote iliyopotea ambayo fulani atasema, ‘Hii ni mali yangu,’ pande zote mbili wataleta mashauri yao mbele ya waamuzi. Yule ambaye waamuzi watamwona kuwa na hatia atamlipa jirani yake mara mbili.
10 Kama mwanaume akimpa jirani yake punda, ng'ombe, kondoo, au mnyama yeyote kumuhifadhia, na kama akifa au kuumia au akibebwa pasipo mtu kumuona,
“Kama mtu akimpa jirani yake punda, ngʼombe, kondoo au mnyama mwingine yeyote amtunzie, akifa au akijeruhiwa au akichukuliwa wakati haonekani na mtu yeyote,
11 kiapo kwa Yahweh lazima wafanye wote wawili, kama ndio au hapana mtu ameeka mkono wake kwenye mali ya jirani yake. Mmiliki lazima akubali hili, na mwengine hatafanya malipo.
jambo hili kati yao wawili litaamuliwa kwa kuapa kiapo mbele za Bwana, kwamba huyo jirani hakuhusika na wizi wa mali ya jirani yake. Mwenye mali itampasa akubali jambo hili, na hakuna malipo yatakayohitajika.
12 Lakini kama iliibwa kwake, mwengine lazima afanye malipo kwa mmiliki kwa ajili yake.
Lakini kama mnyama aliibwa kwa jirani, itampasa amlipe mwenye mnyama.
13 Kama mnyama alikatwa vipande, acha mwanaume mwengine alete huyo mnyama kama ushahidi. Hatalipa kwa ajili ya vile vipande.
Kama ameraruliwa na mnyama pori, ataleta mabaki ya mnyama kama ushahidi, naye hatadaiwa kulipa mnyama aliyeraruliwa.
14 Kama mwanaume akiazima mnyama kutoka kwa jirani yake na mnyama akajeruhia au akafa pasipo mmiliki kuwa naye, mwanaume mwengine lazima afanya malipo.
“Kama mtu akimwazima mnyama kutoka kwa jirani yake, na kama akiumia au akafa na mwenye mnyama hayupo, lazima amlipe huyo mnyama.
15 Lakini kama mmiliki alikuwa nae, mwanaume mwengine haitaji kulipa; kama mnyama aliazimwa, atalipwa kwa gharama ya kuazima.
Lakini mwenye mnyama akiwa angalipo na mnyama wake, mwazimaji hatalazimika kumlipa. Kama mnyama alikuwa amekodishwa, fedha iliyolipwa kwa kukodisha inatosha kwa kufidia hasara.
16 Kama mwanaume akimtongoza bikra ambaye hana mchumba, na kama akilala naye, lazima amfanye kuwa mke wake kwa kulipa gharama za bibi arusi zinazo stahili.
“Kama mtu akimshawishi bikira ambaye hajaposwa na akilala naye, lazima alipe mahari, kisha atamwoa msichana huyo.
17 Kama baba yake akikataa kabisa kumpatia, lazima alipe hela inayo lingana na gharama za bibi arusi bikra.
Baba wa msichana akikataa katakata kumpa huyo mtu huyo msichana wake, bado ni lazima huyo mtu atalipa mahari kama inavyostahili malipo ya ubikira.
18 Hautamwacha mchawi kuishi.
“Usiruhusu mwanamke mchawi aishi.
19 Yeyote atakaye lala na mnyama lazima auawe.
“Mtu yeyote aziniye na mnyama lazima auawe.
20 Yeyote atakaye toa dhabihu kwa mungu mwengine isipo kuwa Yahweh lazima auawe.
“Mtu awaye yote anayemtolea mungu mwingine dhabihu isipokuwa Bwana, lazima aangamizwe.
21 Hauta mkosea mgeni au kumnyanyasa, kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.
“Usimtendee mgeni vibaya au kumwonea, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri.
22 Hauruhusiwi kumtendea vibaya mjane au mtoto asiye kuwa na baba.
“Usimdhulumu mjane wala yatima.
23 Ukiwadhuru ata kidogo, na kama wakiniita mimi, hakika nitasikia sauti yao.
Kama ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao.
24 Hasira yangu itawaka, na nitakuua kwa upanga; wake zenu watakuwa wajane, na watoto wenu pasipo baba.
Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima.
25 Ukiazima hela kwa watu wangu walio maskini, haupaswi kuwa kama anaye kopesha hela kwake au kutoza faida.
“Kama ukimkopesha mmojawapo wa watu wangu fedha ambaye ni mhitaji, usiwe kama mtu mkopesha fedha; usimtoze riba.
26 Ukichukuwa vazi la jirani yako kwa deni, lazima umrudishie kabla jua kuzama,
Kama ukichukua vazi la jirani kama rehani, ulirudishe kwake kabla jua kuzama,
27 kwa kuwa hilo ndilo funiko lake, ni vazi la mwili wake. Nini tena ambacho anaweza kulalia? Atakapo niita mimi, nitasikia, kwa kuwa mimi ni mwenye huruma.
kwa kuwa vazi lake ndilo pekee alilo nalo la kumfunika mwili wake. Ni nini kingine atajifunika nacho? Atakaponililia, nitasikia, kwa kuwa nina huruma.
28 Usinikufuru mimi, Mungu, wala kumtukana mtawala wa watu wako.
“Usimkufuru Mungu au kumlaani mtawala wa watu wako.
29 Husizuie sadaka kutoka kwenye mavuno yako au kwenye hifadhi ya mvinyo wako. Lazima unipe mzaliwa wa kwanza wa wana wako.
“Usiache kutoa sadaka kutoka ghala lako au mapipa yako. “Lazima unipe mzaliwa wa kwanza wa wana wako.
30 Lazima ufanye hivyo hivyo kwa ng'ombe na kondoo wako. Kwa siku saba lazima wabaki na mama zao, lakini siku ya nane lazima unipe mimi.
Ufanye vivyo hivyo kwa ngʼombe wako na kwa kondoo wako. Waache wakae na mama zao kwa siku saba, lakini siku ya nane unipe.
31 Mtakuwa watu walio tengwa kwa ajili yangu. Hivyo hamtakula nyama iliyo uliwa na wanyama porini. Badala yake, uwatupie mbwa.
“Ninyi mtakuwa watu wangu watakatifu. Kwa hiyo msile nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori; mtupieni mbwa.