< Kutoka 16 >

1 Watu wakaendelea na safari kutoka Elimu, na jamii yote ya Waisraeli ikaja nyikani mwa Sinu, iliyopo katikati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili walipo toka Misri.
ויסעו מאילם ויבאו כל עדת בני ישראל אל מדבר סין אשר בין אילם ובין סיני בחמשה עשר יום לחדש השני לצאתם מארץ מצרים׃
2 Jamii yote ya Waisraeli wali walalamikia Musa na Aruni nyikani.
וילינו כל עדת בני ישראל על משה ועל אהרן במדבר׃
3 Waisraeli waliwaambia, “Kama tu tungekufa kwa mkono wa Yahweh nchi ya Misri tulipo kuwa tumeketi kwenye vyombo vya nyama na tulikuwa tunakula mkate kwa tele. Maana umetuleta nyikani uuwe jamii zetu zote kwa njaa.”
ויאמרו אלהם בני ישראל מי יתן מותנו ביד יהוה בארץ מצרים בשבתנו על סיר הבשר באכלנו לחם לשבע כי הוצאתם אתנו אל המדבר הזה להמית את כל הקהל הזה ברעב׃
4 Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Nitakunyeshea mvua ya mkate. Watu wataenda na kukusanya kiasi cha siku kila siku ili niwajaribu kama wataendelea kushika sheria yangu au hapana.
ויאמר יהוה אל משה הנני ממטיר לכם לחם מן השמים ויצא העם ולקטו דבר יום ביומו למען אנסנו הילך בתורתי אם לא׃
5 Itakuja kuwa siku ya sita, kwamba watakusanya mara mbili zaidi ya wanavyo kusanyaga, na watapika wanacholeta.”
והיה ביום הששי והכינו את אשר יביאו והיה משנה על אשר ילקטו יום יום׃
6 Kisha Musa na Aruni wakawaambia watu wote wa Israeli, “Jioni mtajua kuwa ni Yahweh aliye waleta kutoka nchi ya Misri.
ויאמר משה ואהרן אל כל בני ישראל ערב וידעתם כי יהוה הוציא אתכם מארץ מצרים׃
7 Asubui utaona utukufu wa Yahweh, kwa maana anasikia mna mlalamikia. Sisi ni nani hadi mtulalamikie?”
ובקר וראיתם את כבוד יהוה בשמעו את תלנתיכם על יהוה ונחנו מה כי תלונו עלינו׃
8 Musa pia akasema, “Utajua hili pale Yahweh atakapo kupa nyama jioni na mkate asubui kwa tele - kwa kuwa amesikia malalamishi mnayo tamka dhidi yake. Nani ni Aruni na mimi? Malalamishi yenu sio dhidi yetu; ni dhidi ya Yahweh.”
ויאמר משה בתת יהוה לכם בערב בשר לאכל ולחם בבקר לשבע בשמע יהוה את תלנתיכם אשר אתם מלינם עליו ונחנו מה לא עלינו תלנתיכם כי על יהוה׃
9 Musa akamwambia Aruni, “Sema kwa jamii yote ya watu wa Israeli, 'Njoo karibu ya Yahweh, kwa kuwa amesikia malalamishi yenu.'”
ויאמר משה אל אהרן אמר אל כל עדת בני ישראל קרבו לפני יהוה כי שמע את תלנתיכם׃
10 Ikawa, Aruni alipo sema na jamii yote ya watu wa Israeli, wakaangalia kuelekea nyikani, na, tazama, utukufu wa Yahweh ukatokea kwenye wingu.
ויהי כדבר אהרן אל כל עדת בני ישראל ויפנו אל המדבר והנה כבוד יהוה נראה בענן׃
11 Kisha Yahweh akasema na Musa na kumwambia,
וידבר יהוה אל משה לאמר׃
12 “Nimesikia malalamishi ya watu wa Israeli. Sema nao na useme, 'Jioni utakula nyama, na asubui utashiba mkate. Kisha utajua mimi ni Yahweh Mungu wako.'”
שמעתי את תלונת בני ישראל דבר אלהם לאמר בין הערבים תאכלו בשר ובבקר תשבעו לחם וידעתם כי אני יהוה אלהיכם׃
13 Ikaja kuwa kwamba jioni kware wakaja juu na kufunika kambi. Asubui umande ulitanda kambini.
ויהי בערב ותעל השלו ותכס את המחנה ובבקר היתה שכבת הטל סביב למחנה׃
14 Umande ulipo kwisha, pale juu ya ardhi ya nyikani kulikuwa na kama barafu iliyo ganda kwenye ardhi.
ותעל שכבת הטל והנה על פני המדבר דק מחספס דק ככפר על הארץ׃
15 Watu wa Israeli walipo ona, walisema mmoja kwa mwenzake, “Hii ni nini?” Hawakujua ilikuwa ni nini. Musa akawaambia, “Ni mkate Yahweh aliyo wapa mle.
ויראו בני ישראל ויאמרו איש אל אחיו מן הוא כי לא ידעו מה הוא ויאמר משה אלהם הוא הלחם אשר נתן יהוה לכם לאכלה׃
16 Hii ni amri Yahweh aliyotoa: 'Lazima ukusanye, kila mmoja wenu, kiasi unacho itaji kula, lita mbili kwa kila mtu. Hivi ndivyo utakavyo kusanya: Kusanya cha kutosha kula cha kila mtu anaye ishi hemani mwako.'”
זה הדבר אשר צוה יהוה לקטו ממנו איש לפי אכלו עמר לגלגלת מספר נפשתיכם איש לאשר באהלו תקחו׃
17 Watu wa Israeli wakafanya hivyo. Baadhi wakakusanya zaidi, baadhi wakakusanya kidogo.
ויעשו כן בני ישראל וילקטו המרבה והממעיט׃
18 Walipo pima kwa kipimo cha lita, hao walio kusanya zaidi hawakuwa na kilicho salia, na hao walio kusanya kidogo hawakuwa na pungufu. Kila mmoja alikusanya cha kutosha kukidhi maitaji yake.
וימדו בעמר ולא העדיף המרבה והממעיט לא החסיר איש לפי אכלו לקטו׃
19 Kisha Musa akawaambia, “Hakuna ata mmoja kubakiza hadi asubui.”
ויאמר משה אלהם איש אל יותר ממנו עד בקר׃
20 Walakini, hawakumsikiliza Musa. Baadhi yao waliacha baadhi hadi asubui, lakini ilizalisha wadudu na kuwa batili. Kisha Musa akawa na hasira juu yao.
ולא שמעו אל משה ויותרו אנשים ממנו עד בקר וירם תולעים ויבאש ויקצף עלהם משה׃
21 Walikusanya asubui kwa asubui. Kila mtu alikusanya cha kutosha kula kwa hiyo siku. Jua lilipo kuwa kali, ili yayuka.
וילקטו אתו בבקר בבקר איש כפי אכלו וחם השמש ונמס׃
22 siku ya sita walikusanya mkate mara mbili zaidi, lita mbili kwa kila mtu. Viongozi wote wa jamii walikuja na kumwambia hili kwa Musa.
ויהי ביום הששי לקטו לחם משנה שני העמר לאחד ויבאו כל נשיאי העדה ויגידו למשה׃
23 Aliwaambia, “Hili ndilo Yahweh alililo lisema: 'Kesho ni mapumziko ya kujiliwaza, sabato takatifu kwa utukufu wa Yahweh. Oka kile unataka kuoka, na chemsha kile unataka kuchemsha. Vyote vitakavyo baki, jihifadhie hadi asubui.”'
ויאמר אלהם הוא אשר דבר יהוה שבתון שבת קדש ליהוה מחר את אשר תאפו אפו ואת אשר תבשלו בשלו ואת כל העדף הניחו לכם למשמרת עד הבקר׃
24 Hivyo wakaeka pembeni hadi asubui, kama Musa alivyo elekeza. Haikuharibika, wala haikuwa na mdudu yeyote.
ויניחו אתו עד הבקר כאשר צוה משה ולא הבאיש ורמה לא היתה בו׃
25 Musa alisema, “Kula hicho cha kula leo, kwa kuwa leo ni siku iliyo tengwa ya kumtukuza Yahweh. Leo hamtaikuta mashambani.
ויאמר משה אכלהו היום כי שבת היום ליהוה היום לא תמצאהו בשדה׃
26 Mtaikusanya ndani ya siku sita, lakini siku ya saba ni Sabato. Siku ya Sabato hakuta kuwa na manna.”
ששת ימים תלקטהו וביום השביעי שבת לא יהיה בו׃
27 Ilikuja kuwa siku ya saba ambapo baadhi ya watu walienda kukusanya manna, lakini hawakukuta
ויהי ביום השביעי יצאו מן העם ללקט ולא מצאו׃
28 Kisha Yahweh akamwambia Musa, Kwa muda gani utaendelea kukataa kushika amri zangu na sheria zangu?
ויאמר יהוה אל משה עד אנה מאנתם לשמר מצותי ותורתי׃
29 Tazama, Yahweh amekupa Sabato. Hivyo siku ya sita anakupa mkate wa siku mbili. Kila mmoja wenu lazima akae kwenye sehemu yake; hakuna hata mmoja wa kutoka sehemu yake siku ya saba.”
ראו כי יהוה נתן לכם השבת על כן הוא נתן לכם ביום הששי לחם יומים שבו איש תחתיו אל יצא איש ממקמו ביום השביעי׃
30 Hivyo watu watapumzika siku ya saba.
וישבתו העם ביום השבעי׃
31 Watu wa Israeli walikiita chakula kile “manna.” Ilikuwa ni nyeupe kama mbegu ya mgiligani, na ladha yake kama maandazi yaliyo pikwa na asali.
ויקראו בית ישראל את שמו מן והוא כזרע גד לבן וטעמו כצפיחת בדבש׃
32 Musa akasema, “Hili ndilo Yahweh alilo amuru: 'Acha lita mbili ya manna ihifadhiwe kwa ajili vizazi vya watu wako ili kwamba uzao wako uone mkate niliyo kulisha nyikani, baada ya kukutoa kutoka nchi ya Misri.
ויאמר משה זה הדבר אשר צוה יהוה מלא העמר ממנו למשמרת לדרתיכם למען יראו את הלחם אשר האכלתי אתכם במדבר בהוציאי אתכם מארץ מצרים׃
33 Musa akamwambia Aruni, “Chukuwa jagi na uweke lita mbili za manna ndani yake. Hifadhi kwa Yahweh i dumu vizazi vyote vya watu.”
ויאמר משה אל אהרן קח צנצנת אחת ותן שמה מלא העמר מן והנח אתו לפני יהוה למשמרת לדרתיכם׃
34 Kama Yahweh alivyo muamuru Musa, Aruni akahifadhi pembeni mwa mawe yaliyo kuwa na amri za agano.
כאשר צוה יהוה אל משה ויניחהו אהרן לפני העדת למשמרת׃
35 Watu wa Israeli walikula manna miaka arobaini mpaka walipo kuja nchi yenye watu. Walikula mpaka walipo fika kwenye mipaka ya nchi ya Kanani.
ובני ישראל אכלו את המן ארבעים שנה עד באם אל ארץ נושבת את המן אכלו עד באם אל קצה ארץ כנען׃
36 Lita mbili ni makumi ya efa.
והעמר עשרית האיפה הוא׃

< Kutoka 16 >