< Kutoka 14 >

1 Yahweh akasema na Musa na kumwambia,
從厄堂到紅海1. 上主訓示梅瑟說:「
2 “Waambie Waisraeli wageuke na kueka kambi mbele ya Pi Hahirothi, katikati ya Migdoli na bahari, mbele ya Baali Zefoni. Wapaswa kueka kambi pembenni ya Pi Hahirothi.
你吩咐以色列子民轉回,在米革多耳及海之間的丕哈希洛特前,面對巴耳責豐安營,即在巴耳責豐之前,靠近海邊安營。
3 Farao atasema kuhusu Waisraeli, 'Wanaangaika kwenye nchi. Nyikani imewafunika.'
如此,法朗必然以為以色列子民在國境內迷了路,曠野困住了他們。
4 Nitaufanya moyo wa Farao mgumu, na yeye ata wakimbiza. Nitapata utukufu kwasababu ya Farao na jeshi lake lote. Wamisri watajua mimi ni Yahweh.” Kisha Waisraeli wakaeka kambi kama walivyo elekezwa.
我要使法郎心硬,在後面追趕他們,這樣我將在法郎和他全軍身上,大顯神能,使埃及人知道我是上主。」以色列子民就照樣作了。法郎追趕以列
5 Mfalme wa Misri alipo ambiwa Waisraeli wametoroka, nia ya Farao na watumishi wake ikageuka dhidi ya watu. Wakasema, “Tumefanya nini kwa kuwaacha Waisraeli waende huru na wasitutumikie?”
有人報告埃及王說:那百姓逃走了。法郎和他的臣僕對那百姓變了心,說:「我們放走以色列人,不再給我們服役,這是作的什麼事﹖」
6 Kisha Farao akachukuwa magari yake ya farasi na jeshi lake.
法郎遂命人準備他的車,親自率領兵士,
7 Alichukuwa magari ya farasi mia sita imara na magari yote ya farasi ya Misri, pamoja na maafisa wa hayo magari.
還帶了六百輛精良戰車和埃及所有的戰車,每輛車上都有戰士駕駛。
8 Yahweh akafanya mgumu moyo wa Farao, mfalme wa Misri, na mfalme akawafukuzia Waisraeli. Sasa Waisraeli waliondoka kwa shangwe.
上主使埃及王法郎心硬,在後面追趕以色列子民;當以色列子民大膽前行的時候,
9 Lakini Wamisri wali wafukuzia, pamoja na farasi na magari ya farasi, wapanda farasi, na jeshi lake. Walikuta Waisraeli wameeka kambi pembezoni mwa bahari kati ya Pi Hahirothi na Baali Zefoni.
埃及人在後面追趕他們,法郎所有的車馬、騎士和步兵就在靠近丕哈希洛特,巴耳責豐對面,以色列子民安營的地方趕上了。
10 Farao alipo karibia, Waisraeli walitaza juu na kushangaa. Wamisri walikuwa wakija kwao, na waliogopa. Waisraeli walimlilia Yahweh.
當法郎來近的時候,以色列子民舉目,看見埃及人趕來,都十分恐怖,向上主哀號,
11 Walimwambia Musa, “Ni kwasababu hakukuwa na makaburi Misri, hadi umetuleta tufe huku nyikani? Kwanini umetutendea hivi, kwa kututoa Misri?
也向梅瑟說:「你帶我們死在曠野裏,難道埃及沒有墳墓嗎﹖你為什麼這樣待我們,將我們從埃及出來﹖
12 Hili si ndilo tulilo kwambia Misri? Tulikwambia, 'Utuache, ili tuwafanyie Wamisri kazi.' Ingekuwa bora kwetu sisi kuwafanyia kazi kuliko kufa nyikani.”
我們在埃及不是對你說過這話:不要擾亂我們,我們甘願服侍埃及人,服侍埃及人總比死在曠野裏還好啊! 」
13 Musa akawaambia watu, “Msiogope. Simameni imara na muone wokovu Yahweh atakao uleta kwenu leo. Kwa maana hamtawaona tena Wamisri mnao waona leo.
梅瑟向百姓說:「你們不要害怕,站著別動,觀看上主今天給你們施的救恩,因為你們所見的埃及人,永遠再見不到了。
14 Yahweh ata wapigania, na ninyi mtasima imara.”
上主必替你們作戰,你們應安靜等待。」過紅海
15 Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Kwanini wewe, Musa, unaendelea kuniita mimi? Waambie Waisraeli waendelee mbele.
上主向梅瑟說:「你為什麼向我哀號,吩咐以色列子民起營前行。
16 Nyanyua gongo lako juu, nyoosha mkono wako kuelekea baharini na uigawanye sehemu mbili, ili watu wa Israeli wapite baharini kwenye nchi kavu.
你舉起棍杖,把你的手伸到海上,分開海水,叫以色列子民在海中乾地上走過。
17 Jitahadharishe kuwa nitafanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu ili wawafuate. Nitapata utukufu kwasababu ya Farao na jeshi lake lote, magari yake ya farasi, na wapanda farasi.
你看,我要使埃及人的心硬,在後面趕以色列子民;這樣我好叫法郎和他全軍,戰車和騎兵身上,大顯神能。
18 Kisha Wamisri watajua kuwa mimi ni Yahweh nitakapo pata utukufu kwasababu ya Farao, magari yake ya farasi, na wapanda farasi wake.”
我向法郎,向他的戰車和騎兵大顯神能的時候,埃及人將會知道我是上主。」
19 Malaika wa Mungu, aliyeenda mbele ya Waisraeli, aliama na kwenda nyuma yao. Nguzo ya wingu ili sogea mbele yao na kwenda kusimama nyumba yao.
在以色列大隊前面走的天主使者,就轉到他們的後面走,雲柱也從他們前面轉到他們後面停下,
20 Wingu lilikuja katikati ya kambi ya Misri na kambi ya Israeli. Lilikuwa wingu jeusi kwa Wamisri, lakini liliangaza usiku kwa ajili ya Waisraeli, hivyo upande mmoja haukuweza kuja karibu ya mwingine usiku wote.
即來到埃及軍營和以色列軍營中間;那一夜雲柱一面發黑,一面發光,這樣整夜軍隊彼此不能接近。
21 Musa akanyoosha mkono wake kuelekea bahari. Yahweh akasogeza bahari nyuma kwa upepo mkali wa mashariki usiku huo wote na kufanya bahari nchi kavu. Kwa namna hii maji yaligawanyika.
梅瑟向海伸手,上主就用極強的東風,一夜之間把海颳退,使海底成為乾地。水分開以後,
22 Waisraeli walienda katikati ya bahari kwa nchi kavu. Maji yaliunda ukuta mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto.
以色列子民便在海中乾地上走過,水在他們左右好像牆壁。埃及人沉沒海中
23 Wamisri waka wafukuzia. Wali wafuata hadi katikati ya bahari - farasi wote wa Farao, magari ya farasi, na wapanda farasi.
隨後埃及人也趕來,法郎所有的馬、戰車和騎兵,都跟著他們來到海中。
24 Lakini masaa ya mapema ya asubui, Yahweh alitazama chini jeshi la Wamisri kupitia nguzo ya moto na wingu. Alisababisha hofu miongoni mwa Wamisri.
到了晨時末更,上主在火柱和雲柱上,窺探埃及軍隊,使埃及的軍隊混亂。
25 Magari yao ya farasi yalikuwa yana kwama matairi, na wapanda farasi waliendesha kwa ugumu. Hivyo Wamisri walisema, “Acha tuwakimbie Waisraeli, kwa kuwa Yahweh anawapigania dhidi yetu.”
又使他們的車輪脫落,難以行走,以致埃及人說:「我們由以色列逃走罷! 因為上主替他們作戰,攻擊埃及人。」
26 Yahweh akamwambia Musa, “Nyoosha mkono kuelekea bahari ili maji yawarudie Wamisri, magari yao ya farasi, na wapanda farasi wao.”
上主對梅瑟說:「向海伸出你的手,使水回流到埃及人、他們的戰車和騎兵身上。」
27 Hivyo Musa akanyoosha mkono wake kuelekea bahari, na ikarudi kwenye hali yake ya kawaida palipo pambazuka. Wamisri walikimbilia ndani ya bahari, na Yahweh akawaingiza Wamisri katikati ndani yake.
到了天亮,梅瑟向海伸手,海水流回原處;埃及人迎著水逃跑的時候,上主將他們投入海中。
28 Maji yakarudi na kufunika magari ya farasi ya Farao, wapanda farasi, na jeshi lake lote lililo fuata magari ya farasi kwenye bahari. Hakuna aliyepona.
回流的水淹末了法郎的戰車、騎兵和跟著以色列子民來到海中的法郎軍隊,一個人也沒有留下。
29 Walakini, Waisraeli walitembea kwenye nchi kavu katikati ya bahari. Maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kulia na mkono wa kushoto.
但是以色列子民在海中乾地上走過去,水在他們左右好像牆壁。
30 Hivyo Yahweh akaokoa Israeli hiyo siku kutoka mkono wa Wamisri, na Israeli ikaona maiti za Wamisri ufukweni.
這樣上主在那一天從埃及人手中整救了以色列人。以色列人看見了埃及人的屍首浮在海邊上。
31 Israeli ilipoona nguvu kubwa Yahweh aliyo itumia dhidi ya Wamisri, watu walimsifu Yahweh, na kumwamini Yahweh na mtumishi wake Musa.
以色列人見上主向埃及人顯示的大能,百姓都敬畏上主,信了上主和他的僕人梅瑟。

< Kutoka 14 >