< Kutoka 12 >

1 Yahweh akasema na Musa na Aruni katika nchi ya Misri. Alisema,
Bwana akamwambia Mose na Aroni katika nchi ya Misri,
2 “Kwako wewe, mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi, mwezi wa kwanza wa mwaka kwako.
“Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu, yaani mwezi wa kwanza wa mwaka wenu.
3 Liambie kusanyiko la Israeli, 'Siku ya kumi mwezi huu kila mtu lazima achukuwe mwana kondoo au mbuzi mdogo wa kwake, kila familia ifanye hivi, mwana kondoo kwa kila nyumba.
Iambie jumuiya yote ya Israeli kwamba katika siku ya kumi ya mwezi huu, kila mtu atatwaa mwana-kondoo mmoja kwa ajili ya familia yake, mmoja kwa kila nyumba.
4 Kama hiyo nyumba ni ndogo sana kwa mwana kondoo, mwanaume na jirani yake wachukuwe mwana kondoo au nyama ya mbuzi mdogo ambayo itatosha watu. Lazima iwe yatosha kwa kila mtu kula, kwaiyo lazima wachukuwe nyama ya kutosha kulisha wote.
Ikiwa nyumba yoyote ina watu wachache wasioweza kumaliza huyo mwana-kondoo mzima, nyumba hiyo itabidi ishirikiane na nyumba ya jirani wa karibu, baada ya kuzingatia idadi ya watu waliomo. Mtaangalia ni kiasi gani cha nyama kitahitajika kulingana na mahitaji ya kila mtu.
5 Mwana kondoo wako au mbuzi wako mdogo lazima asiwe na upungufu, dume mwenye mwaka mmoja. Unaweza kuchukuwa mmoja wa kondoo au mbuzi.
Wanyama mtakaowachagua, lazima wawe wa kiume wa umri wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari, mwaweza kuwachukua kati ya kondoo au mbuzi.
6 Lazima umtunze mpaka siku ya kumi na nne ya huo mwezi. Kisha kusanyiko lote la Israeli lazima liwaue hawa wanyama jioni.
Tunzeni wanyama hao mpaka siku ya kumi na nne ya mwezi, ambapo lazima watu wa jumuiya yote ya Israeli wachinje wanyama hao wakati wa jioni.
7 Lazima uchukuwe baadhi ya damu na uweke kwenye sehemu mbili za mihimili ya milango na juu ya fremu za milango ambapo utalia hizo nyama.
Ndipo watakapochukua baadhi ya hiyo damu na kuipaka kwenye vizingiti vya juu na miimo ya milango ya nyumba ambamo watakula wana-kondoo hao.
8 Lazima ule hizo nyama usiku, baada ya kuchoma kwenye moto. Kula na mkate ulio andaliwa kwa hamira, pamoja na mimea michungu.
Usiku huo huo watakula nyama iliyookwa kwenye moto, pamoja na mboga chungu za majani na mikate isiyotiwa chachu.
9 Usiile mbichi au imechemshwa kwenye maji. Badala yake, choma kwenye moto na kichwa chake, miguu na sehemu za ndani.
Msile nyama mbichi wala iliyochemshwa, lakini iwe imeokwa kwenye moto, kichwa, miguu na nyama zake za ndani.
10 Usiache ata kidogo kubaki mpaka asubui. Lazima uchome chochote kilicho baki asubui.
Msibakize nyama yoyote mpaka asubuhi; nazo kama zitabakia mpaka asubuhi, lazima mziteketeze kwa moto.
11 Hivi ndivyo wa paswa kula: ukiwa umefunga mkanda wako, umevaa viatu vyako, na gongo lako mkononi mwako. Lazima ule kwa haraka. Ni Pasaka ya Yahweh.
Hivi ndivyo mtakavyokula: Mtajifunga mikanda viunoni, mtakuwa mmevaa viatu vyenu miguuni na kushika fimbo zenu mkononi mwenu. Mle kwa haraka; hii ni Pasaka ya Bwana.
12 Yahweh anasema hili: Nitaenda katika nchi ya Misri usiku na kushambulia wazaliwa wote wa kwanza wa wanadamu na wanyama katika nchi ya Misri. Nitaleta pigo kwa miungu yote ya Misri. Mimi ni Yahweh.
“Usiku huo huo nitapita katika nchi yote ya Misri na kumuua kila mzaliwa wa kwanza, wa wanadamu na wa wanyama, nami nitaihukumu miungu yote ya Misri. Mimi ndimi Bwana.
13 Damu itakuwa ishara kwenye nyumba zenu ya kuja kwangu. Nitakapo ona damu, nitapita nitakapo shambulia nchi ya Misri. Ili pigo halitawajia na kuwaharibu.
Damu itakuwa ishara kwa ajili yenu ya kuonyesha nyumba ambazo mtakuwamo; nami nitakapoiona damu, nitapita juu yenu. Hakuna pigo la uharibifu litakalowagusa ninyi nitakapoipiga Misri.
14 Hii siku itakuwa kumbukumbu kwenu, ambayo lazima muadhimishe kama sherehe ya Yahweh. Itakuwa sheria kwenu pia, kwenye vizazi vyote vya watu wenu, ambayo mwapaswa kuadhimisha leo.
“Siku hii itakuwa kumbukumbu kwenu, mtaiadhimisha kuwa sikukuu kwa Bwana, katika vizazi vyenu vyote: mtaishika kuwa amri ya kudumu.
15 Utakula mkate bila hamira wakati wa siku saba. Siku ya kwanza utaondoa hamira kwenye nyumba zenu. Yeyote atakaye kula mkate uliyotiwa chachu kwanzia siku ya kwanza mpaka siku ya saba, huyo mtu lazima akatwe kutoka Israeli.
Kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu. Katika siku ya kwanza mtaondoa chachu yote ndani ya nyumba zenu, kwa maana yeyote atakayekula chochote chenye chachu kuanzia siku ya kwanza hadi ya saba lazima akatiliwe mbali kutoka Israeli.
16 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko lililo tengwa kwa ajili yangu, na siku ya saba kutakuwa na kusanyiko kama hilo. Hakuna kazi itakayo fanywa hizi siku, zaidi ya kupika kila mmoja ale. Hiyo ndio kazi pekee itakayo fanywa na wewe.
Katika siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu, na kusanyiko jingine katika siku ya saba. Katika siku hizo msifanye kazi kamwe isipokuwa kutayarisha chakula cha kila mmoja; hilo ndilo tu mtakalofanya.
17 Lazima uadhimishe hii Sherehe ya Mkate Usiotiwa Chachu kwasababu ni siku hii ambayo nitawaleta watu wako, makundi yaliyo na silaha, kwa makundi yaliyo na silaha, kutoka nchi ya Misri. Lazima uadhimishe hii siku kwa vizazi vyote vya watu wako. Hii itakuwa sheria kwako.
“Mtaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, kwa sababu hiyo ndiyo siku ile niliyovitoa vikosi vyenu kutoka Misri. Mtaiadhimisha siku hii kwa vizazi vyenu vyote kuwa amri ya kudumu.
18 Lazima ule mkate usiotiwa chachu kuanzia jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza wa mwaka, mpaka jioni ya siku ya ishirini na moja ya mwezi.
Katika mwezi wa kwanza mtakula mikate isiyotiwa chachu, kuanzia jioni ya siku ya kumi na nne hadi jioni ya siku ya ishirini na moja.
19 Wakati wa hizi siku, nyumbani mwenu kusipatikane na hamira. Yeyote atakaye kula mkate ulio andaliwa na hamira lazima akatwe kutoka jamii ya Israeli, huyo mtu awe ni mgeni au mtu aliye zaliwa nchini mwenu.
Kwa muda wa siku saba isionekane chachu yoyote katika nyumba zenu. Yeyote alaye chochote chenye chachu ndani yake, lazima akatiliwe mbali kutoka jumuiya ya Israeli, akiwa ni mgeni au mzawa.
20 Hautakula chochote kilicho andaliwa na hamira. Popote utapo ishi, lazima ule mkate usio na hamira.”'
Msile chochote kilichotiwa chachu. Popote muishipo, ni lazima mle mikate isiyotiwa chachu.”
21 Kisha Musa akawaita viongozi wote wa Israeli na kuwaambia, “Nendeni na mchague mwana kondoo au mbuzi watakao tosha kulisha familia zenu na muue mwana kondoo wa pasaka.
Ndipo Mose akawaita wazee wote wa Israeli na kuwaambia, “Nendeni mara moja mkachague wanyama kwa ajili ya jamaa zenu, mkachinje mwana-kondoo wa Pasaka.
22 Kisha chukua jani la hisopu na uchovye kwenye damu itakayo kuwa kwenye beseni. Paka damu iliyo kwenye beseni juu ya fremu ya mlango na kwenye mihimili miwili ya mlango. Hakuna ata mmoja atakaye toka nje ya mlango wake mpaka asubui.
Chukueni kitawi cha hisopo, kichovyeni kwenye damu iliyopo kwenye sinia na kuipaka baadhi ya hiyo damu kwenye vizingiti na kwenye miimo yote miwili ya milango. Mtu yeyote asitoke nje ya mlango wa nyumba yake mpaka asubuhi.
23 Kwa kuwa Yahweh atapita kushambulia Wamisri. Atakapo ona damu juu ya fremu ya mlango na kwenye mihimili miwili ya mlango, atapita mlango wako na ata ruhusu mharibifu kuja nyumbani kwenu kuwashambulia.
Bwana apitapo katika nchi yote kuwapiga Wamisri, ataiona damu juu ya vizingiti na kwenye miimo ya milango, naye atapita juu, wala hatamruhusu mwangamizi kuingia katika nyumba zenu na kuwapiga ninyi.
24 Lazima uadhimishe hili tukio. Hili litakuwa daima sheria kwako na kwa uzao wenu.
“Shikeni maagizo haya yawe kanuni ya kudumu kwenu na kwa ajili ya wazao wenu.
25 Utakapo ingia nchi Yahweh atakayo kupa, kama alivyo ahidi kufanya, lazima uadhimishe hili tendo la ibada.
Mtakapoingia katika nchi Bwana atakayowapa kama alivyoahidi, shikeni desturi hii.
26 Watoto wako watakapo kuuliza, 'Hili tendo la ibada lina maana gani?'
Watoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’
27 kisha lazima useme, 'Ni sadaka ya Pasaka ya Yahweh, kwasababu Yahweh kapita nyumba za Waisraeli Misri alipo washambulia Wamisri. Aliweka nyumba zetu huru.”' Kisha watu wakamsujudia Yahweh.
Basi waambieni, ‘Hii ni dhabihu ya Pasaka kwa Bwana, ambaye alipita juu ya nyumba za Waisraeli katika nchi ya Misri na hakudhuru nyumba zetu alipowapiga Wamisri.’” Ndipo watu wa Israeli waliposujudu na kuabudu.
28 Waisraeli wakaenda na kufanya kama Yahweh alivyo waamuru Musa na Aruni.
Waisraeli wakafanya kama vile Bwana alivyomwagiza Mose na Aroni.
29 Ikawa usiku wa manane kuwa Yahweh akawashambulia wazaliwa wote wa kwanza wa nchi ya Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, aliye keti kiti chake cha enzi, mzaliwa wa kwanza wa mtu aliye gerezani na wazaliwa wote wa kwanza wa mifugo.
Ilipofika usiku wa manane, Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa, aliyekuwa gerezani, na wazaliwa wa kwanza wa mifugo yote pia.
30 Farao akaamka usiku - yeye, watumishi wake, na Wamisri. Palikuwa na kelele za maombolezo Misri, kwa kuwa hakukuwa na nyumba ambayo hamna mtu hakufa.
Farao, na maafisa wake wote, na Wamisri wote wakaamka usiku, na kulikuwa na kilio kikubwa katika nchi ya Misri, kwa kuwa haikuwepo nyumba ambayo hakufa mtu.
31 Farao akamuita Musa na Aruni usiku na kusema, “Inuka, tokeni miongoni mwa watu wangu, nyie pamoja na Waisraeli. Nenda, mmuabudu Yahweh, kama mlivyo sema mnataka kufanya.
Wakati huo Farao akawaita Mose na Aroni na kuwaambia, “Ondokeni! Tokeni kwa watu wangu, ninyi pamoja na Waisraeli! Nendeni mkamwabudu Bwana kama mlivyoomba.
32 Chukuweni ng'ombe zenu na kondoo zenu, kama mlivyo sema, na muende, na pia mnibariki.”
Chukueni makundi yenu ya kondoo na mbuzi pamoja na ngʼombe, kama mlivyosema, nanyi mwende zenu. Nanyi pia mnibariki.”
33 Wamisri walikuwa na haraka ya kuwa ondoa nchini, kwa kuwa walisema, “Sisi ni watu tuliokufa.”
Wamisri wakawahimiza Waisraeli waondoke kwa haraka na kuacha nchi yao. Kwa kuwa walisema, “La sivyo, tutakufa wote!”
34 Watu wakachukuwa ngano yao pasipo kuongeza hamira yeyote. Bakuli zao zakukandia ngano zilifungiwa kwenye nguo zao na kwenye mabega yao.
Hivyo watu wakachukua donge lao la unga kabla ya kutiwa chachu, wakaweka ndani ya mabakuli ya kukandia, wakayaviringisha katika vitambaa na kuyabeba mabegani mwao.
35 Watu Waisraeli walifanya kama Musa alivyo waambia. Waliwaomba Wamisri vitu vya fedha, vitu vya dhahabu, na nguo.
Waisraeli wakafanya kama Mose alivyowaelekeza, nao wakawaomba Wamisri wawapatie vitu vya fedha, dhahabu na nguo.
36 Yahweh aliwafanya Wamisri na shauku ya kuwapendeza Waisraeli. Hivyo Wamisri waliwapa chochote walicho waomba. Katika hili, Waisraeli waliwachukulia vingi Wamisri.
Basi Bwana alikuwa amewafanya Wamisri kuwa wakarimu kwa hawa watu, wakawapatia Waisraeli vile walivyotaka kwao; kwa hiyo wakawateka nyara Wamisri.
37 Waisraeli wakasafiri kutoka Ramesi kwenda Sakothi. Walikuwa na idadi ya wanaume 600, 000 kwa miguu, kuongezea kwa wanawake na watoto.
Waisraeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi. Walikuwepo wanaume wapatao 600,000 waendao kwa miguu bila kuhesabu wanawake na watoto.
38 Mchanganyiko wa kundi la wasio Waisraeli pia walienda nao, pamoja na ng'ombe na kondoo, idadi kumbwa ya mifugo.
Watu wengine wengi wakafuatana nao, pamoja na makundi makubwa ya mifugo wakiwemo kondoo, mbuzi na ngʼombe.
39 Walioka mikate na unga wa ngano wenye hamira walio utoa Misri. Ulikuwa hauna hamira kwasababu waliondolewa Misri na hawakuweza chelewa kuandaa chakula.
Wakatengeneza maandazi yasiyotiwa chachu kwa ule unga uliokandwa waliokuwa wameutoa Misri, donge hilo la unga halikuwa limetiwa chachu, kwa kuwa walikuwa wameondolewa Misri kwa haraka nao hawakuwa na muda wa kuandaa chakula chao.
40 Waisraeli waliishi Misri kwa miaka 430.
Waisraeli walikuwa wameishi Misri kwa muda wa miaka 430.
41 Baada ya miaka 430, siku hiyo hiyo, majeshi yote ya Yahweh yalio jiami waliondoka kutoka nchi ya Misri.
Ilikuwa ni siku ya mwisho ya hiyo miaka 430, vikosi vyote vya Bwana vilipokuwa vimeondoka Misri.
42 Huu ulikuwa usiku wakuwa macho, ili Yahweh awatoe kutoka nchi ya Misri. Huu ulikuwa usiku wa Yahweh wa kuadhimishwa na Waisraeli wote na watu wa vizazi vyao vyote.
Kwa sababu Bwana aliutenga usiku ule ili kuwatoa Waisraeli katika nchi ya Misri, katika usiku huu Waisraeli wote wanapaswa kuadhimisha kwa kukesha ili kumheshimu Bwana katika vizazi vijavyo.
43 Yahweh akamwambia Musa na Aruni, “Hii ni sheria ya Pasaka: hakuna mgeni anaye ruhusiwa kuila.
Bwana akamwambia Mose na Aroni, “Haya ndiyo masharti kwa ajili ya Pasaka: “Mgeni hataruhusiwa kula Pasaka.
44 Walakini, kila mtumwa wa Misraeli, aliye nunuliwa kwa pesa, anaeza kula baada ya kutahiriwa.
Mtumwa yeyote ambaye mmemnunua aweza kuila kama mmemtahiri,
45 Wageni na watumishi waajiriwa hawapaswi kula chakula chochote.
lakini kibarua yeyote au msafiri haruhusiwi kula.
46 Chakula chapaswa kuliwa ndani ya nyumba moja. Hauruhusiwi kubeba nyama yeyote nje ya nyumba, na hauruhusiwi kuvunja mfumba wowote.
“Sharti iliwe ndani ya nyumba; msichukue nyama yoyote nje ya nyumba hiyo. Msiuvunje mfupa wowote.
47 Jamii zote za Israeli za paswa kuadhimisha sherehe.
Jumuiya yote ya Israeli ni lazima waiadhimishe Pasaka hiyo.
48 Kama mgeni anaishi na wewe na anataka kuadhimisha Pasaka kwa Yahweh, ndugu zake wote wa kiume wapaswa kutahiriwa. Kisha anaeza kuja na kuadhimisha. Atakuwa kama watu walio zaliwa kwenye nchi. Walakini, hakuna mtu asiye tahiriwa anaruhusiwa kula chakula chochote.
“Mgeni aishiye miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka ya Bwana ni lazima wanaume wote waliomo nyumbani mwake wawe wametahiriwa, ndipo aweze kushiriki kama mzawa. Mwanaume yeyote asiyetahiriwa haruhusiwi kuila.
49 Sheria hii hii itahusika kwa mzaliwa wa asili na mgeni anayeishi miongoni mwenu.”
Sheria iyo hiyo itamuhusu mzawa na mgeni anayeishi miongoni mwenu.”
50 Waisraeli wote walifanya kama Yahweh alivyo waamuru Musa na Aruni.
Waisraeli wote walifanya kama vile Bwana alivyomwagiza Mose na Aroni.
51 Ikaja kuwa siku hiyo Yahweh akawaleta Israeli kutoka nchi ya Misri kwa makundi yalio jiami.
Siku ile ile Bwana akawatoa Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.

< Kutoka 12 >