< Esta 1 >
1 Katika siku za utawala wa Ahasuero (huyu ni Ahasuero aliyetawala toka India hadi Ethiopa, zaidi ya majimbo 127),
Hili ndilo lililotokea wakati wa utawala wa Mfalme Ahasuero, yule aliyetawala juu ya majimbo mia na ishirini na saba tangu Bara Hindi hadi Kushi.
2 katika siku hizo Mfalme Ahasuero aliketi katika kiti chake cha utawala katika ngome ya Shushani.
Wakati huo Mfalme Ahasuero alitawala katika kiti chake cha enzi katika ngome ya mji wa Shushani.
3 mwaka wa tatu wa utawala wake aliwaandalia sherehe viongozi na watumwa wake wote. Waliohudhuria katika sherehe hiyo walikuwa wakuu wa jeshi la Uajemi na Umedi, watu wenye vyeo, na viongozi wa majimbo.
Katika mwaka wa tatu wa utawala wake, alifanya karamu kwa ajili ya wakuu wake wote pamoja na maafisa. Akawaalika viongozi wa jeshi wa Uajemi na Umedi, wana wa wafalme na wakuu wa majimbo.
4 Mfalme akaweka wazi utajiri na utukufu wa ufalme wake na heshima ya ukufu wa ukuu alio upata kwa siku nyingi, kwa siku180.
Kwa siku zote 180 mfalme alionyesha utajiri mwingi wa ufalme wake, fahari na utukufu wa enzi yake.
5 Siku hizi zilipotimia, Mfalme aliaandaa karamu iliyodumu kwa siku saba. Karamu hii ilikuwa kwa watu wote walioishi katika ikulu ya Shushani, tangu mkubwa hadi mdogo. Behewa la bustani ya ikulu ya mfalme ndiyo karamu ilipofanyikia.
Siku hizo zilipopita, mfalme alifanya karamu kwa muda wa siku saba, katika bustani ya ndani katika jumba la kifalme, kwa ajili ya watu wote kuanzia mdogo hadi mkubwa, waliokuwa katika ngome ya mji wa Shushani.
6 Behewa la bustani lilipambwa kwa mapazia meupe ya pamba na urujuani, yalifungwa kwa kamba za kitani safi na zambarau, yakiwa yametundikwa kwa pete za fedha na nguzo za marimari. Kulikuwa na makochi ya dhahabu na fedha juu ya sakafu ya marimari, mawe mekundu na meupe, na ya manjano na meusi.
Bustani ilikuwa na mapazia ya kitani nyeupe na buluu, yaliyofungiwa kamba za kitani nyeupe na kitambaa cha zambarau, kwenye pete za fedha juu ya nguzo za marmar. Kulikuwepo viti vya dhahabu na vya fedha vilivyokuwa vimewekwa kwenye ile sakafu iliyotengenezwa kwa mawe ya rangi, marmar, lulumizi na mawe mengine ya thamani.
7 Vinywaji viliandaliwa katika vikombe vya dhahabu. Na kila kikombe kilikuwa ni cha kipekee na kwa sababu ya ukarimu wa mfalme kulikuwa mvinyo mwingi.
Vyombo vya dhahabu vilitumika kwa watu kunywea mvinyo, kila kimoja tofauti na kingine, naye mfalme akatoa mvinyo kwa wingi kwa kadiri ya ukarimu wake.
8 Mfalme aliwambia wahudumu watu wagawiwe vinywaji kwa kila mtu kulingana na matakwa yake. Maana tayari mfalme alikuwa ametoa agizo kwa watumishi wa ikulu kuwafanyia wageni kulingana na matakwa ya kila mgeni.
Kwa amri ya mfalme kila mgeni aliruhusiwa kunywa alichotaka, kwa kuwa mfalme alitoa maagizo kwa watumishi wote wa kuhudumu mvinyo kumhudumia kila mtu kwa jinsi alivyotaka.
9 Wanawake nao walikuwa wamealikwa katika karamu na Malkia Vashiti katika ikulu ya Mfalme Ahusuero.
Malkia Vashti pia akawafanyia wanawake karamu katika jumba la kifalme la Mfalme Ahasuero.
10 katika siku ya saba moyo wa mfalme ulipokuwa na furaha kwa sababu ya mvinyo, aliwaagiza Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkas (hawa saba ndio waliohudumu mbele ya mfalme)
Siku ya saba, wakati Mfalme Ahasuero alikuwa amesisimka roho yake kwa mvinyo, aliamuru matowashi saba waliokuwa wakimhudumia, yaani, Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkasi,
11 kumleta Malkia Vashiti akiwa katika mavazi yake ya kimalkia. Akiwa na lengo la kuwaonyesha watu na maakida urembo wake, maana alikuwa mrembo.
kumleta Malkia Vashti mbele ya mfalme akiwa amevaa taji lake la kifalme, ili aonyeshe uzuri wake kwa watu na wakuu, kwa kuwa alikuwa ni mzuri wa kupendeza.
12 Pamoja na maagizo ya Mfalme, Malkia Vashiti alikataa kwenda kama alivyokuwa amewaagiza viongozi wake. Hivyo mfalme akakasirika sana; ghadhabu yake ikawaka ndani yake
Lakini wakati watumishi walipotoa amri ya mfalme, Malkia Vashti alikataa kuja. Ndipo mfalme alighadhibika, na hasira yake ikawaka.
13 Mfalme akawandea wenye hekima, waliofahamu nyakati (kwa kuwa huu ndio uliokuwa utaratibu wa mfalme kuhusu wale waliokuwa watalaamu wa sheria na hukumu.
Kwa kuwa ilikuwa desturi ya mfalme kupata ushauri kwa wataalamu katika mambo ya sheria na haki, alizungumza na watu wenye busara, ambao walijua nyakati,
14 Carshena, Shethar, Admatha, Tarshish, Meres, Marsena, na Memucan, majimbo saba ya Uajemi na Umedi walikuwa karibu na mfalme na walikuwa na vyeo vikubwa katika ufalme.
nao waliokuwa karibu na mfalme ni Karshena, Shethari, Admatha, Tarshishi, Meresi, Marsena na Memukani, wakuu saba wa Uajemi na Umedi waliokuwa na nafasi ya pekee kwa mfalme nao walikuwa na vyeo vya juu kabisa katika utawala wake.
15 Katika kutafsiri nini kifanyike kwa mjibu wa sheria kutoka na mgomo wa Malkia Vashiti dhidi ya agizo la mfalme Ahusiero kwa Malkia Vashiti.
Mfalme akauliza, “Kulingana na sheria, Malkia Vashti anapaswa kutendewa nini? Malkia hakutii amri ya Mfalme Ahasuero ambayo matowashi walimpelekea.”
16 Mmoja wao aliyejulikana kwa jina la Memukani alisema mbele ya Mfalme na mbele ya viongozi, Malkia Vashiti hajamkosea tu mfame na wakuu na watu wote walio katika majimbo ya mfale Ahusiero.
Kisha Memukani akajibu mbele ya mfalme na wakuu, “Malkia Vashti si kwamba amemkosea mfalme tu bali pia amewakosea wakuu wote na watu wa himaya yote ya Mfalme Ahasuero.
17 kwa kuwa jambo la malkia litafahamika kwa wanawake wote. watawatendea waume zao vibaya. Watasema, 'Mfalme Ahusiero Malkia Vashiti hakumtii mme wake, Mfalme Ahusiero alipotaka ahudhurie mbele yake.'
Kwa maana tendo hili la malkia litajulikana kwa wanawake wote, kwa hiyo watawadharau waume zao na kusema, ‘Mfalme Ahasuero aliagiza Malkia Vashti aletwe mbele yake, lakini alikataa.’
18 Kabla ya siku hii wanawake wa wakuu wa Uajemi na Umedi walipata taarifa ya mgomo wa malkia Vashiti watawatendea waume zao, viongozi wa mfalme. kutakuwa na ghasia na nyingi hasira.
Leo hii wanawake wa wakuu wa Uajemi na Umedi ambao wamesikia juu ya tabia ya malkia watawatendea wakuu wote wa mfalme vivyo hivyo. Hapatakuwepo na mwisho wa dharau na magomvi.
19 kama ni jambo jema kwa mfalme, ruhusu tangazo litolewe, na iwe katika sheria ya Waajemi na Wamedi, ambao haiwezi kutanguliwa, kwamba Vashiti hatakuja tena mbele za mfalme kama malkia. Nafasi ya Vashiti apewe mwingine ambaye ni bora zaidi ya Vashiti.
“Kwa hiyo, kama itampendeza mfalme, atoe amri ya kifalme na iandikwe katika sheria ya Uajemi na Umedi, ambayo haitabadilika, kwamba Vashti kamwe asije tena mbele ya Mfalme Ahasuero. Pia mfalme na atoe hiyo nafasi yake ya umalkia kwa mwanamke mwingine aliye bora kumliko yeye.
20 Tangazo la mfalme litakapotolewa katika ufalme wote, wanawake wote watawaheshimu waume zao, tangu mwenye cheo hadi asiye na cheo.”
Kisha mbiu hii ya mfalme itakapotangazwa katika himaya yake iliyo kubwa sana, wanawake wote watawaheshimu waume zao, kuanzia mdogo hadi mkubwa.”
21 Ushauri huu ulikuwa mzuri kwa mfalme na wakuu wengine, mfalme akafamya kama Memkani alivyopendekeza.
Mfalme na wakuu wake walipendezwa na shauri hili, hivyo basi mfalme akafanya kama Memukani alivyopendekeza.
22 Akatuma barua katika majimbo yote ya mfalme, kwa kilajambo na andiko lake, na watu kwa makabila yao. Aliamuru kwamba kila mme awe msimamizi katika nyumba yake mwenyewe. Tangazo hili lilitolewa katika lungha ya kila mtu katika ufalme.
Alipeleka barua katika sehemu zote za ufalme wake, kwa kila jimbo kwa maandishi yake mwenyewe na kwa kila watu katika lugha yao wenyewe, akitangaza kwa msemo wa kila watu kwamba inampasa kila mwanaume kuwa mtawala wa nyumba yake mwenyewe.