< Esta 9 >

1 Sasa katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya kumi na tatu ambayo ni siku ya Adari, siku ambayo adui wa Wayahudi walitarajia kutekeleza sheria ya mfalme na kupata nguvu dhidi ya Wayahudi. Badala yake Wayahudi wakapata nguvu dhidi ya adui zao.
Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari, amri iliyoagizwa na mfalme ilikuwa itekelezwe. Siku hii adui wa Wayahudi walikuwa wametumaini kuwashinda, lakini sasa mambo yaliwageukia na Wayahudi wakawashinda wale waliokuwa wanawachukia.
2 Wayahudi wote wakakusanyika katika miji yao katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, kutia mikono juu ya wale waliokusudia ubaya. Hakuna aliye kuwa tayari kusimama zao kwa sababu hofu yao ilikuwa imewaangukia watu wote.
Wayahudi walikusanyika katika miji yao, katika majimbo ya Mfalme Ahasuero kuwashambulia wale waliokuwa wanatafuta kuwaangamiza. Hakuna yeyote aliyeweza kushindana nao, kwa sababu watu wa mataifa mengine yote waliwaogopa.
3 Wakuu wote wa majimbo, maakida na magavana, na watawala wa mfalme, waliwasaidia Wayahudi kwa kuwa hofu ya Modekai ilikuwa imewaangukia.
Nao wakuu wote wa majimbo, majemadari, watawala na maafisa wa mfalme wakawasaidia Wayahudi, kwa sababu walimhofu Mordekai.
4 Kwa kuwa Modekai alikuwa mkuu katika nyumba ya mfalme, na umaarufu wake ukasambaa katika majimbo yote, kwa kuwa Modekai alikuwa akifanyika mkuu.
Mordekai alikuwa mtu mashuhuri katika jumba la mfalme; sifa zake zilienea katika majimbo yote naye alipata uwezo zaidi na zaidi.
5 Wayahudi wakawavamia maadi zao kwa upanga, wakiwatenda vibaya kama walivyokuwa wamekusudiwa mabaya dhidi yao Wakawatenda kama walivyo ona vyema machoni pao.
Wayahudi waliwaangusha adui zao wote kwa upanga wakiwaua na kuwaangamiza, nao walifanya kile walichotaka kwa wale waliowachukia.
6 Katika ngome ya mji wa Shushani pekee jumla ya maadui waliouawa na na kuharibiwa na Wayahudi ni wanaume mia tano.
Katika ngome ya Shushani Wayahudi waliua na kuangamiza wanaume 500.
7 Miongoni mwa waliouawa ni pamoja na Parishandatha, Dalphoni, Aspatha,
Pia waliwaua Parshendatha, Dalfoni, Aspatha,
8 Poratha, Adalia, Aridatha,
Poratha, Adalia, Ardatha,
9 Parimashita, Arisai, Aridai, Vaizatha,
Parmashta, Arisai, Aridai na Waizatha,
10 na wana kumi wa Hamani, mwana wa Hammedatha, adui wa Wayahudi. Lakini hawakuchua mateka yoyote.
wana kumi wa Hamani mwana wa Hamedatha, adui wa Wayahudi. Lakini hawakuchukua nyara.
11 Idadi ya wale waliouawa siku hiyo katika mji wa Shushani, ilifikishwa kwa Mfalme Ahusiero.
Mfalme aliarifiwa siku iyo hiyo hesabu ya waliouawa katika ngome ya Shushani.
12 Mfalme akamwambia malkia Esta. Mfalme akamwambia Malkia Esta, “Wayahudi wameua wanaume mia tano katika mji wa Shushani, wakiwemo wana kumi wa Hamani adui wa Wayahudi. Je wamefanya nini katika majimbo mengine? Na sasa haja yako ni nini? Utapewa. Ombi lako ni nini?”
Mfalme akamwambia Malkia Esta, “Wayahudi wamewaua wanaume 500 na wana kumi wa Hamani ndani ya ngome ya Shushani. Wamefanyaje katika majimbo mengine ya mfalme yaliyobaki? Je, sasa haja yako ni nini? Nayo pia utapewa. Nalo ombi lako ni nini? Nalo utafanyiwa.”
13 Esta akamjibu, “Mfalme kama ikikupendeza, ruhusu Wayuadi walio katika mji wa Shushani wapige mbiu hii na kesho, na miili ya watoto wa Hamani itundikwe juu ya miti.”
Esta akajibu, “Ikimpendeza mfalme, uwape ruhusa Wayahudi walioko Shushani warudie amri ya leo kesho pia, na wana wa Hamani kumi wanyongwe mahali pa kunyongea watu.”
14 Mfalme akaamuru ombi la Esta litekelezwe. Mbiu ilipigwa katika mji wa Shushani, na wana kumi wa Hamani wakatundikwa juu ya miti.
Basi mfalme akaamuru kwamba hili litendeke. Amri ilitolewa huko Shushani, nao wakawanyonga wana kumi wa Hamani.
15 Wayahudi katika mji wa Shushani walisanyika pamoja siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, na kuwaua maadui zao mia tatu katika mji wa Shushani, lakini hawakugusa nyara zao.
Wayahudi huko Shushani wakakusanyika pamoja siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, nao wakawaua wanaume 300 huko Shushani, lakini hawakuchukua nyara zao.
16 Na Wayahudi katika majimbo mengine wakakusanyika ili kujilinda na wakapata faraja kutoka kwa maadui na wakawaua maadui zao elfu sabini na tano, lakini hawakugusa mikono yao kwa vitu vya thamani wale waliouwawa.
Wakati ule ule, Wayahudi wengine waliokuwa kwenye majimbo ya mfalme, wakakusanyika kujilinda nao wakapata nafuu kutokana na adui zao. Waliua adui zao wapatao 75,000 lakini hawakugusa nyara zao.
17 Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa Adari, Wayahudi wakapumzika katika siku ya kumi na nne, wakapumzika siku hiyo ya karamu na furaha.
Hili lilitendeka siku ya kumi na tatu ya mwezi wa Adari na siku ya kumi na nne walipumzika na kuifanya siku ya karamu na furaha.
18 Lakini Wayahudi walioishi katika mji wa Shushani wakaja pamoja siku ya kumi na tatu na ya kumi na nne. Na siku ya kumi na tano wakapumzika na wafanya karamu na kufurahia.
Wayahudi huko Shushani, hata hivyo, walikuwa wamekusanyika siku ya kumi na tatu na ya kumi na nne, pia siku ya kumi na tano walipumzika na kuifanya siku ya karamu na furaha.
19 Hii ndiyo sababu Wayahudi wa vijijini, wanaishi maeneo ya vijijini, huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na karamu na siku ambayo hutumiana zawadi kwa kila mmoja.
Ndiyo sababu Wayahudi wanaokaa vijijini na katika miji midogo huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na karamu, siku ambayo wao hupeana zawadi mmoja kwa mwingine.
20 Modekai akaweka mambo haya na akatuma nyaraka kwa Wayahudi wote waliokuwa katika utawala wa Mfalme Ahusiero,
Mordekai aliandika matukio haya, naye akapeleka barua kwa Wayahudi wote walioko katika majimbo ya Mfalme Ahasuero, majimbo yaliyo mbali na karibu,
21 akiwataka kuazimisha siku ya kumi na nne na kumi na tano ya mwezi wa Adari kila mwaka.
akiwataka kila mwaka washerehekee siku ya kumi na nne na ya kumi na tano ya mwezi wa Adari
22 Hizi zilikuwa ndizo siku ambazo Wahudi walipata faraja kutoka kwa maadui zao na wakati huu ndio wakati ambao huzuni ya Wayahudi iligeuzwa kuwa furaha, na kutoka kwa maombolezo hadi kwenye pumziko. Walipaswa kuzifanya siku za karamu na furaha, na kutumiana zawadi ya chakula, na zawadi kwa masikini.
kama wakati ambao Wayahudi walipata nafuu kutoka kwa adui zao na kama mwezi ambao huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha na kuomboleza kwao kuwa siku ya kusherehekea. Aliwaandikia kushika siku hizo kama siku za karamu na za furaha na kupeana zawadi za vyakula wao kwa wao na zawadi kwa maskini.
23 Wayahudi wakaendelea na maadhimisho wakifanya kile ambacho Modekai alikuwa amewaandikia.
Hivyo Wayahudi walikubali kuendeleza sherehe walizokuwa wamezianza, wakifanya lile Mordekai alilokuwa amewaandikia.
24 Na wakati huo Modekai mwana wa Hammedatha mwagagi, adui wa Wayahudi aliyekuwa amepanga njama ya kuwaangamiza Wayahudi, na kwa kupiga Puri (yaani akapiga kura) ili kuwaangamiza kabisa.
Kwa maana Hamani mwana wa Hamedatha Mwagagi, adui wa Wayahudi wote, alikuwa amepanga hila dhidi ya Wayahudi ili kuwaangamiza, na alikuwa amepiga puri (yaani kura) kwa ajili ya maangamizi na uharibifu wao.
25 Lakini Mfalme Ahusiero alipopata taarifa ya mpango mbaya huu alioupanga Modekai dhidi ya Wayahudi, aliagiza kwa nyaraka afanyiwe Modekai mwenyewe, na kwamba yeye na wana wake wanyongwe juu ya miti.
Lakini wakati shauri hilo baya lilipoarifiwa kwa mfalme, alitoa amri iliyoandikwa kwamba mipango mibaya ambayo Hamani ameipanga dhidi ya Wayahudi inapasa imrudie juu ya kichwa chake mwenyewe, na kwamba yeye na wanawe waangikwe mahali pa kunyongea watu.
26 Hivyo Wayahudi wakaziita siku hizi Purimu, kutokana na jina Puri. Kwa sababu ya mambo yote yaliyo kuwa yameandika katika barua, na mambo yote ambayo walikuwa wameyaona kwa macho yao, na yale yalikuwa yamewapata,
(Kwa hiyo siku hizi ziliitwa Purimu, kutokana na neno puri.) Kwa sababu ya kila kitu kilichoandikwa kwenye barua hii na kwa sababu ya yale waliyoyaona na yale yaliyowatokea,
27 Wayahudi wakapokea jukumu na desturi mpya. Desturi hii iwe kwa ajili yao, watoto wao, na kila ambaye aliyeungana nao. Na itakuwa kwamba maadhimisho haya watayafanya kwa kila mwaka. Wataadhimisha kwa namna fulani na nyakati hizo hizo kila mwaka.
Wayahudi wakachukua na kuifanya desturi kwamba wao na wazao wao na wote ambao walijiunga nao wangefanya bila kuacha kushika siku hizi mbili kila mwaka, kwa njia ilivyoelekezwa na kwa wakati wake.
28 Siku hizi zilipaswa kuadhimishwa katika kila kizazi, kila familia, kila jimbo na kwa kila mji. Wayahudi hawa na watoto wao hawakuacha kuadhimisha siku hizi za Purimu, ili kwamba wasizisahau.
Siku hizi zinapasa zikumbukwe na kuadhimishwa katika kila kizazi, kila jamaa na katika kila jimbo na kila jiji. Nazo siku hizi za Purimu kamwe zisikome kusherehekewa na Wayahudi, wala kumbukumbu zake zisipotee miongoni mwa wazao wake.
29 Malkia Esta na Modekai wakaandika kwa mamlaka yote na kuthibitisha barua hii ya pili kuhusu Purimu.
Basi Malkia Esta binti Abihaili, pamoja na Mordekai, Myahudi, waliandika kwa mamlaka yote kuthibitisha barua hii ya pili kuhusu Purimu.
30 Barua zilipelekwa katika majimbo 127 ya mfalme Ahusiero, zikiwatakia Wayahudi wote amani na kweli.
Naye Mordekai akatuma barua kwa Wayahudi wote katika majimbo 127 ya ufalme wa Ahasuero, barua zenye maneno ya amani na matumaini,
31 Na kuthibitisha siku za Purimu sawa sawa na maelekezo ya Modekai na Esta yaliyowataka Wayahudi waadhimishe. Wayahudi wakatii maagizo kwa ajili yao na uzao wao, kama walivyotii siku za kufunga na kuomboleza.
ili kuimarisha siku hizi za Purimu katika majira yake yaliyowekwa, kama Mordekai, Myahudi na Malkia Esta walivyowaamuru, na walivyojiimarisha wenyewe na wazao wao kuhusu nyakati za kufunga na kuomboleza.
32 Agizo la Esta likahakikisha sheria hizi kuhusu Purimu, na ikaandikwa katika kitabu.
Amri ya Esta ilithibitisha taratibu hizi kuhusu Purimu, nayo ikaandikwa katika kumbukumbu.

< Esta 9 >