< Esta 8 >

1 Siku hiyo Mfalme Ahusiero akampa Malkia Esta mali yote ya Hamani, adui wa Wayahudi. Na kisha akampandisha cheo Modekai ili atumike mbele zake, kwa sababu Malkia Esta alikuwa amemueleza Mfalme uhusiano wake na Modekai.
Siku ile ile Mfalme Ahasuero akampa Malkia Esta shamba la Hamani, adui wa Wayahudi. Naye Mordekai akaja mbele ya mfalme, kwa kuwa Esta alikuwa amesema jinsi anavyohusiana naye.
2 Kisha Mfalme akampa pete yake aliyokuwa amempa Hamani. Malkia Esta akampandisha Modekai ili awe mkuu katika shamba la Hamani.
Mfalme akaivua pete yake ya muhuri, ambayo alikuwa amemnyangʼanya Hamani, akampa Mordekai, naye Esta akamweka Mordekai juu ya shamba la Hamani.
3 Kisha Esta akaongea tena na mfalme. Akaanguka chini na kulia mbele za mfalme akimsihi Mfalme abatilishe njama ya kuwaua Wayahudi wote iliyokuwa imetangazwa na Hamani Muagagi
Esta alimsihi tena mfalme, akianguka miguuni pake na kulia. Akamwomba akomeshe mpango mwovu wa Hamani Mwagagi ambao alikuwa ameupanga dhidi ya Wayahudi.
4 kisha mfalme akamnyoshea Esta fimbo yake ya dhahabu, akainuka na kusimama mbele ya mfalme.
Kisha mfalme alimnyooshea Esta fimbo yake ya utawala ya dhahabu naye aliinuka na kusimama mbele yake.
5 Esta akasema, “Kama ikikupendeza na kama nimepata kibali mbele zako, agiza mbiu ipigwe ili kubatilisha barua zilizoandikwa na Hamani mwana wa Hammedatha muagagi, barua alizoziandika ili kuwa angamiza Wayahudi wote walikuwa katika majimbo yote ya mfalme.
Esta akasema, “Kama ikimpendeza mfalme, nami kama nikipata kibali naye akiona ni jambo lililo sawa kunitendea na kama akipendezwa nami, basi iandikwe amri ya kuzitangua barua zile Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuandika kuangamiza Wayahudi katika majimbo yote ya mfalme.
6 Ninawezaje kuona ubaya ukiwapa watu wangu? Ninawezaje kutazama uharibifu wa jamaa zangu?”
Kwa maana nitawezaje kuvumilia kuona maafa yakiwapata watu wangu? Nitawezaje kuvumilia kuona maangamizi ya jamaa yangu?”
7 Mfalme Ahusiero akamwambia Esta na Modekai, Muyahudi, tazama nimempa Esta nyumba yote ya Hamani na wamemtundika Hamani katika mti kwa sababu alikuwa amekusudia kuwaangamiza Wayahudi wote.
Mfalme Ahasuero akawajibu Malkia Esta na Mordekai Myahudi, “Kwa sababu Hamani aliwashambulia Wayahudi, nimetoa shamba la Hamani kwa Esta, naye ameangikwa kwenye mti wa kunyongea.
8 Hivyo andika mbiu nyingine kwa ajili ya Wayahudi kwa jina la mfalme na uipige muhuri kwa pete ya mfalme. Kwa sababu mbiu imekwisha andikwa kwa jina la mfalme na kugongwa muhuri kwa pete ya mfamle na haiwezi kubatilishwa.”
Basi andika amri nyingine kwa jina la mfalme kwa ajili ya Wayahudi kama unavyoona vyema, kisha uifunge kwa kutia muhuri kwa pete ya mfalme kwa kuwa hakuna andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa muhuri kwa pete ya mfalme linaloweza kutanguliwa.”
9 Kisha waandishi wa mfalme wakakusanyika kwa wakati huo huo katika mwezi wa tatu, ambao ni mwezi wa Sivani, siku ya ishirini ya mwezi wa tatu. Mbiu iliandikwa yote ambayo Modekai aliyaamuru kwa Wayahudi watendewe na wenyeji wa kila jimbo. Mbiu iliandikwa kwa maakida magavana na wakuu wa majimbo yote yaliyokuwa toka India hadi Ethiopia, majimbo 127 kila jimbo iliandikwa kuwa maandishi yake, na kila watu kwa lugha yao, na kwa Wayahudi kwa maandishi na lugha yao.
Mara moja waandishi wa mfalme wakaitwa kwenye siku ya ishirini na tatu, mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani. Wakaandika yote Mordekai aliyoamuru kwa Wayahudi, kwa majemadari, watawala na wakuu wa majimbo 127 kuanzia Bara Hindi mpaka Kushi. Maagizo haya yaliandikwa kwa maandishi ya kila jimbo na kwa lugha ya kila mtu pia kwa Wayahudi kwa maandishi yao wenyewe na lugha yao.
10 Modekai akaandika kwa jina la Mfalme Ahusiero na akazipiga muhuri kwa pete ya mfalme. Akapeleka nyaraka kwa matarishi, akawapandisha kwenye farasi waendao kwa haraka waliotumika kwa huduma ya mfalme, waliozaliwa kwa mfalme.
Mordekai aliandika nyaraka kwa jina la Mfalme Ahasuero, akazitia muhuri kwa pete ya mfalme na kuzipeleka kwa njia ya matarishi, ambao waliendesha farasi waendao kasi waliozalishwa maalum kwa ajili ya mfalme.
11 Mfalme akawapa Wayahudi wote katika majimbo ya utawala wake kibali cha kukusanyika na kujilinda na ruhusa ya kuangamiza, kuua na kuharibu mtu yeyote aliyekuwa na kusudi la kuwaua Wayahudi wote na kupora mali zao.
Waraka wa mfalme uliwaruhusu Wayahudi katika kila mji kuwa na haki ya kukusanyika na kujilinda wenyewe; kuharibu, kuua na kuangamiza jeshi lolote, taifa lolote au jimbo lile litakalowashambulia wao, wake zao, watoto wao na kuteka mali za adui zao.
12 Jambo hili lilipaswa litekelezwe katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, siku ya ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ambao ni mwezi wa Adari.
Siku ambayo iliwekwa kwa Wayahudi kufanya hili katika majimbo yote ya Mfalme Ahasuero ilikuwa siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari.
13 Nakala ya mbiu ilipaswa kutolewa kama sheria na kutangazwa kwa watu wote. Wayahudi walikuwa tayari kwa siku hiyo kulipa kisasi kwa adui zao.
Nakala ya tangazo ilikuwa itolewe kama sheria katika kila jimbo na iweze kujulikana kwa watu wa kila taifa, ili kwamba Wayahudi wawe tayari siku hiyo kulipiza kisasi kwa adui zao.
14 Hivyo matarishi wakaendesha farasi waliokuwa wakitumiwa katika huduma za kifalme. Walienda kwa haraka sana. Mbiu hii pia ilikuwa imetolewa katika mji wa Shushani pia.
Matarishi, wakiwa wamepanda farasi wa kifalme, walitoka mbio wakichochewa na agizo la mfalme. Tangazo lilitolewa pia katika ngome ya mji wa Shushani.
15 Kisha Mosekai akaondoka mbele za mfalme akiwa amevaa mavazi ya kifalme, nguo buluu na nyeupe na taji kubwa ya dhahabu na joho la zambarau. Mji wa Shushani ukafurahia.
Mordekai akaondoka mbele ya mfalme akiwa amevaa mavazi ya kifalme ya buluu na nyeupe, taji kubwa la dhahabu na joho la zambarau la kitani safi. Na mji wa Shushani ukasherehekea kwa furaha.
16 Wayahudi walikuwa na nuru, na furaha na heshima. Mji wowote ambao mbiu hii ilipigwa, Wayahudi walifurahia na walifanya karamu na pumziko.
Kwa maana kwa Wayahudi ulikuwa wakati wa raha na furaha, shangwe na heshima.
17 Watu wengi wakatamani kuwa Wayahudi sababu ya hofu ya Wayahudi iliyokuwa juu yao.
Katika kila jimbo na katika kila jiji, popote waraka wa mfalme ulipofika, kulikuwepo furaha na shangwe miongoni mwa Wayahudi, pamoja na karamu na kushangilia. Na watu wengi wa mataifa mengine wakajifanya Wayahudi kwa sababu ya kuwahofu Wayahudi.

< Esta 8 >