< Esta 7 >
1 Kwa hiyo mfalme na Hamani wakaenda kausherekea na malkia Esta.
2 Katika siku ya pili, baada ya kuletwa mvinyo, mfalme akamwambia Esta, “Ni nini haja ya moyo wako? Na nini ombi lako? Hata nusu ya ufalme wangu utapewa.”
3 Kisha Malkia amwambia mfalme, kama nimepata kibali machoni pako, na kama ikikupendeza, nipewe maisha yangu, na hili ndio haja ya moyo wangu, na hili pia ni ombi kwa watu wangu pia.
4 Kwa kuwa mimi na watu wangu tumeuzwa, ili tuharibiwe, tuuwawe, na tungamizwe. Kama tungeuzwa utumwani, kama wanaume na wanawake, ningenyamaza kimya, na nisingeweza kumsumbua mfame.”
5 Kisha Mfalme Ahusiero akamwambia malkia Esta, “Ni nani huyo? Ni nani aliyekusudia moyoni mwake kutenda jambo hili?
6 Esta akasema, “Ni huyu mwovu Hamani, adui!” Hamani akashikwa na Hofu mbele za mfalme na malkia.
7 Na kwa ghadhabu mfalme akatoka karamuni katika sehemu ya mvinyo na akaenda katika bustani ya ikulu, Lakini Hamani alibaki akimsihi Malkia Esta ili aokoe maisha yake. Kwa sababu aliona mfalme amemkusudia ubaya.
8 Mfalme akarudi kutoka katika bustani ya ikulu, na kuingia katika chumba ambamo kulikuwamo mvinyo. Hamani alikuwa ameanguka chini ya kochi alilokuwa ameketi Esta. Mfalme akakasirika na kusema, “atamdharirisha malkia mbele zangu katika nyumba yangu?” Mara tu maneno haya yalipotoka kinywani mwa mfalme, watumizhi wakafunika uso wa Hamani.
9 Kisha Habona, mmoja wa watumishi aliye mtumikia mfalme akamwambia mfalme, “Mti wenye urefu wa futi hamsini uko nyumbani kwa Hamani. Ulikuwa umeandaliwa kwa ajili ya Modekai, aliye toa taarifa kuhusu mpango wa kuangamizwa kwako.” Mfalme akesema,”Mtundikeni Hamani juu yake.”
10 Kwa hiyo wakamtundika Hamani kwenye mti aliuandaa kwa ajili ya Modekai. Na hasira ya mfalme ikatulia.