< Esta 4 >

1 Modeka aliposikia kilichokuwa kimepangwa dhidi yao, alirarua mavazi yake na kuvaa maguni na majivu. Akaenda katikati mwa mji na kulia kwa sauti na uchungu mwingi.
末底改知道所做的這一切事,就撕裂衣服,穿麻衣,蒙灰塵,在城中行走,痛哭哀號。
2 Akaenda hadi langoni mwa mfalme; kwa sababu hakuna aliye ruhusiwa kuingia akiwa amevaa magunia.
到了朝門前停住腳步,因為穿麻衣的不可進朝門。
3 Amri hii ilipofika katika kila jimbo, kulikuwa na kilio kikubwa kwa Wayahudi, na kufunga, kulia na maombolezo. Wengi wao walilala katika magunia na majivu.
王的諭旨所到的各省各處,猶大人大大悲哀,禁食哭泣哀號,穿麻衣躺在灰中的甚多。
4 Malkia Esta alipopata habari kutoka kwa wahudumu wake, alipatwa na majonzi. Akatuma watu wampelekee nguo Modekai ili avue magunia na kuvaa nguo nzuri, lakini Modekai hakukubali.
王后以斯帖的宮女和太監來把這事告訴以斯帖,她甚是憂愁,就送衣服給末底改穿,要他脫下麻衣,他卻不受。
5 kisha Esta akamwita Hathaki, mmoja wa wasimamizi wa mfalme, ambaye alikuwa amepewa wajibu wa kumuhudumia. Akamwagiza kwenda kwa Modekai ili afahamu kwa nini Modekai ameamua kufanya hivyo.
以斯帖就把王所派伺候她的一個太監,名叫哈他革召來,吩咐他去見末底改,要知道這是甚麼事,是甚麼緣故。
6 Hivyo Hathaki akaenda kwa Modekai katika mji mbele ya lango la mfalme.
於是哈他革出到朝門前的寬闊處見末底改。
7 Modekai akamweleza Hathaki mambo yote kuhusu maangamizi ya Wayahudi yaliyo pangwa na kiasi cha fedha ambacho Hamani ameahidi kuwapa wahazini wa mfalme, ili kuwaua Wayahudi.
末底改將自己所遇的事,並哈曼為滅絕猶大人應許捐入王庫的銀數都告訴了他;
8 Na kisha akampa nakala ya mbiu ambayo ilitolewa Shushani kwa uangamivu wa Wayahudi. Alifanya hiivyo ili kwamba Hathaki amwambie Esta achukue jukumu la kwenda na kumuomba mfalme na kumsihi kwa niaba ya Wayahudi.
又將所抄寫傳遍書珊城要滅絕猶大人的旨意交給哈他革,要給以斯帖看,又要給她說明,並囑咐她進去見王,為本族的人在王面前懇切祈求。
9 Hivyo, Hathaki akaenda na kumweleza Esta kile alicho ambiwa na Modekai.
哈他革回來,將末底改的話告訴以斯帖;
10 Esta akaongea na Hathaki na akamwambia arudi kwa Modekai.
以斯帖就吩咐哈他革去見末底改,說:
11 Esta akamwambia Hathaki, “Watumishi wote wa mfalme na watu wote katika majimbo yote wanafahamu kuwa mtu yeyote aingiae kwa mfalme bila kibali anapaswa kufa isipokuwa yule ambaye mfalme atamunyoshea fimbo yake ya dhahabu. Ni siku thelathini sasa sijaenda mbele ya mfalme.
「王的一切臣僕和各省的人民都知道有一個定例:若不蒙召,擅入內院見王的,無論男女必被治死;除非王向他伸出金杖,不得存活。現在我沒有蒙召進去見王已經三十日了。」
12 Hathaki akamwambia Modekai maneno aliyoambiwa na Esta.
人就把以斯帖這話告訴末底改。
13 Modekai akarudisha ujumbe: “usifikiri kwamba wewe utasalimika kuliko Wayahudi wote.
末底改託人回覆以斯帖說:「你莫想在王宮裏強過一切猶大人,得免這禍。
14 Kama ukikaa kimya kwa wakati huu, Mungu ataleta wokovu kwa njia nyingine, lakini wewe na nyumba ya baba yako mtaangamia. Ni nani ajuaye umekuja katika nafasi hii kwa wakati muafaka kama huu.
此時你若閉口不言,猶大人必從別處得解脫,蒙拯救;你和你父家必致滅亡。焉知你得了王后的位分不是為現今的機會嗎?」
15 Kisha Esta akatuma ujumbe kwa Modekai,
以斯帖就吩咐人回報末底改說:
16 “Nenda, uwakusanyea Wayahudi wote wanaoishi katika mji wa Shushani, na wafunge kwa ajili yangu. Wasile wala kunywa kwa muda wa siku tatu. Mimi na watumishi watumishi wangu wa kike tutafunga kwa siku hizo. Na kisha nitaenda mbele ya mfalme kinyume cha sheria. Na kama nitakufa na nife.
「你當去招聚書珊城所有的猶大人,為我禁食三晝三夜,不吃不喝;我和我的宮女也要這樣禁食。然後我違例進去見王,我若死就死吧!」
17 Modekai akaenda na akafanya yote ambayo Esta aliyo mwagiza kufanya.
於是末底改照以斯帖一切所吩咐的去行。

< Esta 4 >