< Esta 2 >
1 Baada ya mambo haya na baada ya hasira ya mfalme Ahusiero kutulia, alifikiri kuhusu Malkia Vashiti na alichokuwa amekifanya na tangazo alilokuwa ameamuru litolewe ya Vashiti kupoteza sifa za kuwa malkia.
Baadaye, wakati hasira ya Mfalme Ahasuero ilikuwa imetulia, alimkumbuka Vashti na kile alichokuwa amekifanya na alilokuwa ameamuru juu yake.
2 Kisha vijana waliomtumikia mfalme wakasema, mfalme atafutiwemabikira warembo.
Kisha watumishi waliomhudumia mfalme walipendekeza, “Na ufanyike utafiti kwa ajili ya wanawali mabikira wazuri wa sura kwa ajili ya mfalme.
3 Mfalme na achague wasimamizi katika majimbo yote ya ufalme wake, ili wawakusanye mabikira warembo wote harem katika ikulu ya Susa. Mabikira hawa wawe chini ya usimamizi wa Hegai, msimamizi, ambaye ni mkuu wa wanawake, na wapewe vipodozi vyao vyote.
Mfalme na ateue maafisa katika kila jimbo la himaya yake kuwaleta hao wanawali wote wazuri wa sura katika nyumba ya wanawake katika ngome ya mji wa Shushani. Kisha wawekwe chini ya utunzaji wa Hegai, towashi wa mfalme, msimamizi wa wanawake; na wapewe matunzo yote ya urembo.
4 Na binti yule atakaye mfurahisha mfalme ndiye atakaye kuwa Malkia badala ya Vashiti.” Mfalme alupenda ushauri na akafanya kama alivoshauriwa,
Kisha yule ambaye atampendeza mfalme na awe malkia badala ya Vashti.” Shauri hili likampendeza mfalme, naye akalifuata.
5 Katika mji wa Shushani alikuwepo Myahudi aliyeitwa Modekai mwana wa Jaira mwana wa Shimei mwana wa Kishi, aliye kuwa wa kabila la Benjamini.
Basi katika mji wa ngome ya Shushani palikuwa na Myahudi wa kabila ya Benyamini, jina lake Mordekai mwana wa Yairi, mwana wa Shimei, mwana wa Kishi,
6 Yeye ni miongoni mwa Wayahudi waliochukuliwa pamoja na Yekonia, mfalme wa Yuda kutoka Yerusalemu na kupelekwa uhamishoni na mfalme Nebukadreza.
ambao walichukuliwa uhamishoni kutoka Yerusalemu na Mfalme Nebukadneza wa Babeli, wakiwa miongoni mwa waliochukuliwa mateka pamoja na Mfalme Yekonia wa Yuda.
7 Modekai alikuwa akimlea, Hadasa, yaani Esta, binti wa mjomba wake kwa sababu hakuwa na wazaai wake wote wawili. Modekai alimchukuwa kama binti yake. Esta alikuwa na umbo zuri na uso wa kupendeza.
Mordekai alikuwa na binamu yake msichana aliyeitwa Hadasa, ambaye alimlea kwa kuwa hakuwa na baba wala mama. Msichana huyu, ambaye pia alijulikana kwa jina la Esta, alikuwa na umbo na sura ya kupendeza, naye Mordekai alimtunza kama binti yake mwenyewe baada ya baba yake na mama yake kufariki.
8 Wasichana wengi waliletwa ikulu Shushani, baada ya tangazo na amri ya mfalme kutolewa. Waliwekwa chini ya usimamizi wa Hegai. Esta naye alikuwa ni miongoni mwa wasichana walioletwa na kuwekwa chini ya usimamizi wa Hegai, mwangalizi wa wanawake.
Wakati agizo na amri ya mfalme lilitangazwa, wanawali wengi waliletwa kwenye ngome ya mji wa Shushani na kuwekwa chini ya uangalizi wa Hegai. Pia Esta alipelekwa katika jumba la mfalme na akakabidhiwa Hegai, aliyekuwa mkuu wa nyumba ya wanawake.
9 Esta alimfurahisha, na akapata kibali mbele ya Hegai. Akampa vipodozi na sehemu ya chakula. Akampa wahudumu wa kike saba kutoka katika ikulu ya mfalme, na akampeleka na wahudumu wa kike katika sehemu bora katika nyumba ya wanawake.
Msichana huyu alimpendeza na kupata kibali mbele zake. Mara moja akaanza kumpa matunzo ya uzuri na chakula maalum. Alimpa Esta vijakazi saba waliochaguliwa kutoka jumba la kifalme, na kumhamishia yeye pamoja na vijakazi wake katika sehemu bora zaidi katika nyumba ya wanawake.
10 Esta hakuwa amemweleza mtu yeyote kuhusu jamaa zake kwa sababu Modekai alikuwa amemzuia.
Esta alikuwa hajadhihirisha uraia wala kabila lake, kwa sababu Mordekai alikuwa amemkataza.
11 kila siku Modekai alienda na kurudi mbele nje ya ua wa nyumba ya wanawake, ili kwamba asikie kuhusu mambo ya Esta na atakachofanyiwa.
Kila siku Mordekai alikuwa akitembeatembea karibu na ua wa nyumba ya wanawake kujua Esta alivyoendelea na kuona yaliyokuwa yakitendeka kwake.
12 Zamu ilipofika ya kila msichana kwenda kwa mfalme Ahusero kwa kufuata maelekezo kwa wanawake, kila msichana alitakiwa kumaliza miezi kumi na miwili ya urembo, miezi sita ya mafuta ya manemane na miezi sita ya vipodozi.
Kabla zamu ya msichana haijafika ya kwenda kwa Mfalme Ahasuero, ilimbidi atimize miezi kumi na miwili ya matunzo ya urembo kama ilivyokuwa imepangwa. Kwa miezi sita walikuwa wajipake mafuta ya manemane, na miezi sita kujipaka manukato na vipodozi.
13 wakati msichana alipoenda kwa mfalme, alipewa chochote alichotamani kutoka katika nyumba ya wanawake ili aende nacho katika nyuma ya mfalme.
Basi hivi ndivyo ambavyo msichana angeingia kwa mfalme: Kila kitu alichohitaji aliruhusiwa kuchukua kutoka nyumba ya wanawake na kwenda navyo katika jumba la mfalme.
14 Msichana alipaswa kwenda wakati wa usiku na kurudi katika nyumba ya wanawake, na kwa msimamizi Shaashigazi, msimamizi wa mfalme, ambaye alikuwa mwenye kuwalinda masulia. Msichana hakuruhusiwa kwenda tena kwa mfalme isipokuwa amemfurahiha mfalme na mfalme akaamuru arudi tena.
Jioni angekwenda pale na asubuhi kurudi sehemu nyingine ya nyumba ya wanawake katika utunzaji wa Shaashgazi, towashi wa mfalme ambaye alikuwa mkuu wa masuria. Hangeweza kurudi kwa mfalme mpaka apendezwe naye na kuagiza aitwe kwa jina lake.
15 Zamu ya Esta ilipotimia( mwana wa Abihaili, mjomba wa Modekai alikuw amemchukua kama kama binti yake) kwenda mbele ya mfalme, hakutaka kitu chochote isipokuwa vile ambavyo Hegai, msimamizi wa wanawake alimtaka avichukue.
Zamu ya Esta ilipofika kwenda kwa mfalme (msichana ambaye Mordekai alikuwa amemlea, binti wa Abihaili mjomba wake), Esta hakutaka vitu zaidi ya vile ambavyo Hegai, towashi wa mfalme aliyekuwa mkuu wa nyumba ya wanawake alivyokuwa amemshauri. Naye Esta alipata kibali kwa kila mtu aliyemwona.
16 Esta akapata kibali mbele ya kila aliyemwona. Esta akapelekwa kwa Mfalme Ahusiero katika makazi ya kifalme mwezi wa kumi, ambao ni mwezi wa Tabeti, katika mwaka wa saba wa utawala wake.
Esta alipelekwa kwa Mfalme Ahasuero katika makao ya mfalme mwezi wa kumi, yaani mwezi wa Tebethi, katika mwaka wake wa saba wa kutawala.
17 Mfalme alimpenda Esta zaidi kuliko wanawake wengine, na alipata kibali kuliko na wema mbele zake zaidi kuliko mabikira wengine na hivyo mfalme akamvika taji ya kimalkia badala ya Vashiti.
Basi ikawa mfalme alivutiwa na Esta kuliko wanawake wengine wote, naye akapata upendeleo na kibali kuliko mabikira wengine. Kisha akamvika taji la kifalme kichwani mwake na kumfanya malkia badala ya Vashti.
18 mfalme akawafanyia karamu kubwa wasimamizi na wahudumu wake wote, karamu ya Esta na akawapa unafuu wa kodi katika majimbo. Pia akawapa zawadi kwa ukarimu.
Mfalme akafanya karamu kubwa, karamu ya Esta, kwa wakuu wake wote na maafisa. Mfalme alitangaza mapumziko katika majimbo yake yote na kugawa zawadi kwa ukarimu wa kifalme.
19 Modekai alikuwa ameketi katika lango la mfalme wakati mabikira walipokuwa wamekusanyika kwa mara ya pili.
Wakati mabikira walikusanyika mara ya pili, Mordekai alikuwa ameketi katika lango la mfalme.
20 Esta alifuata ushauri Modekai ya kutomwambia mtu yeyote kuhusu jamaa zake. aliendelea kufuata ushauri wa Modekai kama alivyofanya alipokuwa mdogo.
Lakini Esta alikuwa ameficha siri ya kabila lake na uraia wake, kama Mordekai alivyokuwa amemwambia, kwa maana aliendelea kufuata maelekezo ya Mordekai kama alivyokuwa akifanya alipokuwa akimlea.
21 katika siku hizo ambazo Modekai alikuwa ameketi getini kwa mfalme, Bighani na Tereshi, wasimamizi wa mfalme walio linda lando, walikasirika na wakatafuta kumuua mfalme Ahusiero.
Wakati Mordekai alikuwa ameketi kwenye lango la mfalme, Bigthana na Tereshi, maafisa wawili wa mfalme waliokuwa walinzi wa lango, walikasirika na kupanga njama ya kumuua Mfalme Ahasuero.
22 Jambo lilipowekwa wazi kwa Modekai, alimtaarifu Malkia Esta na Esta akamweleza kile achoelezwa na Modekai.
Lakini Mordekai aligundua hila hii na kumwambia Malkia Esta, ambaye baadaye alimwarifu mfalme, huku akimsifu Mordekai.
23 Habari hii ilipepelelezwa na kuonekana kuwa kweli na wanaume wawili walinyongwa juu ya mti. Na habari hii ikaandikwa katika kitabu cha taarifa mbele ya mfalme.
Taarifa hiyo ilipochunguzwa na kuonekana kuwa kweli, maafisa hao wawili waliangikwa juu ya miti ya kunyongea. Haya yote yaliandikwa katika kitabu cha kumbukumbu mbele ya mfalme.