< Mhubiri 9 >
1 Kwa kuwa nilifikiri haya yote katika akili zangu kufahamu kuhusu watu wenye haki na wenye hekima na matendo yao. Wote wako katika mikono ya Mungu. Hakuna anayefahamu kama upendo au chuki itakuja kwa mtu.
我将这一切事放在心上,详细考究,就知道义人和智慧人,并他们的作为都在 神手中;或是爱,或是恨,都在他们的前面,人不能知道。
2 kila mmoja ana mwisho sawa. Mwisho sawa una subiria watu wenye haki na waovu, wema, walio safi na wasio safi, yeye atoaye dhabibu na yule asiye dhabihu. Kama vile watu wema watakufa wenye dhambi nao watakufa vivyo hivyo. kama vile yule anayeapa atakavyo kufa, vivyo hivyo mtu yule aogopaye kuweka kiapo naye atakufa.
凡临到众人的事都是一样:义人和恶人都遭遇一样的事;好人,洁净人和不洁净人,献祭的与不献祭的,也是一样。好人如何,罪人也如何;起誓的如何,怕起誓的也如何。
3 Kuna mwisho mwovu kwa kila kitu kinachofanyika chini ya jua, na mwisho kwa kila mtu. Moyo wa mwanadamu umejaa uovu, na wazimu uko katika mioyo yao wakati wanaishi. Hivyo baada ya hilo wanaenda kwa wafu.
在日光之下所行的一切事上有一件祸患,就是众人所遭遇的都是一样,并且世人的心充满了恶;活着的时候心里狂妄,后来就归死人那里去了。
4 Kwa kuwa yeyote anayeungana na wote walio hai kuna tumaini, kama vile mbwa aliye hai ni bora kuliko simba aliye kufa.
与一切活人相连的,那人还有指望,因为活着的狗比死了的狮子更强。
5 Kwa kuwa watu walio hai, lakini walio kufa hawajui chochote. Hawana tena tuzo yeyote kwa sababu kumbukumbu yao imesahaulika.
活着的人知道必死;死了的人毫无所知,也不再得赏赐;他们的名无人记念。
6 Upendo wao, chuki na wivu vimekatiliwa mbali muda mwingi. Hawatapata sehemu katika kitu chochote kinachofanyika chini ya jua.
他们的爱,他们的恨,他们的嫉妒,早都消灭了。在日光之下所行的一切事上,他们永不再有分了。
7 Nenda zako, kula mkate wako kwa furaha, na kunywa mvinyo wako na moyo wa furaha, kwa kuwa Mungu huruhusu kusherehekea kazi njema.
你只管去欢欢喜喜吃你的饭,心中快乐喝你的酒,因为 神已经悦纳你的作为。
8 Nguo zako ziwe nyeupe siku zote, na kichwa chako kipake mafuta.
你的衣服当时常洁白,你头上也不要缺少膏油。
9 Ishi kwa furaha na mwanamke umpendaye siku zako zote za maisha yako ya ubatili, siku ambazo Mungu amekupatia chini ya jua wakati wa siku zako za ubatili. Hiyo ni thawabu kwa ajili ya kazi yako chini ya jua.
在你一生虚空的年日,就是 神赐你在日光之下虚空的年日,当同你所爱的妻,快活度日,因为那是你生前在日光之下劳碌的事上所得的分。
10 Chochote mkono wako unakifanya, kifanye kwa nguvu zako kwa sababu hakuna kazi, au ufafanuzi au ujuzi au hekima katika Sheol, unapoenda. (Sheol )
凡你手所当做的事要尽力去做;因为在你所必去的阴间没有工作,没有谋算,没有知识,也没有智慧。 (Sheol )
11 Nimeona baadhi ya vitu vyakuvutia chini ya jua: Mashindano hayatokani na watu wenye mbio. Vita havitokani na watu imara. Mkate hautokani na watu wenye busara. Mali hazitokani na watu wenye ufahamu. Kibali hakitokani na watu wenye ujuzi. Badala yake muda na bahati huwaathiri wao wote.
我又转念:见日光之下,快跑的未必能赢;力战的未必得胜;智慧的未必得粮食;明哲的未必得资财;灵巧的未必得喜悦。所临到众人的是在乎当时的机会。
12 Kwa kuwa hakuna anaye fahamu wakati wake wa kufa, kama vile samaki wanaswavyo katika nyavu ya kifo, au kama vile ndege akamatwavyo katika mtego. Kama wanyama wanadamu wamefungwa katika nyakati mbaya ambazo ghafla huwaangukia.
原来人也不知道自己的定期。鱼被恶网圈住,鸟被网罗捉住,祸患忽然临到的时候,世人陷在其中也是如此。
13 Pia nimeona hekima chini ya jua kwa namna ambayo kwangu ilionekana kubwa.
我见日光之下有一样智慧,据我看乃是广大,
14 Kulikuwa na mji mdogo na watu wachache ndani yake, na mfalme mkuu akaja kinyume na mji huo na akauzingira na akajenga mahandaki kwa ajili ya kuushambulia.
就是有一小城,其中的人数稀少,有大君王来攻击,修筑营垒,将城围困。
15 Na katika mji kulikuwa na masikini, mtu mwenye hekima, ambaye kwa hekima yake aliuokoa mji. Ila baadaye aliye mkumbuka yule masikini.
城中有一个贫穷的智慧人,他用智慧救了那城,却没有人记念那穷人。
16 Hivyo, nikasema, “Hekima ni bora kuliko nguvu, lakini hekima ya mtu masikini hudharauliwa, na maneno yake hayasikilizwi.”
我就说,智慧胜过勇力;然而那贫穷人的智慧被人藐视,他的话也无人听从。
17 Maneno ya watu wenye hekima yaliongewa polepole yanasikiwa vizuri kuliko makelele ya mtawala yeyote miongoni mwa wapumbavu.
宁可在安静之中听智慧人的言语,不听掌管愚昧人的喊声。
18 Hekima ni bora kuliko silaha za vita, lakini mwenye dhambi mmoja anaweza kuharibu mazuri mengi.
智慧胜过打仗的兵器;但一个罪人能败坏许多善事。