< Mhubiri 8 >
1 Ni mtu gani mwenye hekima? Ambaye anafahamu matukio yana maana gani katika maisha? Hekima ndani ya mtu husababisha uso wake kung'ara, na ugumu wa uso wake hubadilika.
2 Ninakushauri kuitii amri ya mfalme kwa sababu ya kiapo cha Mungu cha kumlinda yeye.
3 Usiharakishe kuondoka mbele ya uwepo wake, na usisimame kuunga mkono jambo lisilofaa, kwa kuwa mfalme anafanya chochote anacho tamani.
4 Neno la mfalme hutawala, kwa hiyo ni nani atakaye mwambia, 'Unafanya nini?
5 Yeyote ashikaye amri za mfalme hukwepa madhara. Moyo wa mwenye hekima hutambua mwelekeo muafaka na muda wa kuenda.
6 Kwa kuwa kila jambo lina jibu sahihi, na wakati wa kujibu, kwa sababu taabu ya mtu ni kubwa.
7 Hakuna anaye fahamu kinacho fuata. Ni nani awezaye kumwambia nini kinacho kuja?
8 Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho; wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa; wala hakuna kuruhusiwa katika vita vile; wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.
9 Mambo hayo yote nimeyaona, nikatia moyo wangu katika kila kazi iliyofanyika chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasira yake.
10 Hivyo niliwaona wabaya wakizikwa hadharani. Waliondolewa mahali patakatifu na kuzikwa mahali waliposifiwa na watu katika mji walipokuwa wamefanya matendo maovu. Hii nayo haifai.
11 Wakati hukumu dhidi ya tendo ovu haihukumiwi haraka, hushawishi mioyo ya wanadamu kutenda ubaya.
12 Hata kama mwenye dhambi afanye uovu mara mia moja na bado aishi kwa muda mrefu, bado ninafahamu itakuwa vyema kwa wale wanao muheshimu Mungu, wanaouheshimu uwepo wake walio nao.
13 Lakini haitakuwa vyema kwa mtu mwovu; mkewe hatacheleweshwa. Siku zake kama kizuri kitowekacho upesi, kwa sababu hamuheshimu Mungu.
14 Kuna mvuke mwingine usio faa, jambo jingine linaofanyika juu ya dunia. Mambo hutokea kwa watu wenye haki kama yatokeavyo kwa watu waovu, na mambo hutokea kwa wenye haki kama yatokeavyo kwa waovu. Ninasema hili pia ni mvuke usiofaa.
15 Kwa hiyo nikapendekeza furaha, kwa sababu mtu hana jambo bora chini ya jua zaidi ya kula na kunywa na kuwa na furaha. furaha ndiyo itamfuata katika kazi zake kwa siku zote za maisha yake ambayo Mungu amempa chini ya jua.
16 Nikauweka moyo wangu kufamu hekima na kufahamu kazi inayofanyika juu ya nchi, kazi ambayo inafanyika mara nyingi pasipo kufumba macho usiku au mchana.
17 Kisha nika tafakari matendo yote ya Mungu, na kwamba mtu hawezi kuelewa kazi inayofanyika chini ya jua. Bila kujali mtu anafanya kupata majibu, hatayapata. Ingawa mwenye hekima anaweza kuamini anajua, kitu kweli hajui.