< Mhubiri 6 >

1 Kuna ubaya ambao nimeuona chini ya jua, na ni mbaya kwa watu.
我看見在太陽下,另有一種不幸,重壓在人身上:
2 Mungu anaweza kumpa mtu mali na utajiri na heshima kwa kiasi kwamba hakosi chochote anachokitamani mwenyewe, lakini kisha hampi uwezo wa kukifurahia. Badala yake mtu mwingine hutumia vitu vyake. Huu ni mvuke, teso baya.
有一人,天主賜他富裕、錢財、光榮;凡他心中所願意的,一件也不缺;但天主沒有讓他享用這一切,卻讓外人享用了:這也是空虛,是一件很悲慘的事。
3 Kama mtu akizaa watoto mia moja na kuishi miaka mingi, ili kwamba siku za miaka yake ni nyingi, lakini kama moyo wake hautosheki kwa mema na hazikwi kwa heshima, kisha ninasema kwamba, mtoto aliyezaliwa akiwa amekufa ni bora kuliko alivyo.
有一人生有百子,活了很大歲數,他年紀雖高,卻沒有隨心享受福樂,且未得安葬,照我看來,他還不如流產的胎兒。
4 Hata mtoto huyo amezaliwa bila faida na anapita katika giza, na jina lake linabaki limefichika.
流產的胎兒徒然而來,悄然而去,他的名字也湮沒無聞;
5 Ingawa mtoto huyu haoni jua au kujua kitu chochote, ana pumziko ingawa mtu huyo hakupumzika.
他沒有見過天日,也沒有任何知覺,但他總比那人更享安寧。
6 Hata kama mtu akiishi miaka elfu mbili lakini hajifunzi kufuraia vitu vizuri, aenda sehemu moja kama mtu yeyote yule.
那人即便活了兩千歲,如未享受福樂,他們二人豈不是同歸一處﹖
7 Ingawa kazi yote ya mtu ni kujaza mdomo wake, ila hamu yake haishibi.
人的一切勞碌都是為了口腹,但他的慾望卻總不知滿足。
8 Hakika ni faida gani aliyo nayo mwenye hekima kuliko mpumbavu? Ni faida gani aliyo nayo masikini hata kama anajua jinsi ya kutenda mbele ya watu?
智者較愚者究有什麼利益﹖知道如何與人往來的窮人,能得什麼好處﹖
9 Ni bora kuridhika na kile ambacho macho hukiona kuliko kutamani kile ambacho hamu isiyo tulia inatamani, ambayo pia ni mvuke na kujaribu kuuchunga upepo.
眼看見過的總勝過心所想望的:這也是空虛,也是追風。
10 Chochote ambacho kimekuwepo, tayari kimekwisha kupewa jina lake, na vile mtu alivyo ni kama tayari amekwisha fahamika. Hivyo imekuwa haifai kugombana na yule ambaye ni muhukumu mkuu wa wote.
已往所有的,都已有名可稱;人為何物,都已知道;人決不能與強於自己的抗辯。
11 Maneno mengi ambayo yanaongelewa, ndivyo yasiyo na maana yanaongezeka, kwa hiyo ni faida gani iliyopo kwa mwanadamu?
說話多,必多空談:這對人能有什麼益處﹖
12 Kwa kuwa ni nani ajuaye nini kilicho kizuri kwa mtu katika maisha yake wakati wa ubatili wake, siku zilizo hesabika ambazo kwa hizo anapita kama kivuri? Ni nina anayeweza kumwambia mtu kile kitakacho kuja chini ya jua baada ya kupita?
在空虛,消逝如影的人生少數歲月內,有誰知道什麼事對人有益﹖又有誰能指給人指示,他身後在太陽下要發生什麼事﹖

< Mhubiri 6 >