< Mhubiri 5 >
1 Linda mwenendo wako unapoenda kwenye nyumba ya Mungu. Nenda kule usikilize. Kusikiliza ni bora kuliko wapumbavu wanapotoa dhabihu wakati hawajuikuwa wanachofanya katika maisha ni kibaya.
2 Usiwe mwepesi wa kuongea kwa mdomo wako, na usiufanye moyo wako kuleta jambo lolote kwa haraka mbele za Mungu. Mungu yuko mbinguni, lakini uko chini, kwa hiyo maneno yako yawe machache.
3 Kama una mambo mengi ya kufanya na kuhangaika, pengine utapata ndoto mbaya. Na pengine utaongea maneno mengi ya upumbavu.
4 Ukiweka nadhili kwa Mungu, usichelewe kuifanya, kwa kuwa Mungu hafurahii upumbavu. Fanya kile ulichoapa utakifanya.
5 Ni bora kutokuweka nadhiri kuliko kuweka nadhiri ambayo usiyoiondoa.
6 Usiuruhusu mdomo wako kusababisha mwili wako kutenda dhambi. Usiseme kwa mtumwa wa kuhani, “Kile kiapo kilikuwa kwa makosa.” Kwani nini kumfanya Mungu akasirike kwa kuapa kwa uongo, kumchochea Mungu aharibu kazi ya mikono yako?
7 Kwa kuwa katika ndoto nyingi, kama ilivyo katika maneno mengi, kuna mvuke ubatili. Hivyo mwogope Mungu.
8 Unapomwona masikini akiteswa na kunyang'anywa haki na kutendewa vibaya katika jimbo lako, usishangae kama kwamba hakuna anaye fahamu, kwa sababu kuna watu katika mamlaka ambao hutazama, kuna hata walio juu yao.
9 Kwa nyongeza uzalishaji wa ardhi ni kwa kila mmoja, na mfalme mwenyewe huchukua uzalishaji kutoka mashambani.
10 Yeyote apendaye fedha hatatosheka na fedha, na yeyote apendaye utajiri mara zote hutaka zaidi. Huu pia ni mvuke.
11 Kadri mafanikio yanapoongezeka, ndivyo wanavyoongezeka watu wanaotumia. Kuna faida gani katika utajiri kwa mmiliki isipokuwa kuutazama kwa macho yake?
12 Usingizi wa mfanyakazi ni mtamu, kama anakula kidogo au sana, lakini utajiri wa mtu tajiri haumuruhusu yeye kulala vizuri.
13 Kuna jambo baya zaidi ambalo nimeliona chini ya jua: mali iliyowekwa akiba na mwenye nayo, inamsababishia taabu mwenyewe.
14 Wakati tajiri anapopoteza utajiri wake kwa bahati mbaya, mwana wake, ambaye amemzaa, habakiziwi chochote mikononi mwake.
15 Kama mtu azaliwavyo uchi kutoka tumboni mwa mamaye, vivyo hivyo ataondoka katika maisha haya akiwa uchi. Hachukui chochote kutoka katika kazi yake.
16 Jambo jingine baya kabisa, kama mtu alivyo kuja ni lazima aende vivyo hivyo. Hivyo ni faida gani mtu yeyote aipatayo katika kufanya kwa ajili ya upepo?
17 Wakati wa siku zake anakula gizani na anafedheheshwa sana na magonjwa na hasira.
18 Tazama, kile nilichokiona kuwa kizuri kufaaa ni kula na knywa na kufurahia faida kutoka katika kazi zetu zote, tuzifanyazo chini ya jua wakati wa siku za maisha haya ambayo Mungu ametupa. Kwa kuwa huu ni wajibu wa mtu.
19 Yeyote ambaye Mungu amempa mali na utajiri na uwezo wa kupokea sehemu yake na kufurahi katika kazi yake hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.
20 Kwa kuwa mara kadhaa hakumbuki siku za maisha yake, kwa sababu Mungu anamfanya kuhangaika na mambo ambayo anafurahia kuyafanya.