< Mhubiri 3 >

1 Kwa kuwa kila kitu na wakati wake, na majira kwa kila kusudi chini ya mbingu.
omnia tempus habent et suis spatiis transeunt universa sub caelo
2 Kuna wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa, wakati wa kupanda na wakati wa kung'oa yaliyopandwa,
tempus nascendi et tempus moriendi tempus plantandi et tempus evellendi quod plantatum est
3 wakati wa kuua na wakati wa kuponya, wakati wa kubomo na wakati wa kujenga.
tempus occidendi et tempus sanandi tempus destruendi et tempus aedificandi
4 Kuna wakati wa kulia na wakati wa kucheka, wakati wa kuomboleza na wakati kucheza,
tempus flendi et tempus ridendi tempus plangendi et tempus saltandi
5 wakati wa kutupa mawe na wakati wa kukusanya mawe, wakati wa kukumbatia watu wengine wakati wa kutokumbatia.
tempus spargendi lapides et tempus colligendi tempus amplexandi et tempus longe fieri a conplexibus
6 Kuna wakati wa kutafuta vitu na wakati wa kutotafuta, wakati wa kutunza vitu na wakati wa kuvitupa,
tempus adquirendi et tempus perdendi tempus custodiendi et tempus abiciendi
7 wakati kuchana mavazi na wakati wa kuyashona, wakati wa kunyamaza na wakati wa kuzungumza.
tempus scindendi et tempus consuendi tempus tacendi et tempus loquendi
8 Kuna wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia, wakati wa vita na wakati wa amani.
tempus dilectionis et tempus odii tempus belli et tempus pacis
9 Ni faida gani mfanyakazi aipatayo katika kazi yake?
quid habet amplius homo de labore suo
10 Nimeona kazi ambayo Mungu amewapa wanadamu kuitimiza.
vidi adflictionem quam dedit Deus filiis hominum ut distendantur in ea
11 Mungu amefanya kila kitu kufaa kwa wakati wake. Pia ameweka umilele ndani ya mioyo yao. Lakini mwanadamu hawezi kuelewa matendo ambayo Mungu ameyafanya, tangu mwanzo wao hadi mwisho.
cuncta fecit bona in tempore suo et mundum tradidit disputationi eorum ut non inveniat homo opus quod operatus est Deus ab initio usque ad finem
12 Ninajua kuwa hakuna kilicho bora kwa mtu yeyote kuliko kufurahi na kutenda mema maadamu anaishi-
et cognovi quod non esset melius nisi laetari et facere bene in vita sua
13 na kwamba kila mmoja anapaswa ale na kunywa na anapaswa kuelewa jinsi ya kufurahia mazuri ambayo yanatoka katika kazi zake zote. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.
omnis enim homo qui comedit et bibit et videt bonum de labore suo hoc donum Dei est
14 Ninajua kwamba chochote afanyacho Mungu kinadumu milele. Hakuna kinaweza kuongezwa au kuondolea, kwa sababu Mungu ndiye aliyekifanya, ili kwamba watu wamsogelee kwa heshima.
didici quod omnia opera quae fecit Deus perseverent in perpetuum non possumus eis quicquam addere nec auferre quae fecit Deus ut timeatur
15 Chochote kilichopo kimekwisha kuwepo; chochote kitakachokuwepo kimekwisha kuwepo. Mungu huwafanya wanadamu kutafuka vitu vilivyjificha.
quod factum est ipsum permanet quae futura sunt iam fuerunt et Deus instaurat quod abiit
16 Na nimeona kwamba chini ya jua ubaya upo mahali palipopaswa kuwa na haki, na sehemu ya haki mara nyingi ina ubaya.
vidi sub sole in loco iudicii impietatem et in loco iustitiae iniquitatem
17 Nikasema moyoni mwangu, “Mungu atahukumu mwenye haki na mbaya kwa wakati muafaka kwa kila jambo na kila tendo.
et dixi in corde meo iustum et impium iudicabit Deus et tempus omni rei tunc erit
18 Nikasema moyoni mwangu, “Mungu huwajaribu wanadamu kuwaonyesha kwamba wao ni kama wanyama.”
dixi in corde meo de filiis hominum ut probaret eos Deus et ostenderet similes esse bestiis
19 Kwa kuwa mwisho watoto wa wanadamu na mwisho wa wanyama ni sawa. Kifo cha mmoja ni sawa na kifo cha mwingine. Wote wana pumzi sawa. Hakuna faida kwa mwanadamu zaidi ya wanyama. Kwa kuwa hakuna kila kitu isipokuwa pumzi?
idcirco unus interitus est hominis et iumentorum et aequa utriusque condicio sicut moritur homo sic et illa moriuntur similiter spirant omnia et nihil habet homo iumento amplius cuncta subiacent vanitati
20 Kila kitu kinaenda sehemu moja. Kila kitu kinatoka mavumbini, na kila kitu kinarudi katika mavumbini.
et omnia pergunt ad unum locum de terra facta sunt et in terram pariter revertentur
21 Ni nani ajuaye kama roho ya mwanadamu inaenda juu na roho ya wanyama inaenda chini ya nchi?
quis novit si spiritus filiorum Adam ascendat sursum et si spiritus iumentorum descendat deorsum
22 kwa hiyo tena nikatambua kwamba hakuna lililo jema kwa yeyote zaidi ya kufurahia kazi yake, kwa kuwa hilo ndilo jukumu lake. Ni nani awezaye kumleta tena kuona kinachotokea baada yake?
et deprehendi nihil esse melius quam laetari hominem in opere suo et hanc esse partem illius quis enim eum adducet ut post se futura cognoscat

< Mhubiri 3 >