< Mhubiri 12 >

1 Pia mkumbuke Muumba wako katika siku za za ujana, kabla ya siku za ugumu hazijaja, na kabla ya miaka haijafika utakapo sema, “Mimi sina furaha katika hizo,”
Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku za taabu, wala haijakaribia miaka utakaposema, “Mimi sifurahii hiyo”:
2 fanya hivi kabla ya nuru ya jua na mwezi na nyota havijawa giza, na mawingu kurudi baada ya mvua.
kabla jua na nuru, nao mwezi na nyota havijatiwa giza, kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;
3 Huo utakuwa wakati ambapo mlinzi wa ikulu atatetemeka, na wanaume imara wameinama, na wanawake wanao saga kukoma, kwa sababu ni wachache, na wale wanao chungulia dirishani hawaoni vizuri tena.
siku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka, nao watu wenye nguvu watakapojiinamisha, wakati wasagao watakapokoma kwa sababu ya uchache, nao wachunguliao madirishani kutiwa giza;
4 Huo utakuwa wakati ambao milango imefungwa katika mtaa, na mlio wa kusanga kukoma, wakati wanaume watasitushwa kwa mlio wa ndege, na wimbo wa sauti ya wasichana kukoma.
wakati milango ya kuingia barabarani itakapofungwa na sauti ya kusaga kufifia; wakati watu wataamshwa kwa sauti ya ndege, lakini nyimbo zao zote zikififia;
5 Utakuwa wakati ambapo watu wataogopa vilivyoinuka na hatari iliyoko barabarani, na wakati ambapo mlozi utachanua maua, na wakati panzi watakapokokotana wenyewe, na wakati ambapo hamu za asili zitakaposhindwa. Kisha mtu aenda katika nyumba yake ya milele na waombolezaji watelemka mitaani.
wakati watu watakapoogopa kilichoinuka juu na hatari zitakazokuwepo barabarani; wakati mlozi utakapochanua maua na panzi kujikokota nawe usiwe na shauku ya kitu chochote. Ndipo mwanadamu aiendea nyumba yake ya milele nao waombolezaji wakizunguka barabarani.
6 Mkumbuke Muumba wako kabla ya kamba ya fedha kukatwa, au bakuli ya dhahabu kupasuka, au gudulia kuvunjwa kwenye chemuchemi, au torori la maji kuvunjika kisimani,
Mkumbuke Muumba wako: kabla haijakatika kamba ya fedha, au bakuli la dhahabu halijavunjika; kabla mtungi kuvunjika kwenye chemchemi, au gurudumu kuvunjika kisimani,
7 kabla mavumbi kurudia mahali yalipotoka, na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.
nayo mavumbi kurudi ardhini yalikotoka, na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.
8 Kama ukungu wa mvuke,” asema mwalimu, kila kitu ni mvuke upoteao.
Mhubiri asema, “Ubatili! Ubatili! Kila kitu ni ubatili!”
9 Mwalimu alikuwa na hekima na aliwafundisha watu maarifa. Alisoma na kuazimu na kutunga mithali nyingi katika mpangilio.
Mhubiri hakuwa tu na hekima, bali aliwagawia watu maarifa pia. Alitafakari na kutafiti na akaweka katika utaratibu mithali nyingi.
10 Mwalimu alitafuta kuandika kwa kutumia vithibitisho dhahiri, maneno ya kweli yaliyo wima.
Mhubiri alitafiti ili kupata maneno sahihi na kila alichoandika kilikuwa sawa na kweli.
11 Maneno ya watu wenye hekima ni kama mchokoo. Kama misumari ilivyogongomewa kwa undani, ndivyo yalivyo maneno ya mabwana katika mkusanyiko wa mithali zao, ambayo yamefundishwa na mchungaji mmoja.
Maneno ya wenye hekima ni kama mchokoro, mithali zao zilizokusanywa pamoja ni kama misumari iliyogongomewa ikawa imara, yaliyotolewa na Mchungaji mmoja.
12 Mwanangu kuwa makini na kitu zaidi, utengezaji wa vitabu vingi, ambacho hakina mwisho, na kusoma kwingi huleta uchovu mwilini.
Tena zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo, hakuna mwisho wa kutunga vitabu vingi, nako kusoma sana huuchosha mwili.
13 Mwisho wa jambo baada ya kila kitu umesikika, ni kwamba ni lazima umche Mungu na kushika amri zake, kwa kuwa huu ndilo jukumu lote la mwanadamu.
Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa: Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
14 Kwa kuwa Mungu ataleta kila tendo hukumuni, pamoja na kila kitu kilichofichika, kizuri au kibaya.
Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au baya.

< Mhubiri 12 >