< Mhubiri 12 >
1 Pia mkumbuke Muumba wako katika siku za za ujana, kabla ya siku za ugumu hazijaja, na kabla ya miaka haijafika utakapo sema, “Mimi sina furaha katika hizo,”
Remember your Creator in the days of your youth, before the days of adversity come and the years approach of which you will say, “I find no pleasure in them,”
2 fanya hivi kabla ya nuru ya jua na mwezi na nyota havijawa giza, na mawingu kurudi baada ya mvua.
before the light of the sun, moon, and stars is darkened, and the clouds return after the rain,
3 Huo utakuwa wakati ambapo mlinzi wa ikulu atatetemeka, na wanaume imara wameinama, na wanawake wanao saga kukoma, kwa sababu ni wachache, na wale wanao chungulia dirishani hawaoni vizuri tena.
on the day the keepers of the house tremble and the strong men stoop, when those grinding cease because they are few and those watching through windows see dimly,
4 Huo utakuwa wakati ambao milango imefungwa katika mtaa, na mlio wa kusanga kukoma, wakati wanaume watasitushwa kwa mlio wa ndege, na wimbo wa sauti ya wasichana kukoma.
when the doors to the street are shut and the sound of the mill fades away, when one rises at the sound of a bird and all the daughters of song grow faint,
5 Utakuwa wakati ambapo watu wataogopa vilivyoinuka na hatari iliyoko barabarani, na wakati ambapo mlozi utachanua maua, na wakati panzi watakapokokotana wenyewe, na wakati ambapo hamu za asili zitakaposhindwa. Kisha mtu aenda katika nyumba yake ya milele na waombolezaji watelemka mitaani.
when men fear the heights and dangers of the road, when the almond tree blossoms, the grasshopper loses its spring, and the caper berry shrivels— for then man goes to his eternal home and mourners walk the streets.
6 Mkumbuke Muumba wako kabla ya kamba ya fedha kukatwa, au bakuli ya dhahabu kupasuka, au gudulia kuvunjwa kwenye chemuchemi, au torori la maji kuvunjika kisimani,
Remember Him before the silver cord is snapped and the golden bowl is crushed, before the pitcher is shattered at the spring and the wheel is broken at the well,
7 kabla mavumbi kurudia mahali yalipotoka, na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.
before the dust returns to the ground from which it came and the spirit returns to God who gave it.
8 Kama ukungu wa mvuke,” asema mwalimu, kila kitu ni mvuke upoteao.
“Futility of futilities,” says the Teacher. “Everything is futile!”
9 Mwalimu alikuwa na hekima na aliwafundisha watu maarifa. Alisoma na kuazimu na kutunga mithali nyingi katika mpangilio.
Not only was the Teacher wise, but he also taught the people knowledge; he pondered, searched out, and arranged many proverbs.
10 Mwalimu alitafuta kuandika kwa kutumia vithibitisho dhahiri, maneno ya kweli yaliyo wima.
The Teacher searched to find delightful sayings and to record accurate words of truth.
11 Maneno ya watu wenye hekima ni kama mchokoo. Kama misumari ilivyogongomewa kwa undani, ndivyo yalivyo maneno ya mabwana katika mkusanyiko wa mithali zao, ambayo yamefundishwa na mchungaji mmoja.
The words of the wise are like goads, and the anthologies of the masters are like firmly embedded nails driven by a single Shepherd.
12 Mwanangu kuwa makini na kitu zaidi, utengezaji wa vitabu vingi, ambacho hakina mwisho, na kusoma kwingi huleta uchovu mwilini.
And by these, my son, be further warned: There is no end to the making of many books, and much study wearies the body.
13 Mwisho wa jambo baada ya kila kitu umesikika, ni kwamba ni lazima umche Mungu na kushika amri zake, kwa kuwa huu ndilo jukumu lote la mwanadamu.
When all has been heard, the conclusion of the matter is this: Fear God and keep His commandments, because this is the whole duty of man.
14 Kwa kuwa Mungu ataleta kila tendo hukumuni, pamoja na kila kitu kilichofichika, kizuri au kibaya.
For God will bring every deed into judgment, along with every hidden thing, whether good or evil.