< Mhubiri 11 >

1 Peleka mkate wako juu ya maji, kwa kuwa utaupata tena baada ya siku nyingi.
Mitte panem tuum super transeuntes aquas: quia post tempora multa invenies illum.
2 Shiriki mkate na watu saba, hata wanane kwa kuwa haujui ni majanga gani yanayo kuja juu ya nchi.
Da partem septem, necnon et octo: quia ignoras quid futurum sit mali super terram.
3 Kama mawingu yamejaa mvua, yanajivua yenyewe chini ya nchi. Na kama mti ukianguka kuelekea kusini au kuelekea kaskazini, popote mti unapoangukia papo hapo utabakia.
Si repletæ fuerint nubes, imbrem super terram effundent. Si ceciderit lignum ad Austrum, aut ad Aquilonem, in quocumque loco ceciderit, ibi erit.
4 Yeyote autazamaye upepo yawezekana asipande, na yeyote atazamaye mawingu yawezekana asivune.
Qui observat ventum, non seminat: et qui considerat nubes, numquam metet.
5 Kama usivyo jua njia ya upepo, wala vile ambavyo mtoto akuavyo tumboni, vivyo hivyo huwezi kuielewa kazi ya Mungu, aliye umba kila kitu.
Quomodo ignoras quæ sit via spiritus, et qua ratione compingantur ossa in ventre prægnantis; sic nescis opera Dei, qui fabricator est omnium.
6 Asubuhi panda mbegu yako; hadi jioni, fanya kazi kwa mikono yako kama inavyo hitajika kwa kuwa haujui ni ipi itafanikiwa, jioni au asubuhi, au hii au ile au zote zitakuwa nzuri.
Mane semina semen tuum, et vespere ne cesset manus tua: quia nescis quid magis oriatur, hoc aut illud: et si utrumque simul, melius erit.
7 Kweli nuru ni tamu, na ni kitu cha kufurahisha kwa ajili ya macho kuona jua.
Dulce lumen, et delectabile est oculis videre solem.
8 Kama mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote, lakina na afikiri juu ya siku zijazo za giza, kwa kuwa zitakuwa nyingi. Kila kitu kijacho ni mvuke unaoteketea.
Si annis multis vixerit homo, et in his omnibus lætatus fuerit, meminisse debet tenebrosi temporis, et dierum multorum: qui cum venerint, vanitatis arguentur præterita.
9 Furahia kijana, katika ujana wako, na moyo wako ufurahie siku za ujana wako. fuatilia yale mema ya moyo wako, chochote kilicho mbele ya macho yako. Ingawa, fahamu kwamba MUngu atakuleta hukumuni kwa ajili ya vitu hivi vyote.
Lætare ergo iuvenis in adolescentia tua, et in bono sit cor tuum in diebus iuventutis tuæ, et ambula in viis cordis tui, et in intuitu oculorum tuorum: et scito quod pro omnibus his adducet te Deus in iudicium.
10 Ondoa hasira kutoka moyoni mwako, na usijali maumivu yoyote katika mwili wako, kwa sababu ujana na nguvu zake ni mvuke.
Aufer iram a corde tuo, et amove malitiam a carne tua. Adolescentia enim et voluptas vana sunt.

< Mhubiri 11 >