< Torati 7 >

1 Wakati Yahwe Mungu wenu atuleta katika nchi ambayo mnaenda kuimiliki na kuwaondoa mataifa mengi mbele zenu- Mhiti, Mgirgashi na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, Mhivi, Myebusi- mataifa saba makubwa na yenye nguvu kuliko wewe.
“耶和华—你 神领你进入要得为业之地,从你面前赶出许多国民,就是赫人、革迦撒人、亚摩利人、迦南人、比利洗人、希未人、耶布斯人,共七国的民,都比你强大。
2 Na wakati Yahwe Mungu wenu awapa ninyi ushindi juu yao pindi mnakutana nao katika vita, mtawashambulia, basi mnapaswa kuwateketeza kabisa. Hamtafanya agano nao, wala kuonesha huruma kwao.
耶和华—你 神将他们交给你击杀,那时你要把他们灭绝净尽,不可与他们立约,也不可怜恤他们。
3 Wala hamtapanga ndoa zozote pamoja nao, hamtawatoa binti zenu kwa vijana wao, na hamtawachukua binti zao kwa vijana wenu.
不可与他们结亲。不可将你的女儿嫁他们的儿子,也不可叫你的儿子娶他们的女儿;
4 Kwa kuwa watawabadilisha vijana wenu kutonifuata mimi, ili kwamba waweze kuabudu miungu yao. Kwa hiyo hasira ya Yahwe itawashwa dhidi yenu na atawaangamiza haraka.
因为他必使你儿子转离不跟从主,去事奉别神,以致耶和华的怒气向你们发作,就速速地将你们灭绝。
5 Hivi ndivyo mtakavyo washughulikia nao; mtavunja madhabahu zao, vunja nguzo zao za mawe katika vipande, kata chini ncha za Asherahi, na kuzichoma sanamu za kutupwa.
你们却要这样待他们:拆毁他们的祭坛,打碎他们的柱像,砍下他们的木偶,用火焚烧他们雕刻的偶像。
6 Kwa kuwa wewe ni taifa uliyetengwa kwa Yahwe Mungu wako. Amekuchagua wewe kuwa watu kwa ajili yake kumiliki, zaidi ya watu wengine wote ambao wako katika uso wa dunia.
因为你归耶和华—你 神为圣洁的民;耶和华—你 神从地上的万民中拣选你,特作自己的子民。
7 Yahwe hakuweka upendo wake juu yenu au kuwachagua kwa sababu mlikuwa zaidi katika idadi kuliko watu wowote, kwa kuwa mlikuwa wachache kuliko watu wote-
“耶和华专爱你们,拣选你们,并非因你们的人数多于别民,原来你们的人数在万民中是最少的。
8 Lakini kwa sababu anawapenda ninyi, anataka kushika kiapo alichoapa kwa baba zenu. Huyu ni Yahwe aliyewatoa kwa mkono wa uweza na kuwakomboa kutoka nyumba ya utumwa, kutoka mkono wa Farao, mfalme wa Misri.
只因耶和华爱你们,又因要守他向你们列祖所起的誓,就用大能的手领你们出来,从为奴之家救赎你们脱离埃及王法老的手。
9 Kwa hiyo tambua ya kuwa Yahwe Mungu wako-ni Mungu, Mungu mwaminifu, anayetunza maagano na uaminifu kwa vizazi elfu kwa wale wanaompenda na kuyashika maagizo yake,
所以,你要知道耶和华—你的 神,他是 神,是信实的 神;向爱他、守他诫命的人守约,施慈爱,直到千代;
10 lakini huwalipa wale wanaomchukia kwa sura zao, kuwaangamiza, hatakuwa na huruma kwa yeyote anayemchukia; atamlipa kwa uso wake.
向恨他的人当面报应他们,将他们灭绝。凡恨他的人必报应他们,决不迟延。
11 Kwa hiyo utashika maagizo, amri, na sheria ninazokuamuru leo, ili kwamba uzifanye.
所以,你要谨守遵行我今日所吩咐你的诫命、律例、典章。”
12 Kama mtasikiliza maagizo haya, kuyashika na kuyafanya, itakuwa Yahwe Mungu wenu atawashika pamoja na agano na uaminifu ambao aliapa kwa baba zenu.
“你们果然听从这些典章,谨守遵行,耶和华—你 神就必照他向你列祖所起的誓守约,施慈爱。
13 Atawapenda, atawabariki, na kuwazidisha, pia atabariki tunda la miili yenu na tunda la ardhi yenu, nafaka zenu, divai mpya, mafuta yenu, atazidisha mifugo na kundi lako la mifugo michanga, katika nchi ambayo aliapa kwa baba zenu kuwapa.
他必爱你,赐福与你,使你人数增多,也必在他向你列祖起誓应许给你的地上赐福与你身所生的,地所产的,并你的五谷、新酒,和油,以及牛犊、羊羔。
14 Mtabarikiwa zaidi kuliko watu wengine wote; hapatakuwa na mwanaume asiyekuwa na mtoto au mwanamke tasa miongoni mwenu au miongoni mwa mifugo.
你必蒙福胜过万民;你们的男女没有不能生养的,牲畜也没有不能生育的。
15 Yahwe atawaondolea magonjwa yote; hakuna magonjwa mabaya ya Misri ambayo mnayajua yatawekwa juu yenu, Lakini atayaweka kwa wote wanaowachukia ninyi.
耶和华必使一切的病症离开你;你所知道埃及各样的恶疾,他不加在你身上,只加在一切恨你的人身上。
16 Mtayaondoa makundi ya watu wote ambayo Yahwe Mungu wenu awapa ushindi, na jicho lenu halitawaonea huruma. Na hamtaabudu miungu yao, kwa kuwa huo utakuwa mtego kwenu.
耶和华—你 神所要交给你的一切人民,你要将他们除灭;你眼不可顾惜他们。你也不可事奉他们的神,因这必成为你的网罗。
17 Kama mtasema kwenye mioyo, Haya mataifa ni mengi zaidi kuliko mimi; nitawezaje kuwafukuza?
“你若心里说,这些国的民比我更多,我怎能赶出他们呢?
18 Usiwaogope; utakumbuka akilini Yahwe nini Mungu wenu alifanya kwa Farao na Misri yote?
你不要惧怕他们,要牢牢记念耶和华—你 神向法老和埃及全地所行的事,
19 Mateso makuu ambayo macho yenu yaliona, ishara, maajabu, mkono wa uweza, mkono ulionyoshwa ambao Yahwe Mungu wenu alivyowatoa. Yahwe Mungu wenu atafanya kile kile kwa watu wote ambao mnawaogopa.
就是你亲眼所看见的大试验、神迹、奇事,和大能的手,并伸出来的膀臂,都是耶和华—你 神领你出来所用的。耶和华—你 神必照样待你所惧怕的一切人民。
20 Zaidi ya yote, Yahwe Mungu wenu atatuma nyigu miongoni mwao, mpaka wale waliobaki na wale wanaojificha wenyewe mbele yenu waangamizwa mbele ya uwepo wenu.
并且耶和华—你 神必打发黄蜂飞到他们中间,直到那剩下而藏躲的人从你面前灭亡。
21 Hamtatishikeni nao, kwa kuwa Yahwe Mungu wenu yuko miongoni mwenu, Mungu mkuu na wa kuogofya.
你不要因他们惊恐,因为耶和华—你 神在你们中间是大而可畏的 神。
22 Yahwe Mungu wenu atayaondoa mataifa mbele zenu kidogo kidogo. Hamtayashinda yote kwa wakati mmoja, au wanyama wa mwitu watakuwa wengi karibu yenu.
耶和华—你 神必将这些国的民从你面前渐渐赶出;你不可把他们速速灭尽,恐怕野地的兽多起来害你。
23 Lakini Yahwe Mungu wenu atawapa ninyi ushindi dhidi yao wakati mkutanapo vitani; atawachanganya kwa kiasi kikubwa mpaka wameangamizwa.
耶和华—你 神必将他们交给你,大大地扰乱他们,直到他们灭绝了;
24 Atawaweka wafalme wao chini ya utawala wenu, na mtafanya jina lao kuangamia toka chini ya mbingu. Hakuna atakayeweza kusimama mbele yenu, mpaka muwaangamize.
又要将他们的君王交在你手中,你就使他们的名从天下消灭。必无一人能在你面前站立得住,直到你将他们灭绝了。
25 Utazichoma sanamu za kuchonga za miungu yao- usitamani madini ya fedha au dhahabu yanayofunika na kuichukua kwa ajili yenu, kwa sababu mkifanya, mtanaswa nayo-kwa kuwa ni chukizo kwa Yahwe Mungu wenu.
他们雕刻的神像,你们要用火焚烧;其上的金银,你不可贪图,也不可收取,免得你因此陷入网罗;这原是耶和华—你 神所憎恶的。
26 Hamtaleta chukizo lolote ndani ya nyumba zenu na kuanza kuiabudu. Mtachukizwa kabisa na kuchukia kwa kuwa imetengwa kwa ajili ya uharibifu.
可憎的物,你不可带进家去;不然,你就成了当毁灭的,与那物一样。你要十分厌恶,十分憎嫌,因为这是当毁灭的物。”

< Torati 7 >