< Torati 30 >
1 Vitu hivi vitakavyokuja juu yako, baraka na laana nilizoziweka mbele yako, na utakapozirejea akilini miongoni mwa mataifa mengine ambapo Yahwe Mungu wako kawapeleka,
And it shall come to pass, when all these things are come upon thee, the blessing and the curse, which I have set before thee, and thou reflectest on them in thy heart among all the nations, whither the Lord thy God hath driven thee,
2 na utakapomrudia Yahwe Mungu wako na kutii sauti yake, na kufuata yote ambayo nayokuamuru leo – wewe na watoto wako – kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote,
So that thou returnest unto the Lord thy God, and hearkenest unto his voice according to all that I command this day, thou and thy children, with all thy heart, and with all thy soul:
3 kisha Yahwe Mungu wako atageuza kutekwa kwako na kukuhurumia; atawarudisha na kuwakusanya kutoka kwa watu wote ambapo Yahwe Mungu wako aliwatawanya.
That then the Lord thy God will restore thy captivity, and have mercy upon thee; and he will again gather thee from all the nations, whither the Lord thy God hath scattered thee.
4 Iwapo yeyote ya watu walio uhamishoni wapo katika sehemu za mbali sana chini ya mbingu, kutoka huko Yawhe Mungu wako atawakusanya, na kutoka huko atawarejesha.
If thy outcasts be at the outmost parts of heaven, from there will the Lord thy God gather thee, and from there will he fetch thee:
5 Yahwe Mungu wako atawaleta katika nchi ambayo mababu zenu walimiliki, nanyi mtaimiliki tena; atawatendea mema na kuwazidisha zaidi ya alivyofanya kwa mababu zenu.
And the Lord thy God will bring thee into the land which thy fathers possessed, and thou shalt possess it; and he will do thee good, and multiply thee above thy fathers.
6 Yahwe Mungu wako atatahiri moyo wako na moyo wa uzao wako, ili umpende Yahwe Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote, ili kwamba uweze kuishi.
And the Lord thy God will circumcise thy heart, and the heart of thy seed, to love the Lord thy God with all thy heart, and with all thy soul, in order that thou mayest live.
7 Yahwe Mungu wako ataweka laana hizi zote kwa maadui zako na kwa wote wakuchukiayo, wale waliokutesa.
And the Lord thy God will put all these denunciations upon thy enemies, and on those that hate thee, who have persecuted thee.
8 Utarudi na kutii sauti ya Yahwe, nawe utatenda amri zake zote ambazo ninakuamuru leo.
And thou wilt return and hearken unto the voice of the Lord, and thou wilt do all his commandments which I command thee this day.
9 Yahwe Mungu wako atakufanikisha katika kazi yote ya mkono wako, katika matunda ya mwili wako, katika matunda ya mifugo yako, na katika matunda ya nchi yako, kwa mafanikio; kwa maana Yahwe atafurahia tena mafanikio yako, kama alivyofurahia kwa baba zako.
And the Lord thy God will make thee pre-eminent in every work of thy hand, in the fruit of thy body, and in the fruit of thy cattle, and in the fruit of thy land, for good; for the Lord will again rejoice over thee for good, as he rejoiced over thy fathers;
10 Atafanya hivi iwapo utatii sauti ya Yahwe Mungu wako, ili kuzishika amri zake na kanuni zake zilizoandikwa katika kitabu hiki cha sheria, iwapo utamgeukia Yahwe Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote.
If thou wilt hearken unto the voice of the Lord thy God, to keep his commandments and his statutes which are written in this book of the law; if thou wilt return unto the Lord thy God with all thy heart, and with all thy soul.
11 Kwa maana amri hii nayokuamuru leo sio ngumu sana, wala haipo nje ya uwezo wako kufikia.
For this commandment which I command thee this day, is not hidden from thee, nor is it far off.
12 Haipo mbinguni, ili usije ukasema, “Nani atayekwenda kwa ajili yetu mbinguni na kutuletea kwetu na kutufanya tuisikie, ili tuweze kutekeleza?”
It is not in heaven; that thou shouldst say, Who will go up for us to heaven, and fetch it down unto us, and cause us to hear it, that we may do it?
13 Wala haipo ng’ambo ya bahari, ili usije ukasema, “Nani atakwenda ng’ambo ya pili ya bahari kwa ajili yetu na kutuletea kwetu na kutufanya tuisikie, ili tuweze kuifanya?”.
Neither is it beyond the sea; that thou shouldst say, Who will go over the sea for us, and fetch it unto us, and cause us to hear it, that we may do it!
14 Lakini neno lipo karibu sana kwako, katika kinywa chako na moyo wako, ili uweze kutekeleza.
But the word is very nigh unto thee, in thy mouth, and in thy heart, that thou mayest do it.
15 Tazama, leo nimeweka mbele yako uzima na wema, mauti na uovu.
See, I have set before thee this day life and the good, death and the evil;
16 Iwapo utatii maagizo ya Yahwe Mungu wako, ambayo ninakuamuru leo kumpenda Yahwe Mungu wako, kutembea katika njia zake, na kushikilia amri zake, kanuni zake, na sheria zake, utaishi na kuongezeka, na Yahwe Mungu wako atakubariki katika nchi ambayo unaingia kumiliki.
In that I command thee this day to love the Lord thy God, to walk in his ways, and to keep his commandments and his statutes and his ordinances; that thou mayest live and multiply; and that the Lord thy God may bless thee in the land whither thou goest to possess it.
17 Lakini moyo wako ukigeuka, na usisikilize na badala yake unavutwa na kusujudia miungu mingine na kuwaabudu,
But if thy heart turn away, so that thou wilt not hearken, and thou sufferest thyself to be drawn away, and thou bowest down to other gods, and servest them:
18 basi leo nakutangazia kwako ya kwamba hakika utaangamia; siku zako hazitaongezeka katika nchi unayoipita juu ya Yordani kuingia na kumiliki.
I announce unto you this day, that ye shall surely perish; ye shall not remain many days upon the land, whither thou passest over the Jordan to go thither to possess it.
19 Naziita mbingu na nchi kushuhudia dhidi yako ya kuwa nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; kwa hiyo chagua uzima ili kwamba uweze kuishi, wewe na uzao wako.
I call heaven and earth as witnesses against you this day, that I have set before you life and death, the blessing and the curse; therefore choose thou life, in order that thou mayest live, both thou and thy seed;
20 Fanya hivi ili umpende Yahwe Mungu wako, kutii sauti yake, na kung’ang’ania kwake. Kwa maana yeye ni uzima wako na urefu wa siku zako; fanya hivi ili kwamba uweze kuishi katika nchi ambayo Yahwe aliapa kwa mababu zako, kwa Abrahamu, kwa Isaka, na kwa Yakobo, kuwapatia.
To love the Lord thy God, to hearken to his voice, and to cleave unto him; for he is thy life, and the length of thy days; that thou mayest dwell in the land which the Lord swore unto thy fathers, to Abraham, to Isaac, and to Jacob, to give unto them.