< Torati 27 >
1 Musa na wazee wa Israeli waliwaamuru watu na kusema, “Zishikeni amri zote ninazowaamuru leo.
2 Katika siku mtakapopita juu ya Yordani kwenye nchi ambayo Yahwe Mungu wako anawapatia, mnapaswa kutengeneza mawe kiasi makubwa na kuyachapa kwa lipu.
3 Mnatakiwa kuyaandika juu yake maneno yote ya sheria hii pale mtakapovuka; ili muweze kwenda katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anawapatia, nchi inayotiririka kwa maziwa na asali, kama Yahwe, Mungu wa mababu zenu, alivyowaahidi.
4 Mtakapovuka juu ya Yordani, yapangane haya mawe ninayowaamuru leo, juu ya mlima wa Ebali, na myapige kwa lipu.
5 Hapo mnapaswa kujenga dhabahu kwa Yahwe Mungu wako, dhabahu la mawe; lakini hautakiwi kuinua chombo cha chuma kujenga mawe.
6 Unatakiwa kujenga dhabahu ya Yahwe Mungu wako kwa mawe yasiyokuwa na kazi; unatakiwa kutoa dhabihu ya kuteketeza juu yake kwa Yahwe Mungu wako,
7 na utatoa sadaka ya pamoja na utakula pale; utafurahia mbele ya Yahwe Mungu wako.
8 Utaandika juu ya mawe maneno yote ya sheria hii kwa wazi.
9 Musa na makuhani, Walawi, waliongea na Waisraeli wote na kusema, “Nyamazeni na sikilizeni Israel: Leo mmekuwa watu wa Yahwe Mungu wenu.
10 Mnapaswa basi kutii sauti ya Yahwe Mungu wenu na kutii amri na sheria zake ambazo ninawaamuru leo.”
11 Musa aliwaamuru watu siku hiyo hiyo na kusema,
12 “Makabila haya yanapaswa kusimama katika mlima Gerizimu kuwabariki watu baada ya nyinyi kuvuka Yordani; Simeoni, Lawi, Judah, Isakari, Yusufu na Benyamini.
13 Haya ni makabila ambayo lazima yasimame juu yam lima Ebali kutamka laana: Rubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dan na Naftali.
14 Walawi watajibu na kusema kwa wanamume wote wa Israeli kwa sauti kubwa:
15 “Alaaniwe mwanamume atakayechonga sanamu au kinyago, chukizo kwa Yahwe, kazi ya mikono ya fundi, ambayo ataifanya sirini”. Kisha watu wote wanapaswa kujibu na kusema, ‘Amina’.
16 Alaaniwe mwanamume atakayemuaibisha baba yake au mama yake. Kisha watu wote waseme, 'Amina'.
17 Alaaniwe mwanamume anayetoa alama ya ardhi.' Kisha watu wote na waseme, 'Amina'.
18 Alaaniwe mwanamume asababishae kipofu kutoka nje ya barabara. Kisha watu wote waseme, ‘Amina’.
19 Alaaniwe mwanamume atumiaye nguvu kupokonya haki inayomstahili mgeni, yatima, au mjane. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
20 Alaaniwe mwanamume atakayelala na mke wa baba yake, kwa sababu atakuwa amechukua haki za baba yake’. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
21 Alaaniwe mwanamume atakayelala na aina yoyote ya mnyama’. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
22 Alaaniwe mwanamume atakayelala na dada yake, binti wa baba yake, au binti wa mama yake. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
23 Alaaniwe mwanamume atakayelala na mama mkwe’. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
24 Alaaniwe mwanamume atakayemuua jirani yake kwa siri’. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
25 Alaaniwe mwanamume apokeaye rushwa kumuua mtu asiye na hatia’. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
26 Alaaniwe mwanamume asiyethibitisha maneno ya sheria hii, ili kwamba ayatii.’ Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.