< Torati 23 >
1 Mwanamume aliyejeruhiwa kwa kupondwa au kukatwa haruhusiwi kuingia katika kusanyiko la Yahwe.
「凡外腎受傷的,或被閹割的,不可入耶和華的會。
2 Mwana haramu haruhusiwi kuwa miongoni mwa kusanyiko la Yahwe; kutoka hadi kizazi cha kumi cha uzao wake, hakuna kati yao anatakiwa kuwa kwenye kusanyiko la Yahwe.
「私生子不可入耶和華的會;他的子孫,直到十代,也不可入耶和華的會。
3 Muamori au Mmoabu haruhusiwi kuwa miongoni mwa kusanyiko la Yahwe; kutoka hadi kizazi cha kumi cha uzao wake, hakuna kati yao anatakiwa kuwa kwenye kusanyiko la Yahwe.
「亞捫人或是摩押人不可入耶和華的會;他們的子孫,雖過十代,也永不可入耶和華的會。
4 Hii ni kwa sababu hawakukutana nanyi kwa mkate na maji barabarani mlipokuwa mmetoka nje ya Misri, na kwa sababu walimkodisha Balaamu mwana wa Beoro kutoka Pethoro kule Aramu Naharaimu, awalaani.
因為你們出埃及的時候,他們沒有拿食物和水在路上迎接你們,又因他們雇了美索不達米亞的毗奪人比珥的兒子巴蘭來咒詛你們。
5 Lakini Yahwe Mungu wako hakumsikiliza Balaamu; badala yake, Yahwe Mungu wako aligeuza laana kuwa baraka kwenu, kwa sababu Yahwe Mungu wako aliwapenda.
然而耶和華-你的上帝不肯聽從巴蘭,卻使那咒詛的言語變為祝福的話,因為耶和華-你的上帝愛你。
6 Hamtakiwi kutafuta amani au mafanikio yao, katika siku zenu zote.
你一生一世永不可求他們的平安和他們的利益。
7 Hutakiwi kumchukia Muedomi, kwa maana ni kaka yako; hutakiwi kumchukia Mmisri, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi yake.
「不可憎惡以東人,因為他是你的弟兄。不可憎惡埃及人,因為你在他的地上作過寄居的。
8 Wazawa wa kizazi cha tatu wanaozaliwa kwao wanaweza kuwa katika kusanyiko la Yahwe.
他們第三代子孫可以入耶和華的會。」
9 Utakapotembea kijeshi dhidi ya maadui zako, basi unapaswa kujitenga na kila aina ya uovu.
「你出兵攻打仇敵,就要遠避諸惡。
10 Iwapo miongoni mwenu kuna mwanamume ambaye sio msafi kwa sababu ya jambo lililofanyika kwake usiku, basi anatakiwa atoke nje ya kambi ya jeshi; hatakiwi kurudi kambini.
「你們中間,若有人夜間偶然夢遺,不潔淨,就要出到營外,不可入營;
11 Jioni ikifika, anatakiwa ajiogeshe kwa maji; na jua likizama atarudi ndani kambini.
到傍晚的時候,他要用水洗澡,及至日落了才可以入營。
12 Pia unatakiwa kuwa na eneo nje ya kambi ambayo utakwenda;
「你在營外也該定出一個地方作為便所。
13 na utakuwa na kitu katika zana zako cha kuchimbia; utakapochuchumaa kujisaidia, unapaswa kuchimbia nacho na kisha kurudishia udongo na kufunika kile kilichotoka kwako.
在你器械之中當預備一把鍬,你出營外便溺以後,用以鏟土,轉身掩蓋。
14 Kwa maana Yahwe Mungu wako anatembea miongoni mwa kambi yenu kuwapa ushindi na kuwapa maadui zenu mkononi mwenu. Kwa hiyo kambi yenu lazima iwe takatifu, ili kwamba asione kitu chochote kichafu miongoni mwenu na kuwaacha.
因為耶和華-你的上帝常在你營中行走,要救護你,將仇敵交給你,所以你的營理當聖潔,免得他見你那裏有污穢,就離開你。」
15 Hutakiwi kumrudishia bwana mtumwa aliyetoroka kwake.
「若有奴僕脫了主人的手,逃到你那裏,你不可將他交付他的主人。
16 Mruhusu aishi pamoja nawe, katika mji wowote atakaochagua. Usimuonee.
他必在你那裏與你同住,在你的城邑中,要由他選擇一個所喜悅的地方居住;你不可欺負他。
17 Hapatakiwi kuwa na kahaba wa kidhehebu miongoni mwa mabinti wa Israeli, na wala hapatakiwi kuwa na kahaba wa kidhehebu miongoni mwa wana wa kiume wa Israeli.
「以色列的女子中不可有妓女;以色列的男子中不可有孌童。
18 Hautakiwi kuleta mshahara wa kahaba au mshahara wa mbwa katika nyumba ya Yahwe Mungu wako kwa kiapo chochote; kwa maana vyote hivi na machukizo mbele ya Yahwe Mungu wako.
娼妓所得的錢,或孌童所得的價,你不可帶入耶和華-你上帝的殿還願,因為這兩樣都是耶和華-你上帝所憎惡的。
19 Hutakiwi kumkopesha Muisraeli mwenzako kwa riba – riba ya fedha, riba ya chakula, au riba ya kitu chochote kinachokopeshwa kwa riba.
「你借給你弟兄的,或是錢財或是糧食,無論甚麼可生利的物,都不可取利。
20 Kwa mgeni unaweza kukopesha kwa riba; lakini kwa Muisraeli mwenzako haupaswi kukopesha kwa riba, ili kwamba Yahwe Mungu wako aweze kukubariki katika kila jambo uwekalo mkono wako, katika nchi ambayo mnaenda kumiliki.
借給外邦人可以取利,只是借給你弟兄不可取利。這樣,耶和華-你上帝必在你所去得為業的地上和你手裏所辦的一切事上賜福與你。
21 Unapofanya kiapo kwa Yahwe Mungu wako, haupaswi kukawia kuikamilsha, kwa maana Yahwe Mungu wako hakika atadai kiapo hicho; itakuwa dhambi kako usipokamilisha.
「你向耶和華-你的上帝許願,償還不可遲延;因為耶和華-你的上帝必定向你追討,你不償還就有罪。
22 Lakini iwapo utajizuia kutoa kiapo, haitakuwa dhambi kwako.
你若不許願,倒無罪。
23 Kile ambacho kimetoka kinywani mwako unapaswa kukifuata na kukitekeleza; kulingana na kiapo ulichotamka kwa Yahwe Mungu wako, chochote ulichotamka kwa hiari kwa kinywa chako.
你嘴裏所出的,就是你口中應許甘心所獻的,要照你向耶和華-你上帝所許的願謹守遵行。
24 Utakapokwenda katika shamba la mizabibu la jirani yako, unatakiwa kula mizabibu idadi yoyote unayotaka, lakini hautakiwi kuhifadhi yoyote katika kikapu chako.
「你進了鄰舍的葡萄園,可以隨意吃飽了葡萄,只是不可裝在器皿中。
25 Utakapokwenda katika shamba la zao lililoiva la jirani yako, unaweza kuvuna kichwa cha mavuno kwa mkono wako, lakini haupaswi kutumia mundu kuvuna zao lililoiva la jirani yako.
你進了鄰舍站着的禾稼,可以用手摘穗子,只是不可用鐮刀割取禾稼。」