< Torati 19 >
1 Wakati Yahwe Mungu wenu anayafutilia mbali mataifa, yale ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa nchi yao, na wakati mnakuja kwao na kuishi katika miji yao na nyumba,
2 mnapaswa kuchagua miji mitatu kwa ajili yenu katikati mwa nchi yenu ambayo Yahwe Mungu anawapa kuimiliki.
3 Mnapaswa kujenga barabara na kugawa mipaka ya nchi yenu katika maeneo matatu, nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anafanya kuimiliki, ili kwamba kila mmoja anayeua mtu mwingine apate kukimbia hapo.
4 Hii ni sheria kwa ajili ya mtu anayeua mwingine na anayekimbilia huko kuishi: yeyote auae jirani yake bila kujua, na hapo awali hakumchukia-
5 kama wakati mtu aingiapo katika msitu pamoja na jirani yake kukata kuni, na mkono wake ukata mti chini kwa shoka, na kichwa uteleza kutoka kwenye mpini na kumpiga jirani yake mpaka akafa- basi mtu huyu anapaswa kukimbilia katika moja ya miji hii na kuishi.
6 Vinginevyo damu ya mlipiza kisasi atamfuata yeye aliyetoa uhai, na kwa hasira kali anampita kwa sababu ilikuwa safari ndefu. Na anampiga na kumuua, ijapokuwa mtu huyo akustahili kufa; na hata akustahili adhabu ya kifo kwa sababu hakumchukia jirani yake kabla hili halijatokea.
7 Basi sasa ninakuamuru kuchagua miji mitatu kwa ajili yako.
8 Kama Yahwe Mungu wenu apanua mipaka yenu, kama alivyoapa kwa mababu zenu kufanya, na kuwapa nchi yote ambayo amewaahadia kuwapa mababu zenu;
9 kama mnazishika amri hizi zote kuzifanya, ambazo ninakuamuru leo- amri za kumpenda Yahwe Mungu wenu na daima kutembea katika njia zake, basi mnapaswa kuongeza miji mitatu zaidi kwa ajili yenu, isipokuwa ile mitatu.
10 Fanya hivi ili kwamba damu isiyo na hatia isimwangwe katikati ya nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa kwa ajili ya urithi, ili kwamba pasiwepo hatia ya damu kwenu.
11 Lakini kama yeyote anamchukia jirani yake, uongo unamsubiri, uinuka dhidi yake, na majeraha ya kufa kwake ili kwamba anakufa, na kama basi anakimbia katika moja ya miji hii-
12 basi wazee wa mji wake wanapaswa kumtoa na kumrudisha toka huko, na kumkabizi katika mkono wa ndugu mhusika, ili kwamba amuue.
13 Jicho lako halipaswi kumuonea huruma; badala yake; unapaswa kuondoa hatia ya damu kutoka Israel, ili kwamba iwe vizuri kwako.
14 Haupaswi kuondoa alama ya jirani yako ambayo wameweka katika eneo muda mrefu, katika urithi wako ambao utarithi, katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupa kumiliki.
15 Shahidi moja peke hapaswi kuinuka dhidi ya mtu kwa ajili ya uovu wowote, au kwa ajili ya dhambi yoyote, katika jambo lolote ambalo amefanya dhambi; kwa kinywa cha mashahidi wawili, au kwa kinywa cha mashahidi watatu, kunapaswa jambo lolote lilithibitishwe.
16 Kama ushuhuda wa mtu asiye na haki anainua dhidi ya mtu yeyote kushuhudia dhidi yake kwa mambo mabaya.
17 Basi watu wote wawili, mmoja kati ya yule utata upo, anapaswa kusimama mbele ya Yahwe, mbele ya makuhani na waamuzi ambao wanatumika siku hizo.
18 Waamuzi wanapaswa kuchunguza kwa uangalifu; ona, kama ushahidi ni ushahidi wa uongo na umeshuhudiwa kwa uongo dhidi ya ndugu yake,
19 basi unapaswa kufanya kwake, kama alivyokusudia kufanya kwa ndugu yake, na utaondoa uovu kutoka miongoni mwenu.
20 Basi wale wanaobaki watasikia na kuogopa, na kuanzia hapo na kuendelea hawatafanya tena aina ya ouvu miongoni mwao.
21 Macho yako hapaswi kuona huruma; maisha yatalipa kwa maisha, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.