< Torati 18 >

1 Makuhani, ambao ni Walawi, na makabila yote ya Lawi, hayatakuwa na mgao wala urithi pamoja na Israel; wanapaswa kula dhabihu ya Yahwe iliyotengenezwa kwa moto kama urithi wao.
The priests, the Levites, [and] the whole tribe of Levi, shall have no portion nor inheritance with Israel: Jehovah's offerings by fire, and his inheritance shall they eat,
2 Hawatakuwa na urithi miongoni mwa ndugu zao; Yahwe ni urithi wao, kama alivyosema nao.
but they shall have no inheritance among their brethren: Jehovah, he is their inheritance, as he hath said unto them.
3 Hii ni sababu ya makuhani kutoka kwa watu, kutoka kwa wale wanaotoa dhabihu, kama itakuwa ng'ombe au kondoo: wanapaswa kutoa kwa kuhani bega, mashavu mawili, na sehemu za ndani.
And this shall be the priest's due from the people, from them that sacrifice a sacrifice, whether ox, or sheep: they shall give unto the priest the shoulder, and the jawbones, and the maw.
4 Mazao ya kwanza ya nafaka zako, mvinyo wako mpya, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo zako, unapaswa umpe.
The firstfruits [also] of thy corn, of thy new wine, and of thine oil, and the firstfruits of the shearing of thy sheep, shalt thou give him;
5 Kwa kuwa Yahwe Mungu wako amemchagua kutoka kwenye makabila yote yako kusimama kutumika kwa jina la Yahwe, yeye na wana wake milele.
for Jehovah thy God hath chosen him out of all thy tribes, that he may stand to serve in the name of Jehovah, he and his sons continually.
6 Kama Mlawi anatoka kati ya miji yenu nje ya Israel yote kutoka ambapo anaishi, na utamani kwa moyo wake wote kuja katika eneo Yahwe atachagua,
And if the Levite shall come from one of thy gates out of all Israel, where he sojourneth, and shall come according to all the desire of his soul unto the place which Jehovah will choose,
7 basi anapaswa kutumika kwa jina la Yahwe Mungu wake kama ndugu zake wote Walawi wanafanya, wanaosimama mbele ya Yahwe.
and shall serve in the name of Jehovah his God, as all his brethren the Levites that stand there before Jehovah,
8 Wanapaswa kuwa na mgao wa kufanana wa kula, badala ya kile kinachokuja kutokana na mauzo ya urithi wa familia yake.
— they shall have like portions to eat, besides that which he hath sold of his patrimony.
9 Wakati mmekuja katika nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa, mnapaswa kujifunza kuangalia machukizo ya mataifa.
When thou art come into the land which Jehovah thy God giveth thee, thou shalt not learn to do according to the abominations of those nations.
10 Pasipatikana miongoni mwenu mmoja anayemweka kijana wake au binti yake kwenye moto, yeyote anatumia uganga, yeyote anatabiri, au mchawi, mchawi yeyote,
There shall not be found among you he that maketh his son or his daughter to pass through the fire, that useth divination, that useth auguries, or an enchanter, or a sorcerer,
11 yeyote aongeae na wafu, au yeyote aongeae na roho.
or a charmer, or one that inquireth of a spirit of Python, or a soothsayer, or one that consulteth the dead.
12 Kwa yeyote afanyae mambo haya ni chukizo kwa Yahwe; ni kwa sababu ya machukizo haya ambayo Yahwe Mungu wenu anawaondosha mbele zenu.
For every one that doeth these things is an abomination to Jehovah, and because of these abominations Jehovah thy God doth dispossess them from before thee.
13 Mnapaswa kuwa wakamilifu mbele ya Yahwe Mungu wenu.
Thou shalt be perfect with Jehovah thy God.
14 Kwa mataifa haya ambayo mtayafukuza kusikiliza wale wafanyao uchawi na uganga; lakini kwenu, Yahwe Mungu wenu amewakataza ninyi kufanya hivyo.
For these nations, which thou shalt dispossess, hearkened unto those that use auguries, and that use divination; but as for thee, Jehovah thy God hath not suffered thee [to do] so.
15 Yahwe Mungu wenu atainua kwa ajili yenu nabii kutoka miongoni mwenu, mmoja wa ndugu zenu, kama mimi. Mnapaswa kumsikiliza.
Jehovah thy God will raise up unto thee a prophet from the midst of thee, of thy brethren, like unto me; unto him shall ye hearken;
16 Hiki ndicho mlichouliza kutoka kwa Yahwe Mungu wenu huko Horebu katika siku ya kusanyiko, kusema, “Acha tusisikie tena sauti ya Yahwe Mungu wetu, wala kuona moto mkuu tena, wala tutakufa.”
according to all that thou desiredst of Jehovah thy God at Horeb on the day of the assembly, saying, Let me not hear again the voice of Jehovah my God, neither let me see this great fire any more, that I die not.
17 Yahwe alisema nami, “Kile walichosema ni kizuri.
And Jehovah said unto me, They have well spoken that which they have spoken.
18 Nitamwinua nabii kwa ajili yao kutoka miongoni mwa ndugu zao, kama wewe. Nitaweka maneno yangu katika kinywa chake, na ataongea nao yote niliyowakuamuru.
A prophet will I raise up unto them from among their brethren, like unto thee, and will put my words in his mouth, and he shall speak unto them all that I shall command him.
19 Itakuwa kama yeyote hatasikia maneno yangu ambayo anazungumza kwa jina langu, nitalitaka kwake.
And it shall come to pass that the man who hearkeneth not unto my words which he shall speak in my name, I will require it of him.
20 Lakini nabii ambaye anazungumza neno kwa kiburi kwa jina langu, neno ambalo sijamuamuru kusema, au ambaye anayezungumza kwa jina la miungu mingine, huyo nabii atakufa.
But the prophet who shall presume to speak a word in my name that I have not commanded him to speak, or that shall speak in the name of other gods, that prophet shall die.
21 Hivyo ndivyo unapaswa kusema katika mioyo yenu: “Tutagunduaje kuwa ujumbe ambao Yahwe hajazungumza?
And if thou say in thy heart, How shall we know the word that Jehovah hath not spoken?
22 Mtagundua ujumbe ambao Yahwe amezungumza pindi nabii azungumzapo kwa jina la Yahwe. Kama hiyo haitokei wala kufanyika, basi hicho ni kile ambacho Yahwe hajazungumza na nabii amezungumza kwa kiburi, na hampaswi kumuogopa.
When a prophet speaketh in the name of Jehovah, and the thing followeth not, nor cometh to pass, that is the word which Jehovah hath not spoken; the prophet hath spoken it presumptuously: be not afraid of him.

< Torati 18 >