< Torati 17 >

1 Haupaswi kumtolea dhabihu Yahwe Mungu wako ng'ombe au kondoo aliye na kasoro au kitu chochote kibaya, kwa kuwa hiyo itakuwa chukizo kwa Yahwe Mungu wako.
Msimtolee Bwana Mungu wenu dhabihu ya maksai au kondoo ambaye ana dosari yoyote au hitilafu ndani yake, kwa kuwa hilo litakuwa chukizo kwake.
2 Kama kunapatikana miongoni mwenu, ndani ya malango ya mji wowote ambao Yahwe Mungu wenu anawapatia, mwanaume yoyote au mwanamke ambaye anafanya uovu mbele ya Yahwe Mungu wenu kuiharibu agano lake -
Ikiwa mwanaume au mwanamke anayeishi kati ya mojawapo ya miji akupayo Bwana, anakutwa anafanya uovu mbele za Bwana Mungu wenu, kwa kuvunja Agano lake,
3 yoyote ambaye ameenda na kuabudu miungu mingine na kuisujudia, wala jua, mwezi, au kati ya jeshi la mbinguni- hakuna chochote nimekuamuru,
naye amekwenda kinyume na agizo langu kuabudu miungu mingine na kuisujudia, kama vile jua, mwezi au nyota za angani,
4 na kama ungeambiwa kuhusu hiki, au kama una mifugo- basi unapaswa kufanya uchunguzi wa makini. Kama ni kweli na hakika kwamba chukizo kama hilo limefanyika Israeli-
hili likiwa limeletwa mbele yenu, ni lazima kulichunguza kikamilifu. Ikiwa ni kweli na kuwa limehakikishwa kwamba hili ni chukizo lililofanyika katika Israeli,
5 -basi utamleta huyo mwanaume au mwanamke, aliyefanya uovu huu, katika malango ya mji, kwamba mwanaume kabisa au mwanamke, na umponde huyo mtu mpaka kufa.
mchukueni huyo mwanaume au mwanamke ambaye amelifanya tendo hili ovu kwenye lango la mji wenu na kumpiga mawe mtu huyo mpaka afe.
6 Kwa kinywa cha mashahidi wawili, au mashahidi watatu, itakuwa yeye anayepaswa kuuwawa; lakini kwa kinywa cha shahidi mmoja peke hatauwawa.
Kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu mtu huyo atauawa, bali hakuna mtu atakayeuawa kwa ushuhuda wa shahidi mmoja tu.
7 Mkono wa mashahidi unapaswa kuwa wa kwanza kumuuwa, na badae mkono wa watu wote; na mtamuondoa muovu miongoni mwenu.
Ni lazima kwanza mikono ya mashahidi itangulie kumuua huyo mtu, kisha mikono ya watu wote. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.
8 Kama jambo linatokea ambalo ni gumu kwenu kufanya maamuzi- pengine swali la mauaji au kifo cha ajali, haki ya mtu mmoja na haki ya mtu mwingine, au swali moja la aina ya kuzulu kufanyika, au aina nyingine ya jambo-mambo ya utata ndani ya malango yenu, basi utapaswa kwenda kwenye eneo ambalo Yahwe Mungu wako atachagua kama patakatifu pake.
Kama mashauri yanaletwa katika mahakama zenu ambayo ni magumu zaidi kwenu kuyaamua, ikiwa ni umwagaji wa damu, madai au mashambulio, yapelekeni mahali ambapo Bwana Mungu wenu atapachagua.
9 Utapaswa kwenda kwa makuhani, wazao wa Lawi, na kwa mwamuzi atakayetumika kwa wakati huo; mtatafuta ushauri wao, na watawapa ninyi maamuzi.
Nendeni kwa makuhani, ambao ni Walawi, na kwa mwamuzi ambaye atakuwa kazini wakati huo. Ulizeni kwao nao watawapa maamuzi.
10 Mnapaswa kufuata sheria mliyopewa, katika eneo Yahwe atachagua kama patakatifu pake. Mtakuwa makini kufanya kila kitu ambacho wanawaelekeza kufanya.
Ni lazima mtende sawasawa na maamuzi watakayowapa mahali Bwana atakapopachagua. Kuweni waangalifu kufanya kila kitu watakachowaongoza kufanya.
11 Fuata sheria wanayowafundisha, na kufanya kulingana na maamuzi wanawapa. Msigeuke kutoka kwa kile wanawambia, kwa kulia au kushoto.
Fanyeni sawasawa na sheria wanayowafundisha na maamuzi wanayowapa. Msigeuke mkono wa kuume au kushoto kuacha kufanya yale wanayowaambia.
12 Yeyote anayefanya kwa kiburi, kwa kutomsikiliza kuhani anayesimama kutumika mbele ya Yahwe Mungu wako, au kwa kutomsikiliza mwamuzi- huyu mtu atakufa; mtaweka mbali uovu kutoka Israeli.
Mwanaume atakayeonyesha dharau kwa mwamuzi au kwa kuhani ambaye amewekwa kumtumikia Bwana Mungu wenu lazima auawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli.
13 Watu wote wanapaswa kusikia na kuogopa, na kutofanya kwa kiburi tena.
Watu wote watasikia na kuogopa, nao hawatakuwa wenye kudharau tena.
14 Wakati mlipokuja kwenye nchi ambayo Yahwe Mungu anawapa, na wakati mnamiliki na kuanza kuishi ndani yake, na halafu unasema, 'Nitajiwekea mfalme juu yangu, kama mataifa yote yanayonizunguka mimi,'
Wakati utakapoingia katika nchi anayowapa Bwana Mungu wenu kuimiliki na kukaa humo, nanyi mkasema, “Na tumweke mfalme juu yetu kama mataifa yanayotuzunguka,”
15 basi unapaswa kwa hakika kujiwekea mfalme juu yako mtu yeyote ambaye Yahwe atachagua. Unapaswa kujiweka kama mfalme juu yako mtu yeyote kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Haupaswi kuweka mgeni, ambaye si ndugu yenu, juu yenu.
kuweni na uhakika wa kumweka mfalme juu yenu ambaye Bwana Mungu wenu atamchagua. Ni lazima atoke miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msimweke mgeni juu yenu ambaye si ndugu wa Kiisraeli.
16 Lakini hapaswi kuzidisha farasi kwa ajili yake, wala kusababisha watu kurudi Misri ili kwamba aweze kuzidisha farasi, kwa kuwa Yahwe alikwisha sema kwako, 'Unapaswa kuanzia sasa usirudi njia hiyo tena.'
Hata hivyo, kamwe mfalme asijipatie hesabu kubwa ya farasi kwa ajili yake mwenyewe, au kuwafanya watu warudi Misri ili kupata farasi zaidi, kwa maana Bwana amekuambia, “Hamtairudia njia ile tena.”
17 Na hapaswi kuzidisha wake kwa ajili yake, ili kwamba moyo wake usigeuke kotoka kwa Yahwe; wala hapaswi sana kuzidisha kwa ajili yake fedha au dhahabu.
Kamwe asioe wake wengi, la sivyo moyo wake utapotoka. Kamwe asijilimbikizie kiasi kikubwa cha fedha na dhahabu.
18 Wakati aketipo kwenye kiti cha enzi cha ufalme wake, anapaswa kuandika kwenye kitabu kwa ajili yake nakala ya sheria hii, kutoka kwenye sheria ambayo iko mbele ya makuhani, ambao ni Walawi.
Atakapokuwa amekalia kiti cha ufalme wake, ajiandikie kwenye kitabu nakala ya sheria kwa ajili yake mwenyewe kutoka zile sheria za makuhani ambao ni Walawi.
19 Kitabu kinapaswa kuwa na yeye, na anapaswa kusoma ndani yake kwa siku zake zote, ili kwamba aweze kujifunza kumheshimu Yahwe Mungu wako, ili kwamba ashike maneno yote ya sheria hii na amri hizi, kuzishika.
Atakuwa na nakala hiyo, naye ataisoma siku zote za maisha yake ili kwamba ajifunze kumheshimu Bwana Mungu wake na kufuata kwa uangalifu maneno yote ya sheria hii na amri hizi,
20 Anapaswa kufanya hivi ili kwamba moyo wake usiinuliwe zaidi ya ndugu zake, na ili kwamba asigeuke mbali na amri, kwa kulia au kwa kushoto' kwa kusudi kwamba aweze kuzidisha siku zake katika ufalme wake, yeye na watoto wake, miongoni mwa Israel.
naye asijifikirie kuwa ni bora kuliko ndugu zake na kuipotosha sheria. Ndipo yeye na wazao wake watatawala katika ufalme wake kwa muda mrefu katika Israeli.

< Torati 17 >