< Torati 16 >

1 Angalia mwezi wa Abibu, na uishike pasaka ya Yahwe Mungu wako, kwa kuwa katika mwezi wa Abibu Yahwe Mungu wako alikuleta toka Misri usiku.
あなたはアビブの月を守って、あなたの神、主のために過越の祭を行わなければならない。アビブの月に、あなたの神、主が夜の間にあなたをエジプトから導き出されたからである。
2 Utamtolea dhabibu ya pasaka Yahwe Mungu wako na baadhi ya mifugo na wanyama kwenye eneo ambalo Yahwe atachagua kama patakatifu pake.
主がその名を置くために選ばれる場所で、羊または牛をあなたの神、主に過越の犠牲としてほふらなければならない。
3 Hautakula mkate wa chachu pamoja nayo, siku saba utakula mkate usio na chachu, mkate wa mateso; kwa kuwa mlitoka katika nchi ya Misri kwa haraka. Fanya haya katika siku zako zote za maisha yako ili uweze kukumbuka akilini siku mliotoka nchi ya Misri.
種を入れたパンをそれと共に食べてはならない。七日のあいだ、種入れぬパンすなわち悩みのパンを、それと共に食べなければならない。あなたがエジプトの国から出るとき、急いで出たからである。こうして世に生きながらえる日の間、エジプトの国から出てきた日を常に覚えなければならない。
4 Hakuna chachu inapaswa kuonekana miongoni mwenu ndani ya mipaka yenu wakati wa siku saba; wala nyama yoyote mnayotoa dhabihu jioni kwa siku ya kwanza inabaki mpaka asubuhi.
その七日の間は、国の内どこにもパン種があってはならない。また初めの日の夕暮にほふるものの肉を、翌朝まで残しておいてはならない。
5 Msitoe dhabihu ya pasaka kati ya malango yenu ya ndani ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa.
あなたの神、主が賜わる町の内で、過越の犠牲をほふってはならない。
6 Badala yake, toa dhabihu katika eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua kama patakatifu pake. Hapo mtatoa dhabihu ya pasaka jioni wakati jua linazama, kwa wakati huo wa mwaka mlitoka Misri.
ただあなたの神、主がその名を置くために選ばれる場所で、夕暮の日の入るころ、あなたがエジプトから出た時刻に、過越の犠牲をほふらなければならない。
7 Mtapaswa kuichoma na kuila katika eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua; asubuhi mtageuka na kwenda kwenye mahema yenu.
そしてあなたの神、主が選ばれる場所で、それを焼いて食べ、朝になって天幕に帰らなければならない。
8 Kwa siku sita mtakula mkate usiotia chachu; katika siku ya saba kutakuwa na kusanyiko makini kwa ajili ya Yahwe Mungu wenu; katika siku hiyo hamtafanya kazi.
六日のあいだ種入れぬパンを食べ、七日目にあなたの神、主のために聖会を開かなければならない。なんの仕事もしてはならない。
9 Mtahesabu wiki saba kwa ajili yenu; tangu wakati mlipoanza kuweka mundu kwenye nafaka iliyosimama mtapaswa kuanza kuhesabu wiki saba.
また七週間を数えなければならない。すなわち穀物に、かまを入れ始める時から七週間を数え始めなければならない。
10 Mtapaswa kushika wiki za sherehe ya Yahwe Mungu wenu pamoja na mchango wa sadaka ya utayari kutoka mkono wako ambayo utatoa, kulingana na Yahwe alivyokubariki.
そしてあなたの神、主のために七週の祭を行い、あなたの神、主が賜わる祝福にしたがって、力に応じ、自発の供え物をささげなければならない。
11 Utafurahi mbele ya Yahwe Mungu wako- wewe, kijana wako, binti wako, mjakazi wako wa kiume, mjakazi wako wa kike, Mlawi aliye katika malango yako, na mgeni, yatima, na mjane alio miongoni mwenu, katika eneo ambalo Yahwe Mungu wako atachagua kwa ajili ya patakatifu pake.
こうしてあなたはむすこ、娘、しもべ、はしためおよび町の内におるレビびと、ならびにあなたがたのうちにおる寄留の他国人と孤児と寡婦と共に、あなたの神、主がその名を置くために選ばれる場所で、あなたの神、主の前に喜び楽しまなければならない。
12 Utakumbuka akilini kwamba ulikuwa mtumwa Misri; unapaswa kuangalia na kuzishika amri hizi.
あなたはかつてエジプトで奴隷であったことを覚え、これらの定めを守り行わなければならない。
13 Unapaswa kushika sherehe za vibanda kwa siku saba baada ya kuwa mmekusanya mavuno toka kwenye sakafu ya mapura na kutoka kwenye kinu chako cha divai.
打ち場と、酒ぶねから取入れをしたとき、七日のあいだ仮庵の祭を行わなければならない。
14 Utafurahi wakati wa sherehe- wewe, kijana wako, binti wako, mjakazi wako wa kiume, mjakazi wako wa kike, Mlawi, na mgeni, na yatima na mjane walio ndani ya malango yako.
その祭の時には、あなたはむすこ、娘、しもべ、はしためおよび町の内におるレビびと、寄留の他国人、孤児、寡婦と共に喜び楽しまなければならない。
15 Kwa siku saba unapaswa kuangalia sherehe ya Yahwe Mungu wako katika eneo ambalo Yahwe atachagua, kwa sababu Yahwe Mungu wako atakubariki katika mavuno yako yote na kazi ya mikono yako yote, na unapaswa kuwa na furaha kabisa.
主が選ばれる場所で七日の間、あなたの神、主のために祭を行わなければならない。あなたの神、主はすべての産物と、手のすべてのわざとにおいて、あなたを祝福されるから、あなたは大いに喜び楽しまなければならない。
16 Mara tatu kwa mwaka wanaume wako wote wanapaswa kuonekana mbele za Yahwe Mungu wako katika eneo ambalo atachagua: katika sherehe ya mkate usiotiwa chachu, katika sherehe za wiki, na sherehe ya vibanda; na hawataonekana mbele za Yahwe mikono mitupu;
あなたのうちの男子は皆あなたの神、主が選ばれる場所で、年に三度、すなわち種入れぬパンの祭と、七週の祭と、仮庵の祭に、主の前に出なければならない。ただし、から手で主の前に出てはならない。
17 badala yake, kila mtu atatoa kama awezavyo, kwamba mtajua baraka kwamba Yahwe Mungu wako amekupa.
あなたの神、主が賜わる祝福にしたがい、おのおの力に応じて、ささげ物をしなければならない。
18 Unapaswa kufanya waamuzi na maakida ndani ya malango yako ambayo Yahwe Mungu wako anakupa; watachukuliwa toka kila kabila, and watahukumu watu kwa hukumu ya haki.
あなたの神、主が賜わるすべての町々の内に、部族にしたがって、さばきびとと、つかさびととを、立てなければならない。そして彼らは正しいさばきをもって民をさばかなければならない。
19 Haupaswi kuiondoa haki kwa nguvu; haupaswi kuonesha upendeleo wala kuchukua rushwa, kwa kuwa rushwa upofusha macho ya hekima na kupotosha maneno ya haki.
あなたはさばきを曲げてはならない。人をかたより見てはならない。また賄賂を取ってはならない。賄賂は賢い者の目をくらまし、正しい者の事件を曲げるからである。
20 Unapaswa kufata baada ya haki, baada ya haki peke yake, ili kwamba uishi na kurithi nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupa.
ただ公義をのみ求めなければならない。そうすればあなたは生きながらえて、あなたの神、主が賜わる地を所有するにいたるであろう。
21 Haupaswi kujitengenezea Asherahi, aina yoyote ya mti, kando ya madhabahu ya Yahwe Mungu wako ambayo utakayojitengenezea.
あなたの神、主のために築く祭壇のかたわらに、アシラの木像をも立ててはならない。
22 Wala usijitengenezee jiwe takatifu la nguzo, ambalo Yahwe Mungu wako anachukia.
またあなたの神、主が憎まれる柱を立ててはならない。

< Torati 16 >