< Torati 14 >

1 Ninyi ni watu wa Yahwe Mungu wenu. Msijikate wenyewe, wala kunyoa sehemu za nyuso zenu kwa ajili ya wafu.
filii estote Domini Dei vestri non vos incidetis nec facietis calvitium super mortuo
2 Kwa kuwa mu taifa lilowekwa wakfu kwa Yahwe Mungu wenu, na Yahwe amewachagua kuwa watu kwa ajili ya urithi wake, zaidi kuliko watu wote walio juu ya uso wa dunia.
quoniam populus sanctus es Domino Deo tuo et te elegit ut sis ei in populum peculiarem de cunctis gentibus quae sunt super terram
3 Hampaswi kula kitu chochote kilicho chukizo.
ne comedatis quae inmunda sunt
4 Hawa ni wanyama ambao mnaweza kula: ng'ombe, kondoo, mbuzi,
hoc est animal quod comedere debetis bovem et ovem et capram
5 kulungu, paa, kulungu wa kiume, mbuzi wa mwituni, paa mweupe na pofu na kondoo wa mlimani
cervum capream bubalum tragelaphum pygargon orygem camelopardalum
6 Mnaweza kula wanyama wowote ambao wamegawanyika kwato, ambaye ana kwato zilizogawanyika mara mbili, na utafuna macheuo.
omne animal quod in duas partes ungulam findit et ruminat comedetis
7 Hata hivyo, hampaswi kula baadhi ya wanyama ambao utafuna macheuo au ambao wana kwato zilizogawanyika mara mbili: ngamia, sungura, pomono, kwa sababu watafuna macheuo lakini hawajagawanyika kwato, ni najisi kwenu.
de his autem quae ruminant et ungulam non findunt haec comedere non debetis camelum leporem choerogyllium quia ruminant et non dividunt ungulam inmunda erunt vobis
8 Nguruwe ni najisi kwenu pia kwa sababu amegawanyika kwato lakini hatafuni macheuo; ni najisi kwenu. Msile nyama ya nguruwe, na msiguse mizoga yao.
sus quoque quoniam dividit ungulam et non ruminat inmunda erit carnibus eorum non vescemini et cadavera non tangetis
9 Haya yaliyo ndani ya maji mnaweza kula: chochote kilicho na mapesi na magamba;
haec comedetis ex omnibus quae morantur in aquis quae habent pinnulas et squamas comedite
10 lakini chochote kisichokuwa na mapesi na magamba msile; ni najisi kwenu.
quae absque pinnulis et squamis sunt ne comedatis quia inmunda sunt
11 Ndege wote safi mnaweza kula.
omnes aves mundas comedite
12 Lakini hawa ni ndege ambao hampaswi kula: tai, tumbusi, kipungu,
inmundas ne comedatis aquilam scilicet et grypem et alietum
13 mwewe mwekundu na mweusi, aina yoyote ya kipanga.
ixon et vulturem ac milvum iuxta genus suum
14 Hampaswi kula aina yoyote ya kunguru,
et omne corvini generis
15 na mbuzi na mwewe wa usiku, Lanes ndege wa baharini, aina yoyote ya mwewe,
strutionem ac noctuam et larum atque accipitrem iuxta genus suum
16 bundi mdogo, bundi mkubwa, na bundi mweupe,
herodium et cycnum et ibin
17 Mwari, nyamafu ya tai, mnandio.
ac mergulum porphirionem et nycticoracem
18 Hampaswi kula korongo, aina yoyote ya kongoti, hudihudi, na popo.
onocrotalum et charadrium singula in genere suo upupam quoque et vespertilionem
19 Wote wenye mabawa; vitu vya utando ni najisi kwenu; havipaswi kuliwa.
et omne quod reptat et pinnulas habet inmundum erit nec comedetur
20 Mnaweza kula vitu vyote virukavyo.
omne quod mundum est comedite
21 Hampaswi kula chochote kinachokufa chenyewe; mnaweza kumpa mgeni ambaye yuko katika mji wenu, kwamba anaweza kula au mnaweza kuuza kwa mgeni. Kwa kuwa mu taifa lilolowekwa wakfu kwa ajili ya Yahwe Mungu wenu. Hampaswi kumchemusha mbuzi kijana katika maziwa ya mama yake.
quicquid morticinum est ne vescamini ex eo peregrino qui intra portas tuas est da ut comedat aut vende ei quia tu populus sanctus Domini Dei tui es non coques hedum in lacte matris suae
22 Hakika mnapaswa kutoa fungu la kumi la mavuno ya mbegu zenu zote, ambazo huja kutoka kwenye shamba kila mwaka.
decimam partem separabis de cunctis frugibus tuis quae nascuntur in terra per annos singulos
23 Mnapaswa kula mbele ya Yahwe Mungu wenu, katika eneo ambalo atachagua kama patakatifu pake, fungu la kumi la nafaka zenu, za mvinyo mpya, na mafuta yenu, na mzaliwa wa kwanza wa wanyama na mifugo, kwamba mnaweza kujifunza daima kumheshimu Yahwe Mungu wenu.
et comedes in conspectu Domini Dei tui in loco quem elegerit ut in eo nomen illius invocetur decimam frumenti tui et vini et olei et primogenita de armentis et ovibus tuis ut discas timere Dominum Deum tuum omni tempore
24 Kama safari ni ndefu kwenu na kwamba hamwezi kuibeba, kwa sababu eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua kama patakatifu pake ni mbali kwenu, basi, wakati Yahwe Mngu anawabariki,
cum autem longior fuerit via et locus quem elegerit Dominus Deus tuus tibique benedixerit nec potueris ad eum haec cuncta portare
25 mtabadilisha sadaka katika pesa. Fungeni pesa kwenye mkono, na nendeni kwenye eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua.
vendes omnia et in pretium rediges portabisque manu tua et proficisceris ad locum quem elegerit Dominus Deus tuus
26 Huko mtatumia pesa kwa chochote mnatamani kwa ng'ombe au kondoo, au kwa mvinyo, au kwa kinywaji imara, au kwa chochote mnatamani; mtakula hapo mbele ya Yahwe Mungu wenu, na mtafurahi, nyie na nyumba zenu.
et emes ex eadem pecunia quicquid tibi placuerit sive ex armentis sive ex ovibus vinum quoque et siceram et omne quod desiderat anima tua et comedes coram Domino Deo tuo et epulaberis tu et domus tua
27 Mlawi ambaye yuko malangoni mwenu- msimsahau, kwa kuwa hana sehemu wala urithi pamoja nanyi.
et Levita qui intra portas tuas est cave ne derelinquas eum quia non habet aliam partem in possessione tua
28 Mwisho mwa kila miaka mitatu mtawasilisha mafungu yote ya kumi ya mazao kwa mwaka huo huo, na mtatunza katika malango yenu;
anno tertio separabis aliam decimam ex omnibus quae nascuntur tibi eo tempore et repones intra ianuas tuas
29 na Mlawi, kwa sababu hana sehemu wala urithi pamoja nanyi, na mgeni, na yatima, na wajane walio ndani ya malango yenu, watakuja na kula na kurithika. Fanya hivyo kwa Yahwe Mungu wenu aweze kuwabariki katika kazi zote za mikono yenuo mnazofanya.
venietque Levites qui aliam non habet partem nec possessionem tecum et peregrinus et pupillus ac vidua qui intra portas tuas sunt et comedent et saturabuntur ut benedicat tibi Dominus Deus tuus in cunctis operibus manuum tuarum quae feceris

< Torati 14 >