< Danieli 8 >
1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa mfalme Belshaza, mimi Danieli niliona maono (baada ya maono ya awali yaliyonipata).
ἔτους τρίτου βασιλεύοντος Βαλτασαρ ὅρασις ἣν εἶδον ἐγὼ Δανιηλ μετὰ τὸ ἰδεῖν με τὴν πρώτην
2 Nilipokuwa nikiangalia katika ndoto, niliona kwamba nilikuwa katika mji wa Shushani wenye ngome katika jimbo la Elamu. Niliona katika ndoto kuwa nilikuwa karibu na mfereji wa Ulai.
καὶ εἶδον ἐν τῷ ὁράματι τοῦ ἐνυπνίου μου ἐμοῦ ὄντος ἐν Σούσοις τῇ πόλει ἥτις ἐστὶν ἐν Ἐλυμαΐδι χώρᾳ ἔτι ὄντος μου πρὸς τῇ πύλῃ Αιλαμ
3 Nilitazama juu na nikaona mbele yangu kondoo dume lenye mapembe mawili, limesimama pembeni mwa mfereji. Pembe moja lilikuwa refu kuliko jingine, lakini pembe ndefu ilikuwa inakua pole pole kuliko ile fupi na pembe fupi ilirefuka na kuizidi nyingine.
ἀναβλέψας εἶδον κριὸν ἕνα μέγαν ἑστῶτα ἀπέναντι τῆς πύλης καὶ εἶχε κέρατα καὶ τὸ ἓν ὑψηλότερον τοῦ ἑτέρου καὶ τὸ ὑψηλότερον ἀνέβαινε
4 Niliona kondoo mme akiishambulia magharibi, kisha kaskazini, na baadaye kusini; hakuna mnyama mwingine aliyeweza kusimama mbele yake. Hakuna yeyote aliyeweza kumwokoa yeyote katika mkono wake. Alifanya chochote kile alichokitaka, na alikuwa mtu mkubwa sana.
μετὰ δὲ ταῦτα εἶδον τὸν κριὸν κερατίζοντα πρὸς ἀνατολὰς καὶ πρὸς βορρᾶν καὶ πρὸς δυσμὰς καὶ μεσημβρίαν καὶ πάντα τὰ θηρία οὐκ ἔστησαν ἐνώπιον αὐτοῦ καὶ οὐκ ἦν ὁ ῥυόμενος ἐκ τῶν χειρῶν αὐτοῦ καὶ ἐποίει ὡς ἤθελε καὶ ὑψώθη
5 Na nilipokuwa natafakari juu ya haya, niliona beberu akitoka magharibi, na kuvuka katika uso wa dunia yote, akikimbia kwa kasi kana kwamba hakuonekana kama aligusa ardhini. Mbuzi huyo alikuwa na pembe kubwa katikati ya macho yake.
καὶ ἐγὼ διενοούμην καὶ ἰδοὺ τράγος αἰγῶν ἤρχετο ἀπὸ δυσμῶν ἐπὶ προσώπου τῆς γῆς καὶ οὐχ ἥπτετο τῆς γῆς καὶ ἦν τοῦ τράγου κέρας ἓν ἀνὰ μέσον τῶν ὀφθαλμῶν αὐτοῦ
6 Alienda mpaka kwa kondoo aliyekuwa na pembe mbili, nilikuwa nimemwona kondoo dume amesimama katika ukingo wa mfereji na mbuzi alikimbia kumwelekea kondoo dume kwa hasira kali.
καὶ ἦλθεν ἐπὶ τὸν κριὸν τὸν τὰ κέρατα ἔχοντα ὃν εἶδον ἑστῶτα πρὸς τῇ πύλῃ καὶ ἔδραμε πρὸς αὐτὸν ἐν θυμῷ ὀργῆς
7 Niliiona mbuzi ikija karibu na kondoo. Mbuzi alikuwa na hasira na kondoo, alimpiga kondoo na alizivunja pembe zake mbili. Kondoo hakuwa na nguvu za kusimama mbele zake. Mbuzi alimgonga kondoo akaanguka chini na akamkanyaga. Hapakuwa na yeyote wa kumwokoa kutoka katika nguvu zake.
καὶ εἶδον αὐτὸν προσάγοντα πρὸς τὸν κριόν καὶ ἐθυμώθη ἐπ’ αὐτὸν καὶ ἐπάταξε καὶ συνέτριψε τὰ δύο κέρατα αὐτοῦ καὶ οὐκέτι ἦν ἰσχὺς ἐν τῷ κριῷ στῆναι κατέναντι τοῦ τράγου καὶ ἐσπάραξεν αὐτὸν ἐπὶ τὴν γῆν καὶ συνέτριψεν αὐτόν καὶ οὐκ ἦν ὁ ῥυόμενος τὸν κριὸν ἀπὸ τοῦ τράγου
8 Ndipo mbuzi alikua akawa mkubwa, lakini alipokuwa na nguvu, pembe kubwa ilivunjwa, na katika sehemu yake zilichipuka na kukua pembe nne kubwa zilizochomoza kuelekea pepo nne za mbingu.
καὶ ὁ τράγος τῶν αἰγῶν κατίσχυσε σφόδρα καὶ ὅτε κατίσχυσε συνετρίβη αὐτοῦ τὸ κέρας τὸ μέγα καὶ ἀνέβη ἕτερα τέσσαρα κέρατα κατόπισθεν αὐτοῦ εἰς τοὺς τέσσαρας ἀνέμους τοῦ οὐρανοῦ
9 Kutoka katika pembe moja ilichipuka pembe nyingine, ilikuwa ndogo hapo awali, lakini baadaye ilikuwa pembe kubwa upande wa kusini, na mashariki, na katika nchi ya uzuri.
καὶ ἐξ ἑνὸς αὐτῶν ἀνεφύη κέρας ἰσχυρὸν ἓν καὶ κατίσχυσε καὶ ἐπάταξεν ἐπὶ μεσημβρίαν καὶ ἐπ’ ἀνατολὰς καὶ ἐπὶ βορρᾶν
10 Pembe ilikuwa kubwa na matokeo yake iliinua vita dhidi ya jeshi la mbinguni. Baadhi ya jeshi na nyota kadhaa zilitupwa chini duniani, na zilikanyagwa.
καὶ ὑψώθη ἕως τῶν ἀστέρων τοῦ οὐρανοῦ καὶ ἐρράχθη ἐπὶ τὴν γῆν ἀπὸ τῶν ἀστέρων καὶ ἀπὸ αὐτῶν κατεπατήθη
11 Alizidi kuwa mkubwa, mkubwa kama kamanda wa jeshi la kimungu. Sadaka za kuteketezwa za kila siku ziliondolewa mbali na yeye, na sehemu yake takatifu zilitiwa unajisi.
ἕως ὁ ἀρχιστράτηγος ῥύσεται τὴν αἰχμαλωσίαν καὶ δῑ αὐτὸν τὰ ὄρη τὰ ἀπ’ αἰῶνος ἐρράχθη καὶ ἐξήρθη ὁ τόπος αὐτῶν καὶ θυσία καὶ ἔθηκεν αὐτὴν ἕως χαμαὶ ἐπὶ τὴν γῆν καὶ εὐωδώθη καὶ ἐγενήθη καὶ τὸ ἅγιον ἐρημωθήσεται
12 Kwasababu ya uasi, pembe ya mbuzi ilipewa jeshi, na sadaka za kuteketezwa zitasitishwa. Pembe itautupa ukweli chini ardhini, na itafanikiwa katika kila jambo ilifanyalo.
καὶ ἐγενήθησαν ἐπὶ τῇ θυσίᾳ αἱ ἁμαρτίαι καὶ ἐρρίφη χαμαὶ ἡ δικαιοσύνη καὶ ἐποίησε καὶ εὐωδώθη
13 Kisha nilimsikia mtakatifu mmoja akiongea na mtakatifu mwingine akamjibu, “Mambo haya yatadumu kwa muda gani, maono haya ya sadaka ya kuteketezwa, dhambi ile iletayo uharibifu, ukabidhiajia wa sehemu takatifu, na jeshi la mbinguni kukanyagwa?
καὶ ἤκουον ἑτέρου ἁγίου λαλοῦντος καὶ εἶπεν ὁ ἕτερος τῷ φελμουνι τῷ λαλοῦντι ἕως τίνος τὸ ὅραμα στήσεται καὶ ἡ θυσία ἡ ἀρθεῖσα καὶ ἡ ἁμαρτία ἐρημώσεως ἡ δοθεῖσα καὶ τὰ ἅγια ἐρημωθήσεται εἰς καταπάτημα
14 Aliniambia, “Itadumu kwa jioni na asubuhi zipatazo 2, 300. Baada ya hapo, mahali patakatifu patawekwa sawa.”
καὶ εἶπεν αὐτῷ ἕως ἑσπέρας καὶ πρωὶ ἡμέραι δισχίλιαι τριακόσιαι καὶ καθαρισθήσεται τὸ ἅγιον
15 Wakati mimi Danieli, nilipoona maono, nilijaribu kuyaelewa. na hapo mbele yangu alisimama yule aliyeoneakana kama mtu.
καὶ ἐγένετο ἐν τῷ θεωρεῖν με ἐγὼ Δανιηλ τὸ ὅραμα ἐζήτουν διανοηθῆναι καὶ ἰδοὺ ἔστη κατεναντίον μου ὡς ὅρασις ἀνθρώπου
16 Niliisikia sauti ya mtu ikiita katikati ya kingo za mfereji wa Ulai. Alisema, “Gabrieli, msaidie mtu huyu kuelewa maono.”
καὶ ἤκουσα φωνὴν ἀνθρώπου ἀνὰ μέσον τοῦ Ουλαι καὶ ἐκάλεσε καὶ εἶπεν Γαβριηλ συνέτισον ἐκεῖνον τὴν ὅρασιν καὶ ἀναβοήσας εἶπεν ὁ ἄνθρωπος ἐπὶ τὸ πρόσταγμα ἐκεῖνο ἡ ὅρασις
17 Basi alikuja karibu na mahali niliposimama. Na alipokuja, niliogopa na nilisujudia hadi chini. Aliniambia,”Fahamu, mwana wa mtu, kwamba maono ni kwa ajili ya wakati wa mwisho.”
καὶ ἦλθε καὶ ἔστη ἐχόμενός μου τῆς στάσεως καὶ ἐν τῷ ἔρχεσθαι αὐτὸν ἐθορυβήθην καὶ ἔπεσα ἐπὶ πρόσωπόν μου καὶ εἶπέν μοι διανοήθητι υἱὲ ἀνθρώπου ἔτι γὰρ εἰς ὥραν καιροῦ τοῦτο τὸ ὅραμα
18 Alipokuwa anaongea na mimi, nilipata usiingizi mzito nikiwa nimelala kifudifudi. Kisha alinishika na kunisimamisha.
καὶ λαλοῦντος αὐτοῦ μετ’ ἐμοῦ ἐκοιμήθην ἐπὶ πρόσωπον χαμαί καὶ ἁψάμενός μου ἤγειρέ με ἐπὶ τοῦ τόπου
19 Akaniambia, “Tazama, nitakuonyesha kile kitachotokea baadaye katika kipindi cha ghadhabu, kwasababu maono haya yanahusu wakati wa mwisho uliopangwa.
καὶ εἶπέ μοι ἰδοὺ ἐγὼ ἀπαγγέλλω σοι ἃ ἔσται ἐπ’ ἐσχάτου τῆς ὀργῆς τοῖς υἱοῖς τοῦ λαοῦ σου ἔτι γὰρ εἰς ὥρας καιροῦ συντελείας μενεῖ
20 Na kuhusu kondoo mme uliyemwona, yule mwenye pembe mbili - ni wafalme wawili wa Umedi na Uajemi.
τὸν κριὸν ὃν εἶδες τὸν ἔχοντα τὰ κέρατα βασιλεὺς Μήδων καὶ Περσῶν ἐστι
21 Mbuzi dume ni mfalme wa Ugiriki. Pembe kubwa katikati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.
καὶ ὁ τράγος τῶν αἰγῶν βασιλεὺς τῶν Ἑλλήνων ἐστί καὶ τὸ κέρας τὸ μέγα τὸ ἀνὰ μέσον τῶν ὀφθαλμῶν αὐτοῦ αὐτὸς ὁ βασιλεὺς ὁ πρῶτος
22 Na kuhusu pembe iliyovunjika, ambayo katika nafasi yake pembe zingine nne zilichipuka - hizi ni falme nne zitakazoinuka kutoka katika taifa lake, lakini hazitakuwa na nguvu kubwa.
καὶ τὰ συντριβέντα καὶ ἀναβάντα ὀπίσω αὐτοῦ τέσσαρα κέρατα τέσσαρες βασιλεῖς τοῦ ἔθνους αὐτοῦ ἀναστήσονται οὐ κατὰ τὴν ἰσχὺν αὐτοῦ
23 Katika siku zijazo za falme hizo, wakati ambapo wahalifu watakuwa wamefikia kikomo chao, mfalme mwenye uso katili, na yeye mwenye akili sana, atainuka.
καὶ ἐπ’ ἐσχάτου τῆς βασιλείας αὐτῶν πληρουμένων τῶν ἁμαρτιῶν αὐτῶν ἀναστήσεται βασιλεὺς ἀναιδὴς προσώπῳ διανοούμενος αἰνίγματα
24 Nguvu zake zitakuwa kubwa, lakini si kwa nguvu zake mwenyewe. Atakuwa wa kustaajabisha kwa kile atakachokuwa anakiharibu; atafanya na kufanikiwa. Atawaangamiza watu wenye nguvu, watu miongoni wa watakatifu.
καὶ στερεωθήσεται ἡ ἰσχὺς αὐτοῦ καὶ οὐκ ἐν τῇ ἰσχύι αὐτοῦ καὶ θαυμαστῶς φθερεῖ καὶ εὐοδωθήσεται καὶ ποιήσει καὶ φθερεῖ δυνάστας καὶ δῆμον ἁγίων
25 Ataufanya udanganyifu usitawi chini ya mkono wake kwasababu ya ujanja wake. Atawaangamiza watu wengi bila kutegemea. Atainuka pia hata kinyume cha Mfalme wa wafalme, na atavunjwa, lakini si kwa mkono wowote wa binadamu.
καὶ ἐπὶ τοὺς ἁγίους τὸ διανόημα αὐτοῦ καὶ εὐοδωθήσεται τὸ ψεῦδος ἐν ταῖς χερσὶν αὐτοῦ καὶ ἡ καρδία αὐτοῦ ὑψωθήσεται καὶ δόλῳ ἀφανιεῖ πολλοὺς καὶ ἐπὶ ἀπωλείας ἀνδρῶν στήσεται καὶ ποιήσει συναγωγὴν χειρὸς καὶ ἀποδώσεται
26 Maono kuhusu jioni na asubuhi ulizoambiwa ni ya kweli. Lakini uyafunge maono haya, kwa kuwa yanahusu siku nyingi za wakati ujao.
τὸ ὅραμα τὸ ἑσπέρας καὶ πρωὶ ηὑρέθη ἐπ’ ἀληθείας καὶ νῦν πεφραγμένον τὸ ὅραμα ἔτι γὰρ εἰς ἡμέρας πολλάς
27 Ndipo mimi, Danieli nilichoka sana na nikalala nikiwa dhaifu kwa siku kadhaa. Kisha nikainuka na nikaenda kufanya kazi za mfalme. Lakini nilikuwa nimetishwa sana na maono, na hapakuwa na mtu yeyote aliyeweza kuyaelewa.
ἐγὼ Δανιηλ ἀσθενήσας ἡμέρας πολλὰς καὶ ἀναστὰς ἐπραγματευόμην πάλιν βασιλικά καὶ ἐξελυόμην ἐπὶ τῷ ὁράματι καὶ οὐδεὶς ἦν ὁ διανοούμενος