< Danieli 5 >
1 Mfalme Belshaza alifanya sherehe kubwa kwa kwa ajili ya wakuu wake wa kuheshimiwa wapatao elfu moja, na alikunywa divai mbele yao wote watu elfu moja.
伯沙撒王为他的一千大臣设摆盛筵,与这一千人对面饮酒。
2 Wakati Belshaza alipokuwa akionja divai, alitoa agizo la kuleta vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu au kwa fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka katika hekalu huko Yerusalemu, ambavyo yeye, na wakuu wake, na wake zake, na masuria waliweza kuvinywea.
伯沙撒欢饮之间,吩咐人将他父尼布甲尼撒从耶路撒冷殿中所掠的金银器皿拿来,王与大臣、皇后、妃嫔好用这器皿饮酒。
3 Watumishi walivileta vyombo ya dhahabu vilivyokuwa vimechukulia katika hekalu, nyumba ya Mungu huko Yerusalemu. Mfalme na wakuu wake, na wake zake na masuria walivinywea.
于是他们把耶路撒冷 神殿库房中所掠的金器皿拿来,王和大臣、皇后、妃嫔就用这器皿饮酒。
4 Walikunywa divai na kuzisifu sanamu zao zilizotengenezwa kwa dhahabu na fedha, shaba, chuma, mbao na mawe.
他们饮酒,赞美金、银、铜、铁、木、石所造的神。
5 Kwa wakati huo huo vidole vya mkono wa mtu vilionekana mbele ya kinara cha taa na kuandika katika ukuta uliopigwa lipu katika ikulu ya mfalme. Mfalme aliweza kuona sehemu ya mkono ulipokuwa unaandika.
当时,忽有人的指头显出,在王宫与灯台相对的粉墙上写字。王看见写字的指头
6 Ndipo uso wa mfalme ulibadilika na mawazo yake yalimwogopesha; miguu yake haikuweza kumfanya asimame, na magoti yake yalikuwa yakigongana kwa pamoja.
就变了脸色,心意惊惶,腰骨好像脱节,双膝彼此相碰,
7 Mfalme alitoa agizo kwa kupiga kelele, waletwe ndani wale ambao hudai wanaweza kuzungumza na wafu, watu wenye hekima, na wataalamu wa nyota. Mfalme akawaambia wale waliojulikana kwa hekima katika Babeli, “Yeyote atakayeyaeleza maandishi haya na maana yake atavikwa nguo za zambarau na atavikwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake. Naye atakuwa mtawala wa tatu wa juu kwa mamlaka katika ufalme.”
大声吩咐将用法术的和迦勒底人并观兆的领进来,对巴比伦的哲士说,谁能读这文字,把讲解告诉我,他必身穿紫袍,项带金链,在我国中位列第三。
8 Ndipo watu wote wa mfalme walikuwa wakijulikana kwa hekima yao waliingia ndani, lakini hawakuweza kuyasoma maandishi wala kueleza maana yake kwa mfalme.
于是王的一切哲士都进来,却不能读那文字,也不能把讲解告诉王。
9 Kisha mfalme Belshaza alishitushwa sana na mwonekano wa uso wake ulibadilika. Wakuu wake nao walishangazwa sana.
伯沙撒王就甚惊惶,脸色改变,他的大臣也都惊奇。
10 Ndipo sasa malkia alikuja katika nyumba ya sherehe kwasababu ya kile ambacho mfalme na wakuu wake walikuwa wamekisema. Malkia akasema, “Mfalme na aishi milele! Usiache mawazo yako yakakusumbua. Usiruhusu mwonekano wa uso wako ubadilike.
太后因王和他大臣所说的话,就进入宴宫,说:“愿王万岁!你心意不要惊惶,脸面不要变色。
11 Kuna mtu katika ufalme wako ambaye ana roho ya miungu watakatifu dani yake. Katika siku za baba yako, mwanga na weledi na hekima ya miungu ilipatikana ndani yake. Mfalme Nebukadneza, baba yako mfalme, alimfanya kuwa mkuu wa waganga, pamoja na mkuu wa wale wanazungumza na wafu, na wa wenye hekima, na wa wataalamu wa nyota.
在你国中有一人,他里头有圣神的灵,你父在世的日子,这人心中光明,又有聪明智慧,好像神的智慧。你父尼布甲尼撒王,就是王的父,立他为术士、用法术的,和迦勒底人,并观兆的领袖。
12 Roho bora, ufahamu, weledi, kutafsiri ndoto, kufafanua mafumbo na kutatua matatizo - hizi ni sifa zilizopatikana kwa mtu huyu Danieli, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Sasa mwiteni Danieli naye atawaambia maana ya kile kilichoandikwa.”
在他里头有美好的灵性,又有知识聪明,能圆梦,释谜语,解疑惑。这人名叫但以理,尼布甲尼撒王又称他为伯提沙撒,现在可以召他来,他必解明这意思。”
13 Ndipo Danieli alipoletwa mbele ya mfalme. Mfalme akamwambia, “Wewe ni yule Danieli, mmoja kati ya watu wa mateka wa Yuda, ambao baba yangu mfalme aliwaleta kutoka Yuda.
但以理就被领到王前。王问但以理说:“你是被掳之犹大人中的但以理吗?就是我父王从犹大掳来的吗?
14 Nimesikia habari kukuhusu wewe, kwamba roho ya miungu iko ndani yako, na ya kwamba mwanga na ufahamu na hekima bora inapatikana ndani yako.
我听说你里头有神的灵,心中光明,又有聪明和美好的智慧。
15 Na sasa watu wanaojulikana kwa hekima na wale wanaozungumza na wafu, wamekwisha kuletwa mbele yangu, ili kusoma maandishi haya na kunijulisha maana ya tafsiri yake, lakini hawakuweza kunijulisha tafsiri yake.
现在哲士和用法术的都领到我面前,为叫他们读这文字,把讲解告诉我,无奈他们都不能把讲解说出来。
16 Nimesikia kwamba unaweza kutoa tafsiri na kutatua matatizo. Sasa kama utaweza kusoma maandishi na kuniambia maana yake, utavikwa nguo za zambarau na kuwa na kuvalishwa mkufu wa dhahabu shingoni mwako, na utakuwa mtawala wa tatu mwenye mamlaka katika ufalme.”
我听说你善于讲解,能解疑惑;现在你若能读这文字,把讲解告诉我,就必身穿紫袍,项戴金链,在我国中位列第三。”
17 Kisha Danieli akajibu mbele ya mfalme, “Zawadi yako na iwe kwa ajili yako mwenyewe, na thawabu yako na umpe mtu mwingine. Hata hivyo, mfalme, nitakusomea maandishi na nitakwaambia maana.
但以理在王面前回答说:“你的赠品可以归你自己,你的赏赐可以归给别人;我却要为王读这文字,把讲解告诉王。
18 Na juu yako, Ewe mfalme, Mungu Aliye juu sana alimpa Nebukadneza baba yako ufalme, ukuu, heshima na enzi.
王啊,至高的 神曾将国位、大权、荣耀、威严赐与你父尼布甲尼撒;
19 Na kwasababu ya ukuu huo, Mungu alimpa watu wote, mataifa, na lugha walimtetemekea na kumwogopa. Aliwauwa wale aliotaka wafe na aliwaacha hai wale aliotaka waishi. Aliwainua wale aliowataka, na aliwashusha wale aliowataka.
因 神所赐他的大权,各方、各国、各族的人都在他面前战兢恐惧。他可以随意生杀,随意升降。
20 Lakini wakati moyo ulipokuwa na kiburi na roho yake ilifanywa kuwa mgumu na kwasababu hiyo alitenda kwa kiburi, alishushwa kutoka kiti chake cha enzi cha kifalme, na waliiondoa enzi yake.
但他心高气傲,灵也刚愎,甚至行事狂傲,就被革去王位,夺去荣耀。
21 Aliondolewa katika ubinadamu, alikuwa na akili za mnyama, na aliishi na punda wa mwituni. Alikula majani kama ng'ombe. Mwili wake ulilowanishwa kwa umande wa kutoka mbinguni mpaka pale alipojifunza kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme za watu na ya kwamba humweka mtu yeyote amtakaye juu yake.
他被赶出离开世人,他的心变如兽心,与野驴同居,吃草如牛,身被天露滴湿,等他知道至高的 神在人的国中掌权,凭自己的意旨立人治国。
22 Wewe mwana wake, Belshaza, haujaunyenyekeza moyo wako, ingawa aliyajua haya yote.
伯沙撒啊,你是他的儿子,你虽知道这一切,你心仍不自卑,
23 Umejiinua mwenyewe kinyume cha Bwana wa mbinguni. Katika nyumba yake walikuletea vyombo ambavyo wewe, wakuu wako, wake zako na masuria wako walivinywea, na kisha ukaisifia sana sanamu zilitengenezwa kwa fedha na dhahabu, shaba, chuma, mbao, na mawe - sanamu ambazo haziwezi kuona, kusikia wa kujua kitu chochote. Haujamheshimu Mungu ambaye anaishikilia pumzi yako katika mkono wake na ambaye anazijua njia zako zote.
竟向天上的主自高,使人将他殿中的器皿拿到你面前,你和大臣、皇后、妃嫔用这器皿饮酒。你又赞美那不能看、不能听、无知无识、金、银、铜、铁、木、石所造的神,却没有将荣耀归与那手中有你气息,管理你一切行动的 神。
24 Ndipo Mungu aliutuma mkono kutoka katika makao yake na maandishi haya yaliandikwa.
因此从 神那里显出指头来写这文字。
25 Haya ndiyo maandishi ambayo yaliandikwa: 'Mene, Mene, Tekeli na Peresin.'
“所写的文字是:‘弥尼,弥尼,提客勒,乌法珥新。’
26 Maana yake ni: 'Mene,' 'Mungu ameuhesabu ufalme wako na ameukomesha.'
讲解是这样:弥尼,就是 神已经数算你国的年日到此完毕。
27 'Tekeli' 'umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua.'
提客勒,就是你被称在天平里,显出你的亏欠。
28 'Peresi' 'ufalme wako umegawanyika na wamepewa Wamedi na Waajemi.'”
毗勒斯,就是你的国分裂,归与米底亚人和波斯人。”
29 Ndipo Belshaza alitoa agizo, na walimvalisha Danieli mavazi ya zambarau. Mkufu wa dhahabu walimvisha shingoni, na mfalme alitoa tamko juu ya Danieli kuwa atakuwa mtawala mwenye mamlaka ya nafasi ya tatu katika ufalme.
伯沙撒下令,人就把紫袍给但以理穿上,把金链给他戴在颈项上,又传令使他在国中位列第三。
30 Usiku ule Belshaza, mfalme wa Babeli aliuawa,
当夜,迦勒底王伯沙撒被杀。
31 na Dario Mwajemi aliuchukua ufalme alipokuwa na miaka ipatayo sitini na miwili.
米底亚人大流士年六十二岁,取了迦勒底国。