< Danieli 3 >
1 Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu ambayo ilikuwa na urefu wa dhiraa sitini na upana dhiraa sita. Aliiweka katika uwanda wa Dura katika jimbo la Babeli.
Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu, yenye kimo cha dhiraa sitini, na upana wa dhiraa sita, akaisimamisha kwenye tambarare ya Dura katika jimbo la nchi ya Babeli.
2 Kisha Nebukadneza alituma ujumbe wa kuwaita pamoja magavana wote wa majimbo, magavana wa mikoa, na magavana wa vijiji, pamoja na na washauiri, wahazini, waamuzi, mahakimu, na maafisa wengine wakuu wa majimbo ili waje kwa ajili ya uzinduzi wa sanamu aliyokuwa ameiweka.
Kisha mfalme akaita wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu na maafisa wengine wote wa jimbo kuja kuizindua sanamu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha.
3 Ndipo magavana wa majimbo, magavana wa mikoa, na magavana wa vijiji, pamoja na washauri, wahasibu, waamuzi, mahakimu, na maafisa wa juu wa majimbo walikusanyika kwa pamoja katika uzinduzi wa sanamu ambayo Nebukadneza aliyokuwa ameiweka. Walisimama mbele yake.
Basi wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu na maafisa wengine wa jimbo walikusanyika ili kuizindua sanamu ile Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha, nao wakasimama mbele ya hiyo sanamu.
4 Kisha mtangazaji alipiga kelele, “Enyi watu, mataifa, na lugha mmeamriwa
Ndipo mpiga mbiu akatangaza kwa sauti kubwa, “Enyi watu wa kabila zote, mataifa na watu wa kila lugha, hili ndilo mnaloamriwa kulifanya:
5 kwamba mtakaposikia sauti za pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki, ni sharti kuanguka na kuisujudia ninyi wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameiweka.
Mara mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari na aina zote za sauti za ala za uimbaji, lazima mwanguke chini na kuabudu sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza ameisimamisha.
6 Na yeyote asiyeanguka na kuiabuda, kwa wakati huo huo atatupwa katika tanuru la moto.”
Mtu yeyote ambaye hataanguka chini na kuiabudu sanamu hiyo, atatupwa saa iyo hiyo ndani ya tanuru iwakayo moto.”
7 Basi watu walilposikia sauti za pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki, watu wote, mataifa na lugha walianguka na kuisujudia wao wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo Nebukadneza mfalme alikuwa ameiweka.
Kwa hiyo, mara waliposikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, kinanda na aina zote za ala za uimbaji, watu wa kabila zote, mataifa na watu wa kila lugha wakaanguka chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha.
8 Wakati huu baadhi ya Walkadayo walikuja na kuleta mashitaka kinyume na Wayahudi.
Wakati huo baadhi ya Wakaldayo walijitokeza na kuwashtaki Wayahudi.
9 Walimwambia mfalme Nebukadneza, “mfalme aishi milele!
Wakamwambia Mfalme Nebukadneza, “Ee mfalme, uishi milele!
10 Ewe mfalme, umeweka amri kwamba kila mtu aisikiye sauti ya pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari, na aina zote za muziki, lazima kuanguka na kuisujudia sanamu ya dhahabu.
Ee mfalme, umetoa amri kwamba kila mmoja atakayesikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, kinanda, zumari na aina zote za ala za uimbaji lazima aanguke chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu,
11 Mtu yeyote asiyeanguka na kuiabudu sharti atupwe katika tanuru linalowaka moto.
na kwamba yeyote ambaye hataanguka chini na kuiabudu atatupwa saa iyo hiyo ndani ya tanuru iwakayo moto.
12 Sasa kuna baadhi ya Wayahudi ambao umewaweka juu masuala ya jimbo la Babeli; majina yao ni Shadraka, Meshaki, na Abednego. Mfalme, hawa watu hawakutii wewe. Hawataiabudu, kuitumikia wala kuisujudia wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo umeiweka.”
Lakini wako baadhi ya Wayahudi ambao umewaweka juu ya mambo ya jimbo la Babeli: yaani, Shadraki, Meshaki na Abednego, ambao hawakujali wewe, ee mfalme. Hawaitumikii miungu yako wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”
13 Ndipo Nebukadneza alijawa na hasira na ghadhabu, aliagiza kwamba Shadraka, Meshaki na Abednego waletwe kwake. Hivyo, waliwalete hawa watu mbele ya mfalme.
Mfalme Nebukadneza, akiwa amekasirika na mwenye ghadhabu kali, akawaita Shadraki, Meshaki na Abednego. Hivyo watu hawa wakaletwa mbele ya mfalme,
14 Nebukadneza aliwaambia, “Je mmejipanga katika akili zenu, enyi Shadraka, Meshaki na Abedinego, kwamba hamtaiabudu miungu yangu wala kuisujudia wenyewe sanamu ile ya dhahabu ambayo nimeiweka?
naye Nebukadneza akawauliza, “Je, ni kweli kwamba ninyi Shadraki, Meshaki na Abednego hamuitumikii miungu yangu wala kuiabudu sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha?
15 Basi sasa kama mko tayari - mtakaposikia sauti pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinumbi na zumari, aina zote za muziki - kuanguka chini na kuisujudia wenyewe sanamu ile ambayo nimeitengeneza, mambo yote yatakuwa mazuri. Lakini kama hamtaiabudu, mtatupwa mara katika tanuru la moto. Ni mungu gani atakayeweza kuwaokoa katika mikono yangu?”
Basi wakati mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari na aina zote za ala za uimbaji, kama mtakuwa tayari kusujudu na kuiabudu hiyo sanamu niliyoitengeneza, vyema sana. Lakini kama hamtaiabudu, mtatupwa saa iyo hiyo ndani ya tanuru iwakayo moto. Naye ni mungu yupi atakayeweza kuwaokoa ninyi, kutoka mkono wangu?”
16 Shadraka, Meshaki, na Abednego wakamjibu mfalme, “Nebukadneza, hatuhitaji kukujibu wewe katika jambo hili.
Shadraki, Meshaki na Abednego wakamjibu mfalme, “Ee Nebukadneza, hatuhitaji kujitetea mbele zako kuhusu jambo hili.
17 Kama kuna jibu, ni kwamba Mungu wetu ambaye tunamtumikia anaweza kutuhifadhi sisi salama katika katika tanuru la moto, na atatuokoa sisi katika mkono wako, mfalme.
Ikiwa tutatupwa ndani ya tanuru iwakayo moto, Mungu tunayemtumikia anaweza kutuokoa na moto, naye atatuokoa kutoka mkononi mwako, ee mfalme.
18 Kama sivyo, na ijulikane kwako, wewe mfalme, kwamba hatutaiabudu miungu yako, na wala hatutaisujudia wenyewe sanamu ya dhahabu uliyoiweka.
Lakini hata ikiwa hatatuokoa, ee mfalme, tunataka ufahamu kwamba, hatutaitumikia miungu yako wala kuiabudu sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”
19 Ndipo Nebukadneza alijawa na ghadhabu; mwonekano wa uso wake ulibadilika kinyume na Shadraka, Meshaki na Abedinego. Aliagiza kuwa tanuru lichochewe ukali mara saba zaidi kuliko lilivyokuwa kawaida.
Ndipo Nebukadneza akawa na ghadhabu kali sana kwa Shadraki, Meshaki na Abednego, nayo nia yake ikabadilika kwao. Akaagiza tanuru ichochewe moto mara saba kuliko kawaida yake
20 Kisha aliwaamuru baadhi ya watu wenye nguvu katika jeshi lake kuwafunga Shadraka, Meshaki na Abednego na kuwatupa katika tanuru liwakalo moto.
na kuwaamuru baadhi ya askari wake wenye nguvu zaidi katika jeshi lake kuwafunga Shadraki, Meshaki na Abednego na kuwatupa ndani ya tanuru iwakayo moto.
21 Walifungwa akali wakiwa wamevaa nguo zao, kanzu, kilemba, na mavazi mengine, na walitupa katika tanuru liwakalo moto.
Hivyo watu hawa, walifungwa na kutupwa ndani ya tanuru iwakayo moto wakiwa wamevaa majoho yao, suruali, vilemba na nguo zao nyingine.
22 Kwasababu ya agizo la mfalme lilifuatwa na tanuru lilikuwa na joto sana, miali ya moto iliwaua watu waliowatupa Shadraka, Meshaki, na Abedinego.
Amri ya mfalme ilikuwa ya haraka sana na tanuru ilikuwa na moto mkali kiasi kwamba miali ya moto iliwaua wale askari waliowapeleka Shadraki, Meshaki na Abednego.
23 Hawa wanaume watatu, Shadraka, Meshaki, na Abednego, waliangukia katika tanuru liwakalo moto wakali wamefungwa.
Watu hawa watatu walianguka ndani ya tanuru iwakayo moto wakiwa wamefungwa kwa uthabiti sana.
24 Kisha Nebukadneza mfalme alishangazwa na alisimam haraka. Aliwauliza washauri wake, “Je hatukutupa watu watatu wakiwa wamefungwa katika moto?” Nao walimjibu mfalme, “Hakika mfalme.”
Ndipo Mfalme Nebukadneza akashangaa, akainuka kwa haraka na kuwauliza washauri wake, “Je, hawakuwa watu watatu ambao tuliwafunga na kuwatupa ndani ya moto?” Washauri wakajibu, “Hakika, ee mfalme.”
25 Alisema, “Lakini ninaona watu wanne ambao hawajafungwa wakizunguka katika moto, na hawajaumizwa. Mng'ao wa mtu wa nne ni kama mwana wa miungu.”
Mfalme akasema, “Tazama! Naona watu wanne wakitembeatembea ndani ya moto, hawajafungwa wala kudhurika, naye mtu yule wa nne anaonekana kama mwana wa miungu.”
26 Ndipo Nebukadneza aliposogea karibu na mlango wa tanuru liwakalo moto na akaaita, “Shadraka, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu, tokeni nje! Njooni hapa! Ndipo Shadraka, Meshaki na Abednego walitoka nje ya moto.
Ndipo Nebukadneza akaukaribia mdomo wa ile tanuru iwakayo moto na kupaza sauti, “Shadraki, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu Sana, tokeni! Njooni hapa!” Ndipo Shadraki, Meshaki na Abednego wakatoka ndani ya moto.
27 Magavana wa majimbo, magavana wengine, na washauri wa mfalme waliokuwa wamekusanyika kwa pamoja waliwaona watu hawa. Moto haukuunguza miili yao; nywele katika vichwa vyao hazikuungua; mavazi yao yalikuwa hayajaharibiwa; na hawakuwa na harufu ya moto.
Nao maliwali, wasimamizi, watawala na washauri wa mfalme wakakusanyika kuwazunguka. Waliona kwamba moto haukudhuru miili yao, wala unywele wa vichwa vyao haukuungua, majoho yao hayakuungua, wala hapakuwepo na harufu ya moto kwenye miili yao.
28 Nebukadneza alisema, “Na tumsifu Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abedinego, ambaye amemtuma mjumbe wake na amewapa ujumbe watumishi wake. Walimtumaini yeye wakati walipoikana amri yangu, na waliitoa miili yao badala ya kuabudu au kusujudia mungu mwingine isipokuwa Mungu wao.
Ndipo Nebukadneza akasema, “Ahimidiwe Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego, ambaye amemtuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake. Walimtumaini na kukaidi amri ya mfalme, nao wakawa tayari kufa kuliko kutumikia au kuabudu mungu mwingine yeyote isipokuwa Mungu wao.
29 Hivyo basi ninaagiza kwamba watu wote, taifa au lugha ambayo itazungumza kitu chochote kinyume na Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abedinego lazima wakatwe vipande, na ya kwamba nyumba zao lazima zifanywe kuwa vichuguu vya uchafu kwasababu hakuna mungu mwingine anayeweza kuokoa kama hivi.”
Kwa hiyo ninaamuru kwamba watu wa taifa lolote au lugha yoyote watakaosema kitu chochote dhidi ya Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego wakatwe vipande vipande na nyumba zao zifanywe kuwa malundo ya kokoto, kwa maana hakuna mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.”
30 Ndipo mfalme aliwapandisha cheo Shadraka, Meshaki na Abednego katika jimbo la Babeli.
Kisha mfalme akawapandisha vyeo Shadraki, Meshaki na Abednego katika jimbo la Babeli.