< Wakolosai 4 >
1 Mabwana, toeni kwa watumwa mambo yaliyo haki na ya adili. Mnajua pia kwamba mnaye Bwana mbinguni.
2 Endeleeni kuwa thabiti katika maombi. Kaeni macho katika hilo kwa shukrani.
3 Ombeni pamoja kwa ajili yetu pia, ili kwamba Mungu afungue mlango kwa ajili ya neno, kunena siri ya ukweli ya Kristo. Kwa sababu ya hili nimefungwa minyororo.
4 Na ombeni kwamba niweze kuliweka wazi, kama inavyonipasa kusema.
5 Enenda kwa hekima kwa wale walioko nje, na muukomboe wakati.
6 Maneno yenu na yawe na neema wakati wote, na yakolee chumvi majira yote, ili kwamba mweze kujua jinsi inavyowapasa kumjibu kila mtu.
7 Kwa mambo yanayonihusu mimi, Tikiko atayafanya yajulikane kwenu. Yeye ni ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, na mtumwa mwenzetu katika Bwana.
8 Namtuma kwenu kwa ajili ya hili, kwamba mweze kujua mambo kuhusu sisi na pia kwamba aweze kuwatia moyo.
9 Namtuma pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpendwa mwaminifu, na mmoja wenu. Watawaambia kila kitu kilichotokea hapa.
10 Aristarko, mfungwa mwenzangu, anawasalimu, pia na Marko binamu yake na Barnaba mliyepokea utaratibu kutoka kwake, “kama akija kwenu, mpokeeni,”
11 Na pia Yesu aitwaye Yusto. Hawa peke yao wa tohara ni watendakazi wenzangu kwa jili ya ufalme wa Mungu. Wamekuwa ni faraja kwangu.
12 Epafra anawasalimu. Yeye ni mmoja wenu na mtumwa wa Kristo Yesu. Yeye hufanya bidii katika maombi kwa ajili, ili kwamba mweze kusimama kwa ukamilifu na kuhakishwa kikamilifu katika mapenzi yote ya Mungu.
13 Kwa kuwa ninamshuhudia, kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa hao walioko Laodekia, na kwa hao walioko Hierapoli.
14 Luka yule tabibu mpendwa, na Dema wanawasalimu.
15 Wasalimu ndugu zangu walioko Laodekia, na Nimfa, na kanisa lile lililoko nyumbani kwake.
16 Barua hii itakapokuwa imesomwa miongoni mwenu, isomwe pia kwa kanisa la walaodekia, nanyi pia hakikisheni mnaisoma ile barua kutoka Laodekia.
17 Sema kwa Arkipo, ''Angalia ile huduma ambayo umeipokea katika Bwana, kwamba unapaswa kuitimiza.”
18 Salamu hii ni kwa mkono wangu mwenyewe - Paulo. Ikuumbukeni minyororo yangu. Neema na iwe nanyi.