< Amosi 8 >
1 Hiki ndicho ambacho bwana Yahwe amenionyesha. Tazama, kikapu cha matunda ya hari!
Hili ndilo alilonionyesha Bwana Mwenyezi katika maono: kikapu cha matunda yaliyoiva.
2 Akasema, “Unaona nini, Amosi?” Nikasema, “Kikapu cha matunda ya hari.” Kisha Yahwe akanambia, “Mwisho umefika kwa watu wangu Israeli; sintowaumiza tena.
Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?” Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.” Ndipo Bwana akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli; sitawahurumia zaidi.”
3 Nyimbo za kwenye hekalu zitakuwa vilio. Katika siku hiyo-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe. Mizoga itakuwa mingi, katika kila sehemu wataitupa katika ukimya!”
Bwana Mwenyezi asema, “Katika siku ile, nyimbo katika Hekalu zitageuka kuwa maombolezo. Miili mingi, mingi sana: itatupwa kila mahali! Kimya!”
4 Lisikilizeni hili, ninyi mkanyagao maskini na kumuondoa fukara wa nchi.
Lisikieni hili, ninyi ambao mnawagandamiza wahitaji, na kuwaonea maskini wa nchi,
5 wakisema, “Wakati mwezi mpya utakapoisha, hivyo tunaweza kuuza mazao tena? Wakati siku ya Sabato itakapoisha, ili kwamba tuuze ngano? Tutafanya kipimo kidogo na kuongeza bei, tukidanganya kwa mizani za udanganyifu.
mkisema, “Ni lini Mwezi Mwandamo utakapopita ili tupate kuuza nafaka, na Sabato itakwisha lini ili tuweze kuuza ngano?” Mkipunguza vipimo, na kuongeza bei, na kudanganya kwa mizani zisizo sawa,
6 Hivi ndivyo ambavyo tunaweza kuuza ngano mbaya, kununua fukara kwa fedha, na masikini kwa jozi moja ya kubadhi.”
mkiwanunua maskini kwa fedha, na wahitaji kwa jozi ya viatu, na mkiuza hata takataka za ngano pamoja na ngano.
7 Yahwe ameapa kwa fahari ya Yakobo, “Hakika sintoweza kusahau kazi zao hata moja.”
Bwana ameapa kwake mwenyewe, aliye Kiburi cha Yakobo: “Kamwe sitasahau chochote ambacho wamefanya.
8 Je nchi haitatetemeka kwa hili, na kila mmoja aishiye kuombolezea? Yote hayo yatainuka kama Mto Naili, nayo itataabika juu na kupwa tena, kama mto wa Misri.
“Je, nchi haitatetemeka kwa ajili ya hili, nao wote waishio ndani mwake hawataomboleza? Nchi yote itainuka kama Naili; itapanda na kushuka kama mto wa Misri.
9 “Itakuja siku ambayo -huu ndio usemi wa Bwana Yahwe- kwamba nitafanya jua litue wakati wa mchana, na nitaiweka giza dunia wakati wa mchana.
“Katika siku ile,” asema Bwana Mwenyezi, “Nitalifanya jua litue alasiri na kuifanya dunia iwe giza wakati wa mchana mwangavu.
10 Nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo na nyimbo zenu zote kuwa masikitiko. Nitawafanya wote kuvaa nguo za magunia na kipara juu ya kila kichwa. Nitayafanya haya kama maombolezo kwa mwana pekee, na siku ya uchungu mwisho wake.
Nitageuza sikukuu zenu za kidini kuwa maombolezo, na kuimba kwenu kote kuwe kilio. Nitawafanya ninyi nyote mvae nguo ya gunia na kunyoa nywele zenu. Nitaufanya wakati ule uwe kama wa kuombolezea mwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.
11 Tazama, siku zinakuja -asema Bwana Yahwe- wakati nitakapoleta njaa katika nchi, sio njaa ya mkate, wala kiu ya maji, ila kusikia maneno ya Yahwe.
“Siku zinakuja,” asema Bwana Mwenyezi, “wakati nitakapotuma njaa katika nchi yote: si njaa ya chakula wala kiu ya maji, lakini njaa ya kusikia maneno ya Bwana.
12 watatangatanga kutoka bahari hata bahari; watakimbia kutoka kaskazini kwenda magharibi kutafuta neno la Yahwe, lakini hawatalipata.
Wanaume watayumbayumba kutoka bahari hadi bahari na kutangatanga kutoka kaskazini mpaka mashariki, wakitafuta neno la Bwana, lakini hawatalipata.
13 Katika siku hiyo wanawali wazuri na wavulana watazimia kutokana na njaa.
“Katika siku ile “wasichana wazuri na vijana wanaume wenye nguvu watazimia kwa sababu ya kiu.
14 Wale waapao kwa dhambi ya Samaria wataanguka na hawatainuka tena.”
Wale waapao kwa aibu ya Samaria, au kusema, ‘Hakika kama miungu yenu iishivyo, ee Dani,’ au ‘Hakika kama mungu wa Beer-Sheba aishivyo’: wataanguka, wala hawatasimama tena.”