< Matendo 6 >
1 Sasa katika siku hizi, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa inaongezeka, lalamiko la Wayahudi wa Kiyunani lilianza dhidi ya Waebrania, kwa sababu wajane wao walikuwa wanasahaulika katika mgao wa kila siku wa chakula.
In diebus illis, crescente numero discipulorum, factum est murmur Graecorum adversus Hebraeos, eo quod despicerentur in ministerio quotidiano viduae eorum.
2 Mitume kumi na wawili waliwaita kusanyiko lote la wanafunzi na kusema, “Siyo sahihi kwetu kuliacha neno la Mungu na kuhudumia mezani.
Convocantes autem duodecim multitudinem discipulorum dixerunt: Non est aequum nos derelinquere verbum Dei, et ministrare mensis.
3 Kwa hiyo, ndugu, chagueni, wanaume saba, kutoka miongoni mwenu, watu wema, waliojaa Roho na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi huduma hii.
Considerate ergo fratres, viros ex vobis boni testimonii septem, plenos Spiritu sancto, et sapientia, quos constituamus super hoc opus.
4 Na sisi, tutaendelea daima katika kuomba na katika huduma ya neno.”
Nos vero orationi, et ministerio verbi instantes erimus.
5 Hotuba yao ikaupendeza mkutano wote. Hivyo, wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, Prokoro, Nikanori, Timoni, Parmena, na Nikolao, mwongofu kutoka Antiokia.
Et placuit sermo coram omni multitudine. Et elegerunt Stephanum, virum plenum fide, et Spiritu sancto, et Philippum, et Prochorum, et Nicanorem, et Timonem, et Parmenam, et Nicolaum advenam Antiochenum.
6 Waumini waliwaleta watu hawa mbele ya mitume, walioomba na badaye wakawawekea mikono yao.
Hos statuerunt ante conspectum Apostolorum: et orantes imposuerunt eis manus.
7 Hivyo, neno la Mungu lilienea; na idadi ya wanafunzi ilizidi kuongezeka huko Yesrusalem; na idadi kubwa ya makuhani wakaitii imani.
Et verbum Domini crescebat, et multiplicabatur numerus discipulorum in Ierusalem valde: multa etiam turba sacerdotum obediebat fidei.
8 Na Stefano, aliyejaa neema na nguvu, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa miongoni mwa watu.
Stephanus autem plenus gratia, et fortitudine faciebat prodigia, et signa magna in populo.
9 Lakini hapo wakainuka baadhi ya watu wafuasi wa Sinagogi liitwalo Sinagogi la Mahuru, na la Wakirene na la Waeskanderia, na baadhi kutoka Kilikia na Asia. Watu hawa walikuwa wakihojiana na Stefano.
Surrexerunt autem quidam de synagoga, quae appellatur Libertinorum, et Cyrenensium, et Alexandrinorum, et eorum qui erant a Cilicia, et Asia, disputantes cum Stephano:
10 Lakini, hawakuweza kushindana na hekima na Roho ambayo Stefano alikuwa akitumia katika kuzungumza.
et non poterant resistere sapientiae, et Spiritui, qui loquebatur.
11 Kisha waliwashawishi baadhi ya watu kwa siri kusema, “Tumesikia Stefano akizungumza maneno ya kufuru dhidi ya Musa na dhidi ya Mungu.”
Tunc summiserunt viros, qui dicerent se audivisse eum dicentem verba blasphemiae in Moysen, et in Deum.
12 Waliwashurutisha watu, wazee, na waandishi, na kumwendea Stefano, wakamkamata, na kumleta mbele ya baraza.
Commoverunt itaque plebem, et seniores, et Scribas: et concurrentes rapuerunt eum, et adduxerunt in concilium,
13 waliwaleta mashahidi wa uongo, waliosema, “mtu huyu haachi kunena maneno mabaya dhidi ya eneo hili takatifu na sheria.
et statuerunt falsos testes, qui dicerent: Homo iste non cessat loqui verba adversus locum sanctum, et legem.
14 Kwani tumemsikia akisema kwamba huyu Yesu wa Nazareti atapaharibu mahali hapa na kuzibadili desturi tulizokabidhiwa na Musa.”
audivimus enim eum dicentem: quoniam Iesus Nazarenus hic, destruet locum istum, et mutabit traditiones, quas tradidit nobis Moyses.
15 Kila mmoja aliyekuwa katika baraza, akaelekeza macho yake kumwangalia Stefano, nao wakauona uso wake ulikuwa kama uso wa malaika.
Et intuentes eum omnes, qui sedebant in concilio, viderunt faciem eius tanquam faciem Angeli.