< Matendo 3 >

1 Sasa Peter na Yohana walikuwa wanaelekea katika hekalu wakati wa maombi, saa tisa.
Petar i Ivan uzlazili su u Hram na devetu molitvenu uru.
2 Mtu fulani, kiwete tangu kuzaliwa, alikuwa akibebwa kila siku na alikuwa akilazwa katika mlango wa hekalu uitwao mzuri, ili aweze kuomba sadaka kutoka kwa watu waliokuwa wakielekea hekaluni.
Upravo su donosili nekog čovjeka, hroma od majčine utrobe; njega bi svaki dan postavljali kod hramskih vrata, zvanih Divna, da prosi milostinju od onih koji ulaze u Hram.
3 Alipowaona Petro na Yohana wanakaribia kuingia hekaluni, aliomba sadaka.
On ugleda Petra i Ivana upravo kad zakoračiše u Hram te zamoli milostinju.
4 Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, alisema,”tutazame sisi.”
Petar ga zajedno s Ivanom prodorno pogleda i reče: “Pogledaj u nas!”
5 Kiwete akawatazama, akitazamia kupokea kitu fulani kutoka kwao.
Dok ih je molećivo motrio očekujući od njih nešto dobiti,
6 Lakini Petro akasema, “fedha na dhahabu mimi sina, lakini kile nilichonacho nitatoa kwako. Katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth, tembea.”
reče mu Petar: “Srebra i zlata nema u mene, ali što imam - to ti dajem: u ime Isusa Krista Nazarećanina hodaj!”
7 Petro akamchukua kwa mkono wake wa kulia, na akamwinua juu: mara moja miguu yake na vifundo vya mifupa yake vikapata nguvu.
I uhvativši ga za desnu ruku, pridiže ga: umah mu omoćaše noge i gležnjevi
8 Akiruka juu, mtu kiwete alisimama na akaanza kutembea; akaingia hekaluni pamoja na Petro na Yohana, akitembea, akiruka, na kumsifu Mungu.
pa skoči, uspravi se, stane hodati te uđe s njima u Hram hodajući, poskakujući i hvaleći Boga.
9 Watu wote walimwona akitembea na akimsifu Mungu.
Sav ga narod vidje kako hoda i hvali Boga.
10 Wakatambua kwamba alikuwa ni yule mtu ambaye alikuwa akikaa akiomba sadaka kwenye mlango mzuri wa hekalu; walijawa na mshangao na kustaajabu kwa sababu ya kile kilichotokea kwake.
Razabraše da je to on - onaj koji je na Divnim vratima Hrama prosio milostinju - i ostadoše zapanjeni i izvan sebe zbog onoga što se s njim dogodilo.
11 Namna alivyokuwa amewashikilia Petro na Yohana, watu wote kwa pamoja wakakimbilia kwenye ukumbi uitwao wa Sulemani, wakishangaa sana.
Kako se pak on držao Petra i Ivana, sav se narod zapanjen strča k njima u trijem zvani Salomonov.
12 Petro alipoliona hili, yeye akawajibu watu, “Enyi watu wa Israel, kwa nini mnashangaa? Kwa nini mnayaelekeza macho yenu kwetu, kama kwamba tumemfanya huyu atembee kwa nguvu zetu wenyewe au uchaji wetu?”
Kada to vidje Petar, obrati se narodu: “Izraelci, što se ovomu čudite? Ili što nas gledate kao da smo svojom snagom ili pobožnošću postigli da ovaj prohoda?
13 Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Yakobo, Mungu wa Baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu. Huyu ndiye ambaye ninyi mlimkabidhi na kumkataa mbele ya uso wa Pilato, japo yeye alikuwa ameamua kumwachia huru.
Bog Abrahamov, Izakov i Jakovljev, Bog otaca naših, proslavi slugu svoga, Isusa kojega vi predadoste i kojega se odrekoste pred Pilatom kad već bijaše odlučio pustiti ga.
14 Mlimkataa Mtakatifu na Mwenye Haki, na badala yake mkataka muuaji aachwe huru.
Vi se odrekoste Sveca i Pravednika, a izmoliste da vam se daruje ubojica.
15 Ninyi mlimuua Mfalme wa uzima, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu - Sisi ni mashahidi wa hili.
Začetnika života ubiste. Ali Bog ga uskrisi od mrtvih, čemu smo mi svjedoci.”
16 Sasa, kwa imani katika jina lake, mtu huyu ambaye mnamwona na kujua, alifanywa kuwa na nguvu. Imani ambayo inapitia kwa Yesu imempa yeye afya hii kamilifu, mbele yenu ninyi nyote.
“I po vjeri u njegovo ime, to je ime dalo snagu ovomu kojega gledate i poznate: vjera u Njega vratila je ovomu potpuno zdravlje naočigled vas sviju.”
17 Sasa, Ndugu, najua kwamba mlitenda katika ujinga, ndivyo pia walivyofanya viongozi wenu.
“I sada, braćo, znam da ste ono uradili iz neznanja kao i glavari vaši.
18 Lakini mambo ambayo Mungu aliwaambia mapema kwa vinywa vya manabii wote, kwamba huyu Kristo atateseka, sasa ameyatimiza.
Ali Bog tako ispuni što unaprijed navijesti po ustima svih proroka: da će njegov Pomazanik trpjeti.
19 Kwa hiyo, tubuni na mgeuke, ili kwamba dhambi zenu ziweze kuondolewa kabisa, kusudi zije nyakati za kuburudika kutokana na uwepo wa Bwana;
Pokajte se dakle i obratite da se izbrišu grijesi vaši
20 na kwamba aweze kumtuma Kristo ambaye ameshateuliwa kwa ajili yenu, Yesu.
pa od Gospodina dođu vremena rashlade te on pošalje vama unaprijed namijenjenog Pomazanika, Isusa.”
21 Yeye ndiye ambaye lazima mbingu zimpokee mpaka wakati wa kurejeshwa kwa vitu vyote, ambavyo Mungu alizungumzia zamani za kale kwa vinywa vya manabii watakatifu. (aiōn g165)
Njega treba da nebo pridrži do vremena uspostave svega što obeća Bog na usta svetih proroka svojih odvijeka.” (aiōn g165)
22 Hakika Musa alisema, 'Bwana Mungu atainua nabii kama mimi kutoka katika ndugu zenu. Mtamsikiliza kila kitu ambacho atawaambia ninyi.
“Mojsije tako reče: Proroka poput mene od vaše braće podignut će vam Gospodin, Bog vaš. Njega slušajte u svemu što vam god reče.
23 Itatokea kwamba kila mtu ambaye hasikilizi kwa nabii huyo ataangamizwa kabisa atoke kati ya watu.'
I svaka duša koja ne posluša toga proroka, neka se iskorijeni iz naroda.”
24 Ndiyo, na manabii wote tokea Samweli na wale waliofuata baada yake, walizungumza na walitangaza siku hizi.
“I svi Proroci koji su - od Samuela dalje - govorili, također su navijestili ove dane.”
25 Ninyi ni wana wa manabii na wa agano ambalo Mungu alilifanya pamoja na mababu, kama alivyosema kwa Abrahamu, 'Katika mbegu yako familia zote za dunia zitabarikiwa.'
“Vi ste sinovi proroka i Saveza koji sklopi Bog s ocima vašim govoreći Abrahamu: Potomstvom će se tvojim blagoslivljati sva plemena zemlje.
26 Baada ya Mungu kumwinua mtumishi wake, alimtuma kwenu kwanza, ili awabariki ninyi kwa kugeuka kutoka katika uovu wenu.”
Vama najprije podiže Bog Slugu svoga i posla ga blagoslivljati vas da se svatko obrati od opačina svojih.”

< Matendo 3 >