< Matendo 25 >

1 Ndipo Festo alipoingia katika jimbo hilo na baada ya siku tatu alienda toka Kaisaria hadi Yerusalemu.
Ndipo Festo ajhingili mu lijimbo elu ni baada jha magono madatu akalota kuhoma Kaisaria hadi Yerusalemu.
2 Kuhani mkuu na Wayahudi mashuhuri walileta shutuma dhidi ya Paulo kwa Festo, na walizungumza kwa nguvu kwa Festo.
Kuhani mbaha ni bhayahudi mashuhuri bhaletili shutuma dhidi jha Paulo kwa Festo, na bhalongili kwa nghofu kwa Festo.
3 Na walimwomba Festo fadhili juu ya habari za Paulo apate kumwita Yerusalemu ili waweze kumwua njiani.
Na bhan'sokili Festo fadhili juu jha habari sya Paulo abhwesiajhi kunkuta Yerusalemu ili bhabhwesiajhi kun'koma munjela.
4 Lakini Festo alijibu kwamba Paulo alikuwa mfungwa katika Kaisaria, na kwamba yeye mwenyewe atarudi huko haraka.
Lakini Festo ajibili kujha Paulo ajhele mfungwa mu Kaisaria, ni kwamba muene ikerebhuka okhu manyata.
5 Alisema “Kwa hiyo, wale ambao wanaweza, wanaweza kwenda huko na sisi. Kama kuna kitu kibaya kwa mtu huyu, mnapaswa kumshtaki.”
Ajobhili “Kwa hiyo, bhala ambabho bhibhwesya kulota okhu ni tete. Kama kujhe ni khenu kibaya kwa munu ojho, mwilondeka kun'shtaki.”
6 Baada ya kukaa siku nane au kumi zaidi, akarudi Kaisaria. Na siku iliyofuata akakaa katika kiti cha hukumu na kuamuru Paulo aletwe kwake.
Baada jha kutama magono nane au kumi zaidi, akakerebhuka Kaisaria. Na ligono lyalafuatili atamili pa kiti kya hukumu ni kuamuru Paulo aletibhwayi kwa muene.
7 Alipofika, Wayahudi kutoka Yerusalemu wakasimama karibu, Wakatoa mashtaka mengi mazito ambayo hawakuweza kuyathibitisha.
Bho afikili, Bhayahudi kuhoma Yerusalemu bhajhemi karibu, bhakapisya mashtaka mazito ambajho bhabhwesilepi kughathibitisha.
8 Paulo alijitetea na kusema, 'Si dhidi ya jina la Wayahudi, si juu ya hekalu, na si juu ya Kaisari, nimefanya mabaya.'
Paulo akitetili ni kujobha, sio dhidi jha lihina lya bhayahudi, sio panani pa hekalu, na sio panani pa Kaisaria, nibhombi mabaya.'
9 Lakini Festo alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, na hivyo akamjibu Paulo kwa kusema, 'Je, unataka kwenda Yerusalemu na kuhukumiwa na mimi kuhusu mambo haya huko?'
Lakini Festo alondeghe kwipendekesya kwa bhayahudi, efyo akan'jibu Paulo ni kujobha, 'Je, wilonda kulota Yerusalemu ni kuhukumulibhwa ni nene kuhusu mambo agha okhu?'
10 Paulo alisema, 'ninasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari ambapo napaswa kuhukumiwa. Sijawakosea Wayahudi, kama wewe ujuavyo vema.
Paulo ajobhili, 'nijhemili mbele jha kiti kya hukumu kya Kaisari ambapo nilondeka kuhukumulibhwa. Nibhakosilepi bhayahudi, kama kya umanyi bhebhe.
11 Ikiwa nimekosa na kama nimefanya kinachostahili kifo, sikatai kufa. Lakini kama shutuma zao si kitu, hakuna mtu anaweza kunikabidhi kwao. Ninamwomba Kaisari. '
Nikajhiajhi nikosili na kama nibhombi kyakilondeka kifo, nibelepi kufwa. Lakini kama shutuma sya bhene khenu lepi, ajhelepi munu jhaibhwesya kunikabidhi kwa bhene. Nikansoka Kaisari. '
12 Baada ya Festo kuongea na baraza akajibu, “unamwomba Kaisari; utaenda kwa Kaisari.”
Baada jha Festo kulongela ni baraza akajibu, “Ukan'soka Kaisari; wibetalota kwa Kaisari.”
13 Baada ya siku kadhaa, mfalme Agripa na Bernike walifika Kaisaria kufanya ziara rasmi kwa Festo.
Baada jha magono kadhaa, mfalme Agripa ni Bernike bhafikili Kaisaria kubhomba ziara rasmi kwa Festo.
14 Baada ya kukaa hapo kwa siku nyingi, Festo aliwasilisha kesi ya Paulo kwa mfalme; Akasema, 'Mtu mmoja aliachwa hapa na Feliki kama mfungwa.
Baada jha kutamaapu kwa magono mingi, Festo awasilishi kesi jha Paulo kwa mfalme; Akajobha, 'Munu mmonga alekibhu apa ni Feliki kama mfungwa.
15 Nilipokuwa Yerusalemu makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi walileta mashtaka juu ya mtu huyu kwangu, nao waliuliza juu ya hukumu dhidi yake.
Bho nijhe Yerusalemu makuhani bhabhaha ni bhaseya bha bhayahudi bhaletili mashtaka juu jha munu ojho kwa nene na bhene bhakotili juu jha hukumu dhidi jha muene.
16 Kwa hili mimi niliwajibu kwamba si desturi ya Waroma kumtoa mtu kwa upendeleo badala yake, mtuhumiwa anapaswa kuwa na nafasi ya kuwakabili washitaki wake na kujitetea dhidi ya tuhuma hizo.
Kwa e'le nene nabhajibili kujha desturi jha Bharoma lepi kumpisya munu upendeleo badala jhiake, mtuhumibhwa ilondeka kujha ni nafasi jha kubhakabili bhashtaki bha muene ni kwitetela dhidi jha tuhuma e'su.
17 Kwa hiyo, walipokuja pamoja hapa, sikuweza kusubiri, lakini siku iliyofuata niliketi katika kiti cha hukumu na kuamuru mtu huyo aletwe ndani.
Kwa hiyo, bhobhahidili pamonga apa, nabhwesilepi kulendela, lakini ligono lya lyafwatili natamili pakiti kya hukumu ni kuamuru munu ojho aletibhwayi mugati.
18 Wakati washitaki waliposimama na kumshtaki, nilifikiri kwamba hakuna mashtaka makubwa yaliyoletwa dhidi yake.
Wakati bhashtaki bhajhemili ni kun'shtaki, nifikirileghe kujha ghajhelepi mashtaka mabaha ghaghaletibhu dhidi jha muene.
19 Badala yake, walikuwa na mabishano fulani pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu Yesu ambaye alikuwa amekufa, lakini Paulo anadai kuwa yu hai.
Badala jhiake, bhajhele ni mabishano fulani pamonga ni muene kuhusu dini jha bhene ni kuhusu Yesu ambajhe afuili, lakini Paulo idai kuwa ajhe muomi.
20 Nilikuwa nimefumbwa jinsi ya kuchunguza suala hili, na nikamwuliza kama angeenda Yerusalemu kuhukumiwa kuhusu mambo haya.
Nafumbibhu jinsi jha kuchungusya lisuala e'le, na nan'kotili kama ngaalotili Yerusalemu kuhukumibhwa kuhusu mambo agha.
21 Lakini Paulo alipoitwa awekwe chini ya ulinzi kwa ajili ya uamuzi wa Mfalme, niliamuru awekwe hata nitakapompeleka kwa Kaisari. '
Lakini Paulo bho akutibhu abhekibhwayi chini jha ulinzi kwandabha jha uamuzi bhwa Mfalme, naamuiri abhekibhwayi hata panibeta kumpeleka kwa Kaisari.'
22 Agripa alizungumza na Festo, “ningependa pia kumsikiliza mtu huyu.” “Festo, akasema, “kesho utamsikiliza.”
Agripa alongilili ni Festo, “Nilondeghe kabhele kumpelekesya munu ojho.” “Festo, akajobha, “kilabhu wibeta kumpelekesya.”
23 Hivyo kesho yake, Agripa na Bernike walifika na sherehe nyingi; walifika katika ukumbi na maafisa wa kijeshi, na watu mashuhuri wa mji. Na Festo alipotoa amri, Paulo aliletwa kwao.
Hivyo kilabhu jhiake, Agripa ni Bernike bhafikili ni sherehe simehele; bhafikili pa ukumbi ni maafisa bha kijeshi, ni bhanu mashuhuri bha mji. Ni Festo bho apisili amri, Paulo aletibhu kwa bhene.
24 Festo akasema, “Mfalme Agripa, na watu wote ambao wapo hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu; jumuiya yote ya Wayahudi huko Yerusalemu na hapa pia wametaka niwashauri, na wao wakapiga kelele kwangu kwamba asiishi.
Festo akajobha, “Mfalme Agripa, ni bhanu bhoha ambabho bhabhajhele apa pamonga natu, mukambona munu ojho; Jumuiya jhioha jha bhayahudi okhu Yerusalemu ni apa kabhele bhilonda nibhashauriajhi, ni bhene bhakapiga kelele kwa nene kwamba asitami.
25 Naliona kwamba hakufanya lolote linalostahili kifo; lakini kwa sababu amemwita Mfalme, niliamua kumpeleka kwake.
Nibhona kujha abhombilepi lyalilondeka kufwa; Lakini kwandabha an'kutili Mfalme, naamuili nimpelekayi kwa muene.
26 Lakini sina kitu dhahiri cha kuandika kwa Mfalme. Kwa sababu hii, nimemleta kwako, hasa kwako wewe, Mfalme Agripa, ili nipate kuwa na kitu cha kuandika kuhusu kesi.
Lakini nijhelepi ni khenu dhahiri kya kulemba kwa Mfalme. Kwandabha ejhe, nindetili kwa bhebhe, hasa kwa bhebhe, Mfalme Agripa, ili nibhwesiajhi kujha ni khenu kya kulemba kuhusu kesi.
27 kwa kuwa naona haina maana kumpeleka mfungwa na bila kuonyesha mashitaka yanayomkabili.
Kwa kujha nibhona ijhelepi ni maana kumpeleka mfungwa ni bila kulasya mashtaka ghaghakan'kabili.

< Matendo 25 >