< Matendo 20 >
1 Baada ya ghasia kumalizika, Paulo aliwaita wanafunzi na kuwatia moyo. Kisha kuwaaga na akaondoka kwenda Makedonia.
2 Naye akiishakupita mikoa hiyo na alikuwa akiwatia moyo waamuni, akaingia Uyunani.
3 Baada ya yeye kuwa pale kwa muda wa miezi mitatu, njama ziliundwa dhidi yake na Wayahudi alipokuwa akikaribia kusafiri kwa njia ya bahari kuelekea Shamu, hivyo aliazimu kurudi kupitia Makedonia.
4 Walioandamana naye hadi Asia walikuwa Sopatro, mwana wa Pirho kutoka Berea; Aristariko na Sekundo, wote kutoka waamini wa Wathesalonike; Gayo wa Derbe; Timotheo; Tikiko na Trofimo kutoka Asia.
5 Lakini watu hawa wamekwisha tangulia na walikuwa wanatungojea kule Troa.
6 kwa njia ya Bahari kutoka Filipi baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, na katika siku tano tukawafikia huko Troa. Tulikaa huko kwa siku saba.
7 Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekusanyika pamoja ili kuumega mkate, Paulo alizungumza na Waamini. Alikuwa akipanga kuondoka kesho yake, hivyo akaendelea kuongea hadi usiku wa manane.
8 Kulikuwa na taa nyingi katika chumba cha juu ambapo tulikuwa tumekusanyika pamoja.
9 Katika dirisha alikuwa amekaa kijana mmoja jina lake Utiko, ambaye alielemewa na usingizi mzito. Hata Paulo alipokuwa akihutubu kwa muda mrefu, kijana huyu, akiwa amelala, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu na aliokotwa akiwa amekufa.
10 Lakini Paulo alishuka chini, alijinyoosha yeye mwenyewe juu yake, akamkumbatia. Kisha akasema, “Msikate tamaa, kwa kuwa yu hai.”
11 Kisha akapanda tena ghorofani na akaumega mkate, akala. Baada ya kuzungumza nao kwa muda mrefu hadi alfajiri, akaondoka.
12 Wakamleta yule kijana akiwa hai wakafarijika sana.
13 Sisi wenyewe tulitangulia mbele ya Paul kwa meli na tukaelekea Aso, ambapo sisi tulipanga kumchukua Paul huko. Hiki ndicho yeye mwenyewe alitaka kufanya, kwa sababu alipanga kwenda kupitia nchi kavu.
14 Alipotufikia huko Aso, tukampakia kwenye Meli tukaenda Mitilene.
15 Kisha sisi tukatweka kutoka huko na siku ya pili tulifika upande wa pili wa kisiwa cha Kio. Siku iliyofuata, tukawasili kisiwa cha Samo, na kesho yake tukafika mji wa Mileto.
16 Kwa sababu Paulo alikuwa ameamua kusafiri kupitia Efeso, ili kwamba asitumie muda wowote katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka ya kuwahi Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu ya Pentekoste, kama ingeliwezekana yeye kufanya hivyo.
17 Kutoka Mileto akatuma watu hadi Efeso na akawaita wazee wa Kanisa.
18 Walipofika kwake, akawaambia, ninyi wenyewe mwajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu muda wote.
19 Nimemtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote na kwa machozi, na mateso yaliyonipata mimi kwa hila za Wayahudi.
20 Mwajua jinsi ambavyo sikujizuia kutangaza kwenu kitu chochote ambacho kilikuwa muhimu, na jinsi mimi nilivyowafundisha wazi wazi na pia kwenda nyumba kwa nyumba.
21 Mnajua jinsi mimi nilivyoendelea kuwaonya Wayahudi na Wayunani juu ya toba kwa Mungu na imani katika Bwana wetu Yesu.
22 Na sasa, angalieni, mimi, nikiwa ninamtii Roho Mtakatifu kuelekea Yerusalemu, nisiyajue mambo ambayo yatanitokea mimi huko,
23 ila kwa kuwa Roho Mtakatifu hunishuhudia mimi katika kila mji na anasema kwamba minyororo na mateso ndivyo vinavyoningojea.
24 Lakini mimi si kufikiria kwamba maisha yangu ni kwa njia yoyote ya thamani kwangu, ili niweze kumaliza mwendo wangu na huduma niliyopokea kutoka kwa Bwana Yesu, kuishuhudia injili ya neema ya Mungu.
25 Na sasa, tazama, najua kwamba wote, miongoni mwa wale nilioenda kuwahubiri Ufalme, hamtaniona uso tena.
26 Kwa hiyo nawashuhudia leo hii, kwamba sina hatia kwa damu ya mtu yeyote.
27 Kwa maana sikujizuia kuwatangazia mapenzi yote ya Mungu.
28 Kwa hiyo iweni waangalifu juu yenu ninyi wenyewe, na juu ya kundi lolote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi. Iweni waangalifu kulichunga kusanyiko la Bwana, ambalo alilinunua kwa damu yake mwenyewe.
29 Najua kwamba baada ya kuondoka kwangu, mbwa mwitu wakali wataingia kwenu, na wasilihurumie kundi.
30 Najua kwamba hata miongoni mwenu wenyewe baadhi ya watu watakuja na kusema mambo mapotovu, ili kuwavuta wanafunzi wawafuate wao.
31 Kwa hiyo muwe macho. Kumbukeni kwamba kwa miaka mitatu sikuweza kuacha kuwafundisha kila mmoja wenu kwa machozi usiku na mchana.
32 Na sasa mimi nawakabidhi kwa Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliowekwa wakfu kwa Mungu.
33 Sikutamani fedha, dhahabu, au mavazi.
34 Mnajua ninyi wenyewe kwamba mikono hii imenipatia mahitaji yangu mwenyewe na mahitaji ya wale waliokuwa pamoja nami.
35 Katika mambo yote niliwapa mfano wa jinsi inavyopasa kuwasaidia wanyonge kwa kufanya kazi, na jinsi mnavyopaswa kukumbuka maneno ya Bwana Yesu, maneno ambayo yeye mwenyewe alisema: “Ni heri kutoa kuliko kupokea.”
36 Baada ya kusema namna hii, alipiga magoti akaomba pamoja nao.
37 Wote wakalia sana na kumwangukia Paulo shingoni na kumbusu.
38 Walihuzunika zaidi ya yote kwa sababu ya kile ambacho alikuwa amesema, kwamba kamwe hawatauona uso wake tena. Kisha wakamsindikiza merikebuni.