< 3 Yohana 1 >
1 Mzee, kwa Gayo mpenzi, ninayempenda katika kweli.
Senior Gaio charissimo, quem ego diligo in veritate.
2 Mpendwa, nakuombea ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema, kama vile roho yako inavyofanikiwa.
Charissime, de omnibus orationem facio prospere te ingredi, et valere, sicut prospere agit anima tua.
3 Maana nilifurahi sana wakati nilipoambiwa na ndugu waliokuja na kutoa ushuhuda juu ya kweli yako, kama vile unavyoenenda katika kweli.
Gavisus sum valde venientibus fratribus, et testimonium perhibentibus veritati tuae, sicut tu in veritate ambulas.
4 Sina furaha kubwa zaidi ya hii, kusikia kwamba watoto wangu wanatembea katika kweli.
Maiorem horum non habeo gratiam, quam ut audiam filios meos in veritate ambulare.
5 Mpendwa, unaenenda kwa uaminifu unapowahudumia ndugu na wageni,
Charissime, fideliter facis quidquid operaris in fratres, et hoc in peregrinos,
6 ambao wametoa ushuhuda wa upendo wako mbele ya kanisa. Unafanya vizuri kuwasafirisha katika safari zao kwa namna ambayo inampendeza Mungu.
qui testimonium reddiderunt charitati tuae in conspectu Ecclesiae: quos, benefaciens, deduces digne Deo.
7 Kwa sababu kwa ajili ya Jina, walienda bila kuchukua kitu chochote kutoka kwa watu wa Mataifa.
Pro nomine enim eius profecti sunt, nihil accipientes a Gentibus.
8 Hivyo, tunatakiwa kuwakaribisha watu kama hawa, ili tuwe watenda kazi wenza kwa ajili ya kweli.
Nos ergo debemus suscipere huiusmodi, ut cooperatores simus veritatis.
9 Nililiandikia kusanyiko jambo fulani, lakini Diotrofe, anayependa kuwa wa kwanza miongoni mwao, hakubaliani na sisi.
Scripsissem forsitan Ecclesiae: sed is, qui amat primatum gerere in eis, Diotrephes, non recipit nos.
10 Hivyo, kama nikija nitayakumbuka matendo yake anayoyafanya, jinsi anavyosema maneno mabaya kinyume nasi. Hajaridhika na matendo haya, yeye mwenyewe hawapokei ndugu. Hata huwakataza wengine ambao wanatamani kuwakaribisha hao ndugu na kuwafukuza watoke kwenye kusanyiko.
propter hoc si venero, commonebo eius opera, quae facit: verbis malignis garriens in nos: et quasi non ei ista sufficiant: neque ipse suscipit fratres: et eos, qui suscipiunt, prohibet, et de Ecclesia eiicit.
11 Mpenzi, usiige kilicho kibaya, bali iga kilicho chema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu; na yeye atendaye mabaya hajamwona Mungu.
Charissime, noli imitari malum, sed quod bonum est. Qui benefacit, ex Deo est: qui malefacit, non videt Deum.
12 Demetrio ameshuhudiwa na wote na kweli yenyewe. sisi pia ni mashahidi, na unajua kuwa ushahuhuda wetu ni wa kweli.
Demetrio testimonium redditur ab omnibus, et ab ipsa veritate, sed et nos testimonium perhibemus: et nosti quoniam testimonium nostrum verum est.
13 Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa kalamu na wino.
Multa habui tibi scribere: sed nolui per atramentum et calamum scribere tibi.
14 Bali ninatarajia kukuona hivi karibuni, na tutaongea nawe ana kwa ana. Amani iwe pamoja nawe. Marafiki wanakusalimu. Wasalimu marafiki kila mmoja kwa jina lake.
Spero autem protinus te videre, et os ad os loquemur. Pax tibi. Salutant te amici. Saluta tu amicos nominatim.