< 2 Timotheo 3 >
1 Lakini fahamu hili: katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati ngumu.
But know this: that in the last days, grievous times will come.
2 kwa sababu watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye majivuno, wenye dhihaka, wasiotii wazazi wao, wasiokuwa na shukurani na waovu.
For men will be lovers of self, lovers of money, boastful, arrogant, blasphemers, disobedient to parents, unthankful, unholy,
3 Wasio na upendo wa asili, wasiotaka kuishi kwa amani na yeyote, wachonganishi, wasingiziaji, wasioweza kujizuia, wenye vurugu, wasiopenda mema.
without natural affection, unforgiving, slanderers, without self-control, fierce, not lovers of good,
4 Watakuwa wasaliti, wakaidi, wenye kujipenda wenyewe na wapenda anasa kuliko kumpenda Mungu.
traitors, headstrong, conceited, lovers of pleasure rather than lovers of God,
5 Kwa nje watakuwa na sura ya ucha Mungu, lakini wataikana nguvu yake. Jiepushe na watu hao.
holding a form of godliness but having denied its power. Turn away from these, also.
6 Kwa kuwa baadhi yao ni wanaume wanaoingia kwenye familia za watu na kushawishi wanawake wajinga. Hawa ni wanawake waliojawa dhambi na wenye kuongozwa na tamaa za kila aina.
For some of these are people who creep into houses and take captive gullible women loaded down with sins, led away by various lusts,
7 Wanawake hawa hujifunza siku zote, lakini kamwe hawawezi kuufikia ufahamu wa ile kweli.
always learning and never able to come to the knowledge of the truth.
8 Kama vile ambavyo Yane na Yambre walisimama kinyume na Musa. Kwa njia hii walimu hawa wa uongo husimama kinyume na kweli. Ni watu walioharibiwa katika fikira zao, wasiokubalika kuhusiana na imani.
Even as Jannes and Jambres opposed Moses, so these also oppose the truth, men corrupted in mind, who concerning the faith are rejected.
9 Lakini hawataendelea mbali. Kwa kuwa upumbavu wao utawekwa wazi kwa watu wote, kama ulivyokuwa wa wale watu.
But they will proceed no further. For their folly will be evident to all men, as theirs also came to be.
10 Lakini wewe umeyafuata mafundisho yangu, mwenendo wangu, makusudi yangu, imani yangu, uvumilivu wangu, upendo wangu na ustahimilivu wangu,
But you followed my teaching, conduct, purpose, faith, patience, love, steadfastness,
11 mateso, maumivu na yaliyonipata kule Antiokia, Ikonio na Listra. Niliyavumilia mateso. Bwana aliniokoa katika yote hayo.
persecutions, and sufferings—those things that happened to me at Antioch, Iconium, and Lystra. I endured those persecutions. The Lord delivered me out of them all.
12 Wote wanaotaka kuishi katika maisha ya kumcha Mungu katika Kristo Yesu watateswa.
Yes, and all who desire to live godly in Christ Jesus will suffer persecution.
13 Watu waovu na wadanganyifu watazidi kuwa waovu zaidi. Watawapotosha wengine. Wao wenyewe wamepotoshwa.
But evil men and impostors will grow worse and worse, deceiving and being deceived.
14 Lakini wewe, dumu katika mambo uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti. Kwa kuwa unajua umejifunza kwa nani.
But you remain in the things which you have learned and have been assured of, knowing from whom you have learned them.
15 Unatambua ya kuwa tangu utotoni mwako uliyajua maandiko matakatifu. Haya yanaweza kukuhekimisha kwa ajili ya wokovu kwa njia ya imani katika kristo Yesu.
From infancy, you have known the holy Scriptures which are able to make you wise for salvation through faith which is in Christ Jesus.
16 Kila andiko limetiwa pumzi na Mungu. Linafaa kwa mafundisho yenye faida, kwa kushawishi, kwa kurekebisha makosa, na kwa kufundishia katika haki.
Every Scripture is God-breathed and profitable for teaching, for reproof, for correction, and for instruction in righteousness,
17 Hii ni kwamba mtu wa Mungu awe kamili, akiwa amepewa nyenzo zote kwa ajili ya kutenda kila kazi njema.
that each person who belongs to God may be complete, thoroughly equipped for every good work.