< 2 Samweli 5 >
1 Kisha kabila zote za Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni nao wakasema, “Tazama, sisi ni nyama na mifupa yako.
以色列众支派来到希伯 见大卫,说:“我们原是你的骨肉。
2 Kipindi kilichopita, Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, ni wewe uliyeliongoza jeshi la Waisraeli. Yahwe akakwambia, 'Utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala juu ya Israeli.”
从前扫罗作我们王的时候,率领以色列人出入的是你;耶和华也曾应许你说:‘你必牧养我的民以色列,作以色列的君。’”
3 Hivyo wazee wote wa Israeli wakaja kwa mfalme huko Hebron na mfalme Daudi akafanya nao agano mbele ya Yahweh. Wakamtawaza Daudi kuwa mfalme wa Israeli.
于是以色列的长老都来到希伯 见大卫王,大卫在希伯 耶和华面前与他们立约,他们就膏大卫作以色列的王。
4 Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala miaka arobaini.
大卫登基的时候年三十岁,在位四十年;
5 Alitawala juu ya Yuda miaka saba na miezi sit a huko Hebroni, na huko Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu juu ya Israeli yote na Yuda.
在希伯 作犹大王七年零六个月,在耶路撒冷作以色列和犹大王三十三年。
6 Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kupigana na wayebusi, waliokuwa wenyeji wa nchi. Wakamwambia Daudi, “Hautaweza kuja hapa kwani hata wipofu na vilema waweza kukudhuia kuingia. Daudi haweze kuja hapa.”
大卫和跟随他的人到了耶路撒冷,要攻打住那地方的耶布斯人。耶布斯人对大卫说:“你若不赶出瞎子、瘸子,必不能进这地方”;心里想大卫决不能进去。
7 Lakini, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, ambayo sasa ni mji wa Daudi.
然而大卫攻取锡安的保障,就是大卫的城。
8 Wakati huo Daudi akasema, “Waliowashambulia wayebusi watapaswa kupita katika mfereji wa maji ili wawafikie virema na vipofu ambao ni adui wa Daudi.” Hii ndiyo maana watu husema, “Vipofu na virema wasingie katika kasri.”
当日,大卫说:“谁攻打耶布斯人,当上水沟攻打我心里所恨恶的瘸子、瞎子。”从此有俗语说:“在那里有瞎子、瘸子,他不能进屋去。”
9 Hivyo Daudi akaishi ngemeni naye akaiita mji wa Daudi. Akaizungushia ukuta, kuanzia barazani kuelekea ndani.
大卫住在保障里,给保障起名叫大卫城。大卫又从米罗以里,周围筑墙。
10 Daudi akawa na nguvu sana kwa maana Yahwe, Mungu wa utukufu, alikuwa pamoja naye.
大卫日见强盛,因为耶和华—万军之 神与他同在。
11 Kisha Hiramu mfalme wa Tiro akatuma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, mafundi seremala na wajenzi. Wakamjengea Daudi nyumba.
泰尔王希兰将香柏木运到大卫那里,又差遣使者和木匠、石匠给大卫建造宫殿。
12 Daudi akatambua kuwa Yahwe alikuwa amemweka ili awe mfalme juu ya Israeli, na kwamba alikuwa ameutukuza ufalme wake kwa ajili ya Israeli watu wake.
大卫就知道耶和华坚立他作以色列王,又为自己的民以色列使他的国兴旺。
13 Baada ya Daudi kuondoka Hebroni na kwenda Yerusalemu, akajitwalia wake na masuria wengi huko Yerusalemu, na wana na binti wengi walizaliwa kwake.
大卫离开希伯 之后,在耶路撒冷又立后妃,又生儿女。
14 Haya ndiyo majina ya wanawe waliozaliwa kwake huko Yerusalemu: Shamua, Shobabu, Nathani, Selemani,
在耶路撒冷所生的儿子是沙母亚、朔罢、拿单、所罗门、
15 Ibhari, Elishua, Nefegi, Yafia,
益辖、以利书亚、尼斐、雅非亚、
16 Elishama, Eliada na Elifeleti.
以利沙玛、以利雅大、以利法列。
17 Basi wafilisti waliposikia kwamba Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli, wakaenda wote kumtafuta. Daudi aliposikia hilo akashuka ngomeni.
非利士人听见人膏大卫作以色列王,非利士众人就上来寻索大卫;大卫听见,就下到保障。
18 Basi Wafilisiti walikuwa wamekuja na kuenea katika bonde la Mrefai.
非利士人来了,布散在利乏音谷。
19 Kisha Daudi akaomba msaada kutoka kwa Yahwe. Akasema, “Je niwashambulie wafilisti? Je utanipa ushindi juu yao?” Yahwe akamwambia Daudi, “Washambulia, kwa hakika nitakupa ushindi juu ya wafilisti.”
大卫求问耶和华说:“我可以上去攻打非利士人吗?你将他们交在我手里吗?”耶和华说:“你可以上去,我必将非利士人交在你手里。”
20 Hivyo Daudi akawashambulia huko Baali Perasimu, naye akawashinda. Akasema, Yahwe amewafurikia adui zangu mbele yangu kama mafuriko ya maji. Kwa hiyo jina la mahali pale likawa Baali Perasimu.
大卫来到巴力·毗拉心,在那里击杀非利士人,说:“耶和华在我面前冲破敌人,如同水冲去一般。”因此称那地方为巴力·毗拉心。
21 Wafilisiti wakaacha vinyago vyao pale, na Daudi na watu wake wakaviondoa.
非利士人将偶像撇在那里,大卫和跟随他的人拿去了。
22 Kisha wafilisiti wakaja kwa mara nyingine tena na kujieneza zaidi katika bonde la Mrefai.
非利士人又上来,布散在利乏音谷。
23 Hivyo Daudi akatafuta msaada tena kutoka kwa Yahweh, naye Yahweh akamwambia, “Usiwashambulie kwa mbele, lakini uwazunguke kwa nyuma na uwaendee kupitia miti ya miforosadi.
大卫求问耶和华;耶和华说:“不要一直地上去,要转到他们后头,从桑林对面攻打他们。
24 Wakati utakaposikia sauti za mwendo katika upepo uvumao juu ya miti ya miforosadi, hapo ushambulie kwa nguvu. Fanya hivi kwa kuwa Yahwe atatangulia mbele yako kulishambulia jeshi la Wafilisiti.”
你听见桑树梢上有脚步的声音,就要急速前去,因为那时耶和华已经在你前头去攻打非利士人的军队。”
25 Hivyo Daudi akafanya kama Yahwe alivyomwamuru. Akawaua wafilisti njiani mwote toka Geba hadi Gezeri.
大卫就遵着耶和华所吩咐的去行,攻打非利士人,从迦巴直到基色。