< 2 Samweli 4 >

1 Ikawa Ishboshethi, mwana wa Sauli, aliposikia kwamba Abneri amekufa huko Hebroni, mikono yake ikadhoofika, na Israeli yote ikataabika.
And Jebosthe the son of Saul heard that Abenner the son of Ner had died in Chebron; and his hands were paralyzed, and all the men of Israel grew faint.
2 Basi mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili waliokuwa wakuu wa vikosi vya askari. Mmoja wao alikuwa Baana na mwingine alikuwa Rekabu, wana wa Rimoni Mbeerothi wa wana wa Benjamini(kwa maana Berothi ilihesabiwa kuwa sehemu ya Benjamini,
And Jebosthe the son of Saul had two men that were captains of bands: the name of the one [was] Baana, and the name of the other Rechab, sons of Remmon the Berothite of the children of Benjamin; for Beroth was reckoned to the children of Benjamin.
3 na Waberothi walikimbilia Gitaimu na wamekuwa wakiishi pale hadi sasa).
And the Berothites ran away to Gethaim, and were sojourners there until this day.
4 Basi Yonathani, mwana wa Sauli, alikuwa na mwana mlemavu wa miguu. Alikuwa na umri wa miaka mitano habari kuhusu Sauli na Yonathani ilipofika Yezreeli. Yaya wake akamchukua ili akimbie. Lakini wakati anakimbia, mwana wa Yonathani alianguka na akawa kirema. Jina lake aliitwa Mefiboshethi.
And Jonathan Saul's son [had] a son lame of his feet, five years old, and he was [in the way] when the news of Saul and Jonathan his son came from Jezrael, and his nurse took him up, and fled; and it came to pass as he hasted and retreated, that he fell, and was lamed. And his name [was] Memphibosthe.
5 Hivyo wana wa Rimoni mbeerothi, Rekabu na Baana, wakasafiri mchana wakati wa jua kali mpaka nyumbani mwa Ishbothethi, yeye alikuwa amepumzika mchana.
And Rechab and Baana the sons of Remmon the Berothite went, and they came in the heat of the day into the house of Jebosthe; and he was sleeping on a bed at noon.
6 Mwanamke aliyekuwa akililinda lango alisinzia wakati akipepeta ngano, Rekabu na Baana waliingia ndani polepole na wakampita.
And, behold, the porter of the house winnowed wheat, and he slumbered and slept: and the brothers Rechab and Baana went privily into the house:
7 Hivyo walipoingia ndani ya nyumba, walimpiga na kumuua wakati amelala chumbani mwake. Kisha wakakata kichwa chake na wakaondoka nacho, wakasafiri njiani usiku kucha mpaka Araba.
And Jebosthe was sleeping on his bed in his chamber: and they strike him, and kill him, and take off his head: and they took his head, and went all the night by the western road.
8 Wakaleta kichwa cha Ishboshethi kwa Daudi huko Hebroni, nao wakamwambia mfalme, “Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi mwana wa Sauli, adui yako, aliyekuwa akiutafuta uhai wako. Leo Yahwe amemlipia kisasi bwana wetu mfalme dhidi ya Sauli na uzao wake.”
And they brought the head of Jebosthe to David to Chebron, and they said to the king, Behold the head of Jebosthe the son of Saul your enemy, who sought your life; and the Lord has executed for my lord the king vengeance on his enemies, as [it is] this day: even on Saul your enemy, and on his seed.
9 Daudi akawajibu Rekabu na Baana nduguye, wana wa Rimoni mbeerothi, akawambia, “Kama Yahwe aishivyo, aliyeuokoa uhai wangu na kila shida,
And David answered and Rechab and Baana his brother, the sons of Remmon the Berothite, and said to them, [As] the Lord lives, who has redeemed my soul out of all affliction;
10 mtu mmoja aliponiambia, 'Tazama, Sauli amekufa,' akifikiri alileta habari njema, nilimkamata na kumwua huko Siklagi. Huo ndio ujira niliompa kwa habari yake.
he that reported to me that Saul was dead, even he was as one bringing glad tidings before me: but I seized him and killed him in Sekelac, to whom I ought, [as he thought], to have given a reward for his tidings.
11 Namna gani, mtu mwovu anapomwua mwenye haki kitandi mwake ndani ya nyumba, Je nisiitake damu yake kutoka katika mikono yenu, na kuwaondoa duniani?”
And now evil men have slain a righteous men in his house on his bed: now then I will require his blood of your hand, and I will destroy you from off the earth.
12 Kisha Daudi akawaagiza vijana, nao wakawaua wakakata mikono na miguu yao na kuwatundika kando ya bwawa huko Hebroni. Lakini wakakichukua kichwa cha Ishboshethi na kukizika katika kaburi la Abneri katika Hebroni.
And David commanded his young men, and they kill them, and cut off their hands and their feet; and they hung them up at the fountain in Chebron: and they buried the head of Jebosthe in the tomb of Abenezer the son of Ner.

< 2 Samweli 4 >