< 2 Samweli 24 >

1 Kisha hasira ya Yahwe ikawaka dhidi ya Israeli, naye akamchochea Daudi kinyume chao kusema, “Nenda, ukawahesabu Israeli na Yuda.”
耶和華又向以色列人發怒,就激動大衛,使他吩咐人去數點以色列人和猶大人。
2 Mfalme akamwambia Yoabu, jemedari wa jeshi, aliyekuwa pamoja naye, “Nenda upite katika kabila zote za Israeli, toka Dani mpaka Beersheba, uwahesabu watu wote, ili niweze kujua idadi kamili ya watu wanaofaa kwa vita.”
大衛就吩咐跟隨他的元帥約押說:「你去走遍以色列眾支派,從但直到別是巴,數點百姓,我好知道他們的數目。」
3 Yoabu akamwambia mfalme, “Yahwe Mungu wako na aizidishe hesabu ya watu mara mia, na macho ya bwana wangu mfalme yaone ikifanyika. Lakini kwa nini bwana wangu mfalme analitaka jambo hili?
約押對王說:「無論百姓多少,願耶和華-你的上帝再加增百倍,使我主我王親眼得見。我主我王何必喜悅行這事呢?」
4 Walakini neno la mfalme lilikuwa la mwisho dhidi ya Yoabu na dhidhi ya majemedari wa jeshi. Hivyo Yoabu na majemedari wakatoka mbele ya mfalme kuwahesabu watu wa Israeli.
但王的命令勝過約押和眾軍長。約押和眾軍長就從王面前出去,數點以色列的百姓。
5 Wakavuka Yordani na kupiga kambi karibu na Aroeri, kusini mwa mji bondeni. Kisha wakasafiri kupitia Gadi mpaka Yazeri.
他們過了約旦河,在迦得谷中、城的右邊亞羅珥安營,與雅謝相對,
6 Wakaja Gileadi na nchi ya Tahtimu Hodshi, kisha Dani, Jaani na karibu kuelekea Sidoni.
又到了基列和他停‧合示地,又到了但‧雅安,繞到西頓,
7 Wakafika ngome ya Tiro na miji yote ya Wahivi na Wakanaani. Kisha wakaenda Negebu katika Yuda huko Beersheba.
來到泰爾的保障,並希未人和迦南人的各城,又到猶大南方的別是巴。
8 Walipokuwa wamepita katika nchi yote, wakarejea Yerusalemu mwishoni mwa miezi tisa na siku ishirini.
他們走遍全地,過了九個月零二十天,就回到耶路撒冷。
9 Ndipo Yoabu alipotoa taarifa ya hesabu kamili kwa mfalme kuhusu watu wawezao kupigana vita. Katika Israeli kulikuwa na watu 800, 000 jasiri wawezao kutoa upanga, na wale wa Yuda walikuwa watu 500, 000.
約押將百姓的總數奏告於王:以色列拿刀的勇士有八十萬;猶大有五十萬。
10 Ndipo moyo wa Daudi ukamchoma alipokuwa amewahesabu watu. Hivyo akamwambia Yahwe, “Kwa kufanya hivi nimetenda dhambi sana. Sasa, Yahwe, uiondoe hatia ya mtumishi wako, kwani nimetenda kwa upumbavu.”
大衛數點百姓以後,就心中自責,禱告耶和華說:「我行這事大有罪了。耶和華啊,求你除掉僕人的罪孽,因我所行的甚是愚昧。」
11 Daudi alipoinuka asubuhi, neno la Yahwe likamjia nabii Gadi, mwonaji wa Daudi, kusema,
大衛早晨起來,耶和華的話臨到先知迦得,就是大衛的先見,說:
12 Nenda umwambie Daudi; 'Hivi ndivyo asemavyo Yahwe: “Ninakupa mambo matatu. Uchague mojawapo.”
「你去告訴大衛,說耶和華如此說:『我有三樣災,隨你選擇一樣,我好降與你。』」
13 Hivyo Gadi akaenda kwa Daudi na kumwambia, “Je miaka mitatu ya njaa ije katika nchi yako? au miezi mitatu ukimbie kutoka kwa adui zako huku wakikufuatia? au kuwe na tauni ya siku tatu katika nchi yako? Amua sasa jibu gani nimrudishie aliyenituma.”
於是迦得來見大衛,對他說:「你願意國中有七年的饑荒呢?是在你敵人面前逃跑,被追趕三個月呢?是在你國中有三日的瘟疫呢?現在你要揣摩思想,我好回覆那差我來的。」
14 Ndipo Daudi alipomwambia Gadi, “Nipo katika shida kubwa. Haya na tuanguke katika mikono ya Yahwe kuliko kuanguka katika mikono ya mwanadamu, kwani matendo yake ya rehema ni makuu sana.”
大衛對迦得說:「我甚為難!我願落在耶和華的手裏,因為他有豐盛的憐憫。我不願落在人的手裏。」
15 Hivyo akatuma tauni juu ya Israeli kuanzia asubuhi kwa muda ulioamriwa, na watu sabini na tano elfu kutoka Dani mpaka Beersheba wakafa.
於是,耶和華降瘟疫與以色列人,自早晨到所定的時候;從但直到別是巴,民間死了七萬人。
16 Malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili kuuharibu, Yahwe akabadili nia yake kuhusu madhara, na akamwambia malaika aliyekuwa tiyari kuwaangamiza watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako sasa.” Wakati huo malaika wa Yahwe alikuwa amesimama katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.
天使向耶路撒冷伸手要滅城的時候,耶和華後悔,就不降這災了,吩咐滅民的天使說:「夠了!住手吧!」那時耶和華的使者在耶布斯人亞勞拿的禾場那裏。
17 Daudi alipomwona malaika aliyekuwa amewapiga watu, akamwambia Yahwe kusema, “Nimetenda dhambi, na nimetenda kwa upumbavu. Lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Tafadhari, mkono wako na uniadhibu mimi na familia ya baba yangu!”
大衛看見滅民的天使,就禱告耶和華說:「我犯了罪,行了惡;但這群羊做了甚麼呢?願你的手攻擊我和我的父家。」
18 Kisha Gadi akaja siku hiyo kwa Daudi na kumwambia, “Kwea na ujenge madhabahu kwa ajili ya Yahwe katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.”
當日,迦得來見大衛,對他說:「你上去,在耶布斯人亞勞拿的禾場上為耶和華築一座壇。」
19 Hivyo Daudi akakwea kama Gadi alivyomwelekeza kufanya, kama Yahwe alivyokuwa ameagiza.
大衛就照着迦得奉耶和華名所說的話上去了。
20 Arauna akatazama na kumwona mfalme na watumishi wake wakikaribia. Ndipo Arauna akaondoka na kumsujudia mfalme uso wake mpaka juu ya ardhi.
亞勞拿觀看,見王和他臣僕前來,就迎接出去,臉伏於地,向王下拜,
21 Kisha Arauna akasema, “Kwa nini bwana wangu mfalme amekuja kwangu, mtumishi wake? Daudi akajibu, “Kununua uwanja wako wa kupuria, ili nimjengee Yahwe madhabahu, ili kwamba tauni iondolewe kwa watu.”
說:「我主我王為何來到僕人這裏呢?」大衛說:「我要買你這禾場,為耶和華築一座壇,使民間的瘟疫止住。」
22 Arauna akamwambia Daudi, “Chukua liwe lako, bwana wangu mfalme. Ulifanyie lolote lolote lililojema machoni pako. Tazama, ng'ombe kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na miganda ya kupuria na nira kwa kuni.
亞勞拿對大衛說:「我主我王,你喜悅用甚麼,就拿去獻祭。看哪,這裏有牛可以作燔祭,有打糧的器具和套牛的軛可以當柴燒。
23 Haya yote bwana wangu mfalme, mimi Arauna nakupa.” Kisha akamwambia mfalme, “Yahwe Mungu wako na awe nawe.”
王啊,這一切,我亞勞拿都奉給你」;又對王說:「願耶和華-你的上帝悅納你。」
24 Mfalme akamwambia Arauna, “Hapana, nahimiza kukinunua kwa thamani yake. Sitatoa kama sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe chochote nisichokigharimia.” Hivyo Daudi akakinunua kiwanja cha kupuria na ng'ombe kwa shekeli hamsini za fedha.
王對亞勞拿說:「不然。我必要按着價值向你買;我不肯用白得之物作燔祭獻給耶和華-我的上帝。」大衛就用五十舍客勒銀子買了那禾場與牛。
25 Daudi akajenga madhabahu kwa Yahwe pale na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Hivyo wakamsihi Yahwe kwa niaba ya nchi, hivyo akaizuia tauni katika katika Israeli yote.
大衛在那裏為耶和華築了一座壇,獻燔祭和平安祭。如此,耶和華垂聽國民所求的,瘟疫在以色列人中就止住了。

< 2 Samweli 24 >